Bomani ataka mjadala wa Katiba usiwe wa pupa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bomani ataka mjadala wa Katiba usiwe wa pupa

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Rutashubanyuma, Jan 11, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,846
  Trophy Points: 280
  Bomani ataka mjadala wa Katiba usiwe wa pupa

  Imeandikwa na Grace Chilongola, Magu; Tarehe: 10th January 2011 @ 23:50 Imesomwa na watu: 221; Jumla ya maoni: 0
  JAJI mstaafu Mark Bomani ametaka mabadiliko ya katiba yafanyike kwa amani na utulivu na kuepuka pupa ambayo inaweza kulitumbukiza Taifa katika vurugu.

  Alisema kwa kuwa katiba sio Biblia wala Msaafu kwa kuwa inaweza kubadilishwa, lakini akataka mabadiliko hayo yaepuke vurugu.

  Alisema hayo mwishoni mwa wiki katika kijiji cha Mwamanyili wilayani Magu, mkoani Mwanza katika hafla ya kupongezwa kwa familia yake kwa kufanikisha ujenzi wa Kanisa la Wasabato (SDA).

  Bomani alitumia nafasi hiyo kuwatahadharisha wanasiasa na Watanzania kwa ujumla, kudai mabadiliko hayo kwa njia ya amani na utulivu, ili kuepusha nchi na machafuko yanayoweza kujitokeza.

  Alisema jamii inahitaji katiba mpya lakini madai hayo yasitumiwe kisiasa na kuielekeza nchi katika janga la machafuko na kuwataka wanaodai mabadiliko hayo, kuketi na serikali kujadiliana, ili wafikie makubaliano ya nini kifanyike.

  Jaji Bomani alisema njia pekee ya kuepukana na machafuko, ni kukutana mezani na kuzungumza ili muafaka upatikane na kuondoa uwezekano wa kuzuka kwa vurugu.

  “Katiba mpya inapaswa kupatikana, lakini tuzingatie umoja wetu na tuulinde katika kipindi hiki cha kudai mabadiliko hayo, alisema Bomani.

  Kuhusu uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete wa kuunda Tume alisema ni njia ya kufikia mabadiliko ya Katiba na kuongeza kuwa hata mjadala wa bungeni pia ni njia sahihi na kwamba hali hiyo inaonyesha mitazamo tofauti yenye lengo moja.

  Alifafanua kwamba njia ya kuunda Tume inaweza kuwa bora zaidi kutokana na ukweli kuwa ndiyo njia pekee inayowashirikisha wananchi wote kwa makundi na vipindi tofauti.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,846
  Trophy Points: 280
  Huyu mzee kwa kweli amechoka hata haelewi tofauti ya tume ya Raisi na Mkutano wa kikatiba mbao wajumbe wake wamechaguliwa na wapigakura............Vile vile hajajibu hoja za kimsingi ya kuwa ni kwa nini Tume ya Raisi huko nyuma zilizochangia hadi tukapa viraka 14 kwenye katiba hazijaweza kukidhi mahitaji ya taifa hili...............
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mzee Bomani, swala la katiba mpya kwa zaidi ya miaka 50 ya uhuru na 20 ya kudai mabadiliko bado unaona PUPA fulani hapo?

  Tafadhali kapumzike mzee wetu, katiba na ratiba yake tutaisimamia wenyewe wananchi bila kuletewa zengwe lolote la madalali safari hii kutuandikia tena katiba, tume mpya ya uchaguzi na tume ya bunge ya kuchunguza matokeo ya uchaguzi wa rais 2010.
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,846
  Trophy Points: 280
  Bomani: Mabadiliko ya katiba yasivuruge nchi Monday, 10 January 2011 21:02

  Frederick Katulanda, Magu

  JAJI Mstaafu, Mark Bomani ametaka Wanasiasa na Watanzania kudai mabadiliko ya Katiba kwa njia ya amani, upendo na utulivu ili kuiepusha nchi na machafuko.

  Alisema kuwa Katiba inaweza kubadilishwa kwa vile siyo msaafu wa Biblia lakini akasema mabadiliko hayo yafanyike kwa amani na utulivu na kuepuka pupa ambayo inaweza kulitumbukiza Taifa katika vurugu kama zile za uchaguzi wa Umeya Arusha.

  Jaji Bomani alisema hayo juzi, wilayani Magu katika Kijiji cha Mwamanyili katika hafla ya kupongezwa kwa familia yake kufanikisha ujenzi wa Kanisa la Seventh Day Adventist (SDA) iliyohudhuria pia na Askofu Joseph Bulengela wa Dayosisi ya Nyanza, Mbunge wa Jimbo la Busega Dk Titus Kamani, mkewe Bomani Rahma Bakari Mwapachu pamoja na watoto wake wawili.

  Alisema wote wanahitaji katiba mpya, lakini madai ya kuwepo kwa katiba hiyo, yasitumiwe kisiasa kuigeuza nchi kuingia katika janga la machafuko na kuwataka wanaodai mabadiliko hayo kukaa pamoja na serikali kuzungumza ili waweze kufikia makubaliano ya nini kifanyike katika mabadiliko hayo.

  Akizungumzia uamuzi wa Rais Kikwete kuamua kuunda kamati ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Bomani alisema kuwa hiyo ni njia ya kufikia mabadiliko ya Katiba na kusema hata njia ya wanaotaka mabadiliko ya katiba yaanzie kujadiliwa Bungeni pia ni njia sahihi na hali hii inaonyesha mitazamo tofauti yenye lengo moja.

  Aidha Jaji Bomani alisema kuwa njia ya kamati inaweza kuwa bora zaidi kutokana na ukweli kuwa ndiyo njia pekee inayoweza kuwasikiliza wananchi wote kwa makundi na vipindi tofauti na pia kupitia mapendekezo ya zamani ya mabadiliko ya katiba ambayo yaliainisha zamani.

  "Mie sioni tatizo kwa njia zote za kuleta mabadiliko, kwangu njia siyo hoja, hoja ni mabadiliko hayo kukidhi haja na matakwa ya wengi. Katiba mpya inapaswa kupatikana, lakini tuzingatie umoja wetu na tuulinde katika kipindi hiki cha kudai mabadiliko hayo," alieleza Jaji Bomani.

  Alisema kwa muda sasa nchi imeanza kuingia katika mivutano ya kisiasa na kusema vurugu za Arusha za umeya zinatosha kuwa onyo na kielelezo cha kufungua milango ya majadiliano ili kujenga utamaduni na mazoea ya kuzungumza kwa pamoja na kufikia muafaka.

  Alisema njia pekee ya kuepuka machafuko ni kukutana mezani na kuzungumza na kurejea onyo lake kuwa iwapo katika mabadiliko ya katiba hawatakutana na kukubaliana kwa pamoja basi upo uwezekano wa kuzuka kwa vurugu.
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,846
  Trophy Points: 280
  Mzee wetu Bomani unasikia busara na utashi huu?
   
 6. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #6
  Jan 17, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Bomani kwishachoka ile
   
 7. m

  mian Member

  #7
  Jan 18, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hana jipya anahesabu siku tu...atuachie tanzania yetu...hatuna muda huo vijana wakuendelea kushangaa shangaa mmekula za kutosha..
  nawashauri mkubali sasa kabla hasira hazijawa nyingi plus chuki..
   
Loading...