Bomani awashukia wanaobeza kazi ya Tume ya Warioba

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
JAJI mstaafu Mark Bomani, ameeleza kushangazwa na kuhuzunishwa na kauli za baadhi ya viongozi, miongoni mwao wakiwamo anaowaheshimu kuhusu kupinga mapendekezo ya serikali tatu yaliyomo katika rasimu ya pili ya katiba.

Amesema lawama wanazotoa juu ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba haina mashiko, kwani alichowasilisha ni mapendekezo ya tume iliyokuwa na wajumbe wenye kuheshimika na wenye uzoefu katika masuala ya utawala, wakiwa sawia kutoka Zanzibar na Tanzania Bara.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, alisema anafadhaishwa kusikia Wana CCM kulishana kiapo ili kupinga serikali tatu.

Jaji Warioba si mwanzilishi wa serikali tatu. Wa kwanza katika viongozi wa kitaifa alikuwa Aboud Jumbe, akiwa Rais wa Zanzibar mwaka 1984mwaka 1991 tume maalumu yenye mchanganyiko ya wajumbe kutoka Zanzibar na Tanzania Bara chini ya Mwenyekiti Jaji Nyalali ilipendekeza Serikali tatu na mwaka 1998 iliundwa kamati chini ya Jaji Kisanga ilitoa mapendekezo hayo ambayo yalitupwa mbali na kwa kejeli kubwa.

Jaji Warioba mwaka 1985 aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais. Nafasi hiyo aliyopewa ilikuwa inampa fursa kubwa sana ya kupenyeza ajenda ya serikali tatu kama angependa. Hakufanya hivyo.

Vipi leo alaumiwe kwa jambo ambalo wala hakulianzisha?
Nikisikia kitu kama Wana CCM kulishana kiapo ili wapinge serikali tatu nafadhaishwa sana. Haya yote ya nini? Waacheni wanachama wenu waamue kile wanachokitaka, alisema Jaji Bomani ambaye ana uzoefu juu ya masuala ya Katiba.

Alisema alihusika na uandaaji wa Katiba ya Namibia mwaka 1990 na Katiba ya Burundi mwaka 2000.
Jaji Bomani alisema anaipongeza tume ya Jaji Warioba kwa kuandaa rasimu ya Katiba, kwani imefanya kazi nzuri juu ya suala zito na gumu, pia alimpongeza Rais Kikwete na Rais wa Zanzibar kwa ukomavu walioonyesha katika kupokea rasimu hiyo.

Pamoja na hayo, Jaji Bomani alishauri kutokana na upungufu wa fedha, uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu uhairishwe hadi mwakani, ili fedha hizo zitumike kuboresha daftari la wapiga kura.

Chanzo Tanzania daima
 
Safi sana Jaji Bomani kwa kusema ukweli, hata jana kwenye kipima joto ITV kuna genge la wahuni liliandaliwa kumdharirisha Warioba bila kujali kazi nzuri yote aliyoifanya katika Rasimu hii ya katiba
 
''' Mwanasheria mkuu mstaafu , jaji Mark Bomani amekitaka Chama cha Mapinduzi (CCM) kuachana na muundo wake wa serikali mbili na kwamba , wawaachie wananchi waamue.

Pia Jaji Bomani alisema anasikitishwa na madai yanayoelekezwa na baadhi ya viongozi ,tena anaowaheshimu kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba ,Jaji Joseph Warioba ni muumini wa Serikali Tatu na kwamba ni upuuzi, kwani yeye sio wa kwanza kutaja muundo huo.

Licha ya hilo, alisema anashangazwa na baadhi ya viongozi kuwa rasimu imekwenda kinyume cha matakwa ya waasisi wa Tanzania na kwamba, kama hali inalazimu kubadili uamuzi unafanyika.

Akitoa maoni yake kuhusu Rasimu ya pili ya katiba, Jaji Bomani alisema licha ya kwamba yeye ni mwana CCm, anaona Serikali tatu ni muhimu kwani ndiyo suluhisho la migogoro ua Muungano....'Mwisho wa kunukuu'''

Mimi napenda kumsifu Jaji Bomani kwa kuweka wazi ukweli wa mambo na pia kuonyesha hisia zake kwa mfumo wa Serikali tatu kama ilivyo kwa watanzania walio wengi.:A S thumbs_up:

Source: Mwananchi, Januari 24,2014.
 
Back
Top Bottom