Bollen Ngetti: Nini hasa kilichonitokea...

Mwemary

JF-Expert Member
May 25, 2016
330
340
WHAT REALLY HAPPENED TO ME

Na Bollen Ngetti

ILIKUWA ni majira ya saa 4:27 usiku wa 8/8 nikiwa ndani ya FQ Hotel na marafiki zangu pamoja na mmiliki wa hoteli tajwa tukibadilishana mawazo. Hoteli ilivyo ina geti moja ya kutokea.

Niliwaaga wenzangu kwamba ninaondoka. Kimsingi si kwenda nyumbani bali kubadilisha mazingira baada ya mdogo wangu kuniomba tukutane River side Hotel jirani na Tabata.

Nilipotoka tu getini nikakutana na maaskari watatu wote wamesheheni silaha za SMG wakaniambia niko chini ya ulinzi ninahitajika kwa mahojiano. Niliuliza mahojiano ya nini? Sikujibiwa zaidi ya kukamatwa na kutupwa ndani ya difenda na kuondoka. Kauli ya "hatimaye umenasa" ilitawala midomo yao jambo lililonitia hofu sana.

Ni maeneo ya Njiapanda ya Segerea lakini safari ikaelekea Gongo la Mboto. Ghafla baada ya simu zao za "ova" ova safari ikageuka kurudi kituo cha Stakishari. Tukiwa kituoni niliingizwa ndani bila kuandikwa kwenye kumbukumbu yoyote na hata ndugu waliofuatilia safari hizi toka mwanzo akiwemo mmiliki wa FQ Hotel walifurushwa kituoni hapo.

Kila nilipotaka nichukuliwe maelezo niliambiwa, "wewe si mkosoaji maarufu? Sasa kosoa leo " nikaanza kujua kinachoendelea lakini nikiwa nimekata tamaa kabisa.

Ghafla lilikuja gari lingine na askari wengine na nikaamriwa kuingia kwenye gari hilo tukaondoka. Tulienda mbali sana ila sijui ni wapi maana nilipokaa ndani ya gari haikuwa rahisi kusoma alama za barabarani lakini ni ndani ya Ilala. Ndipo kupitia hayo ma-ova ova ikaelekezwa nipelekwe Buguruni.

Bado niliendelea kuomba niambiwe kosa langu lakini sikuambiwa bado zaidi ya vitisho. Nikaulizwa kama ninamiliki akaunti hii nikawaambia naam. Nikaulizwa nitaacha lini ukosoaji sikujibu. Nikaoneshwa baadhi ya posts zangu za nyuma ambazo kiukweli ni za ukosoaji pia sikujibu. Nikaomba kujua nashikiliwa kwa kosa gani kimsingi? Nikaambiwa, "matumizi mabaya ya mtandao". Yepi? Sikujibiwa na nikaachwa!

Ghafla nikaambiwa umemtukana mkeo. Nikauliza mke wangu yupi? Akatajwa " mtaliki" wangu Highness Koka (si mbunge). Nikahoji, amekuja kulalamika? Nikaambiwa, hapana lakini tunafuatilia matumizi yote ya mitandao. Nikakosa jibu. Hapo pia nikaachwa pending!

Baada ya masaa 3 akaingia askari na mtaliki wangu. Hatukuzungumza chochote zaidi ya kuulizwa mbona haupeleki hela za matumizi kwa mtoto? Kesi ikabadilika. Mtaliki akatoweka na yule askari.

Ndugu zangu, mimi ni mtu mzima mwenye akili timamu na makini. Ni dhahiri kesi haikuwepo na sasa ilitafutwa mbinu yoyote ya kunitia hatiani. Ni mpango wa muda mrefu baada ya mimi kushinda ile kesi yangu ya uchochezi.

Kipekee kabisa niwashukuru wote mliopiga kelele na kutaka niachiwe. Siwezi kuwataja kwa majina maana mko wengi. Nimejifunza upendo mkubwa kutoka kwenu. Namshukuru Zitto Kabwe kwa kutoa taarifa hii na hivyo kusambaa kwa haraka. Kumbe kupitia matatizo mtu unaweza kutambua thamani yako katika jamii. Nimejifunza.

Kipekee ninashukuru jopo la Mawakili wasomi kutoka THRDC wakiongozwa na Jones Sendodo walionitafuta vituoni hadi kunikuta Buguruni na kusimamia show mwanzo mwisho hadi kuhakikisha ninaachiwa kwa dhamana. Ahsanteni sana. Nashukuru Bondia maarufu nchini Mada Maugo kwa kushirikiana na mawakili hao kunitafutia haki. Lakini pia siwezi kumsahau Kamanda Msangi kwa weledi aliouonesha.

Nitakosea sana nisipowashukuru EU na Ubalozi wa Marekani kwa statement yao waliyoitoa kwa kadhia hii iliyokuwa chachu ya mimi kuachiwa. Viongozi wa dini mliokuja kunifariji na wengine kusema nawashukuru sana.

Nakushukuru pia Mhe Bernard Membe kwa kukosa usingizi ukifuatilia kwa karibu tukio zima kwa macho ya kikachero. Mwisho na kipekee nikushukuru Mwenyekiti wangu wa chama Ndugu John Magufuli, salamu zako nilizipata.

Jambo moja niliseme kwamba Maagi Mulaga hakuna vita hats moja utakayoshinda. Watanzaniq wameshaamua kufanya mabadiliko 2020. Hakuna namna zaidi ya kuyaunga mkono mabadiliko hayo. Huu ni mlipo ambao haujawahi kutoka Tanzania. Tuyaunge mkono, no way out. Nawatakia Jumamosi Njema. Ahsante ni.
Bollen Ngetti (Mbunge Nje ya Bunge)
10/8/2019
 
Ndugu zangu, mimi ni mtu mzima mwenye akili timamu na makini. Ni dhahiri kesi haikuwepo na sasa ilitafutwa mbinu yoyote ya kunitia hatiani. Ni mpango wa muda mrefu baada ya mimi kushinda ile kesi yangu ya uchochezi.

Kipekee kabisa niwashukuru wote mliopiga kelele na kutaka niachiwe. Siwezi kuwataja kwa majina maana mko wengi. Nimejifunza upendo mkubwa kutoka kwenu. Namshukuru Zitto Kabwe kwa kutoa taarifa hii na hivyo kusambaa kwa haraka. Kumbe kupitia matatizo mtu unaweza kutambua thamani yako katika jamii. Nimejifunza.

Kipekee ninashukuru jopo la Mawakili wasomi kutoka THRDC wakiongozwa na Jones Sendodo walionitafuta vituoni hadi kunikuta Buguruni na kusimamia show mwanzo mwisho hadi kuhakikisha ninaachiwa kwa dhamana. Ahsanteni sana. Nashukuru Bondia maarufu nchini Mada Maugo kwa kushirikiana na mawakili hao kunitafutia haki. Lakini pia siwezi kumsahau Kamanda Msangi kwa weledi aliouonesha.

Nitakosea sana nisipowashukuru EU na Ubalozi wa Marekani kwa statement yao waliyoitoa kwa kadhia hii iliyokuwa chachu ya mimi kuachiwa. Viongozi wa dini mliokuja kunifariji na wengine kusema nawashukuru sana.

Wema ni bima ya maisha
 
Maagi mulaga ndio nani?. Hiyo haya ya mwisho ndio imenichanganya kabisaaa, ni nani tena alitaka kukuulimboka wakati unaunga mkono juhudi za mwenyekiti?.
 
Mimi nimependa tu kwenye hizo shukrani zako ulizotoa! Yaani hujaonesha kabisa dalili za ubaguzi. Umewashukuru wote na kwa upendo mkubwa. Hadi kamanda wetu Ahmed Msangi, Membe, Magufuli, Zitto, Mbunge halisi wa Rorya Mada Maugo, nk.

Ila kwenye suala la matumizi kwa mtoto wako ilifanyie kazi aisee! Peleka hela ya matumizi bhana hata kama umetalikiana na mama yake! maana huo ndiyo uanaume. Lazima uwajibike.
 
Hiyo paragraph ya mwisho inaoneaha nini kinaendelea, kumbe yanayosemwa huenda yakawa kweli, Mr President huenda ukawa ndio mwisho wake ikulu2020.
Acha ndoto za alinacha, hivi huyu akitoka nani wa kuvaa viatu vyake?
 
Back
Top Bottom