Bollen Ngeti: Hili nalo ni jaribio la kumuua Lissu?

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
MIMI si Muislamu lakini sasa naanza kuamini katika imani hii. Baada ya Tundu Lissu kushambuliwa na watu wasiojulikana Wazee wa Kiislamu Pemba, Unguja, Tanga, Bwagamoyo na Dar es salaam walisoma kinachoitwa "al-badir". Ninaambiwa ikisomwa hii basi aliyetenda jambo la unyama kwa siri wanapatwa na madhara. Wanaweweseka, wanaweza kuongea wenyewe kama vichaa, na wengine wanaweza hata kujiua au kuumbuka. Kwa mbali na karibu naona dalili za matokeo ya "al-badir".

Imenichukua muda kuamini macho yangu na masikio yangu. Nimetafakari na kujiuliza hatimaye nimejiundia majibu kuwa Tundu Lissu amehukumiwa kifo na watu wasiojulikana kwa gharama na namna yoyote. Ninaumia mno! Nashindwa kuamini kama hii ni Tanzania au Rwanda!

Kitendo cha Mawakili wa Serikali kupeleka ombi mahakamani Kisutu ili afutiwe dhamani ili aandikiwe Hati ya Kukamatwa popote alipo chini ya jua ni jaribio la kifo lililoshindwa kama risasi 16. Inaumiza mno. Lissu ameikosea nini nchi hii kiasi cha kumtakia kaburi? Kwa nini tumefikia hatua mbaya namna hii? Imefikia hatua dunia iitazame Tanzania kwa jicho lisilo la kawaida.

Lissu amepigwa risasi 16 mwilini. Mwili wa Lissu aijuaye ni mkewe lakini mwenyewe anasema "umechanwachanwa". Mifupa imevurugwa. Lissu ana maumivu makali. Lissu amesahau hata tendo la ndoa maana nyonga haifai. Lissu amepona kichwa tu. Yuko kitandani Ubelgiji. Mnaitana, mnakaa chini, anakuwepo mwenyekiti, hoja inatolewa, "sasa tunamfanyaji Lissu". Hatimaye mnaafikiana kuwa afutiwe dhamana ili tumkamate mgonjwa huyu, badala ya kulala wodini akalale Segerea kusiko hata na panadoli ya kutuliza maumivu. Hii ni nini kama siyo kutaka Lissu afe?

Ninatamani kuwaona kwa macho mawakili hawa kwa macho yangu. Niwaulize ni dini gani? Wana familia? Wamewahi kuumwa au kuuguza? Ni binadamu kama sisi? Wana nyama na damu kama sisi? Nani aliwatuma kufanya jaribio ovu hili? Walilipwa shilingi ngapi kwa jaribio hili?

Hakimu Simba Mungu akubariki. Mungu akuzungushie fensi ya Moto. Umeongozwa na Mungu kutupilia mbali jaribio hilo la shetani uliposema "HUO SI UBINADAMU". Najua umewaudhi mno waliopanga jaribio hilo. Umejiweka hatarini. Mungu akutetee! Thawabu yako ni kubwa mno!

Inawezekana baada ya jaribio hili kushindwa kikao kitakaa tena kutafuta Lissu afanywe nini? Maana Hakimu Simba amenawa kama Herode kwa Yesu. Lakini bado kuna sauti za asulubiwe?

Natoa wito kila mtu kwa imani yake tumuombee Lissu. Mungu awatie upofu wote wanaopanga "kummaliza". Mungu mtetee maana anakusudi naye!

Tumeshindwa kumdhibiti Lissu kwa hoja sasa tunataka afe gerezani. Mungu shuka! Kama hiyo ndiyo Tanzania mpya, basi siitaki. Mturudishie Tanzania yetu iliyokuwa imejaa watu wenye huruma, upole, upendo, udugu, umoja, amani na raha!
#AchaWoga 2020
 
Wanatumia kichaka cha lissu kujificha wanataka kututoa kwenye mstari ili kutusahaulisha mambo ya msingi. Kuna mambo ya msingi ambayo serikali inatakiwa ishuhulike nayo kuliko kufatilia habari za lissu ambazo hazita weza kufix matatizo yetu

Ndege iliyoletwa 2016 imeharibika inatakiwa kwenda kanada kufanyiwa service itakayo kosti bilion 16, ikitengamaa itaendelea kubeba nyama ya mbuzi kupeleka dubai.

Tani zaidi ya 60 zimerejeshwa kwa wakulima wa korosho zikisemekana hazina ubora.

Deni la taifa laongezeka hadi kufikia tilion 60+ wakati tumeambiwa hii nchi inajiendesha yenyewe bila kutegemea sponsa kutoka nje.

Tanzania imekua nchi ya 7 katika nchi zenye watu masikini wakati mwaka 2015 tulikua wa 25. Juzi dolla ilipanda kufikia 2415 leo imeongezeka hadi kufikia 2418.

Sent using unknown device
 
Kweli! Hii ya kumfutia Lissu dhamana kayo ni haki?
Ndio maana nasema tafsiri ya haki huwa ni pana sana,

Kwako inaweza ikawa haki kwa mwingine ikawa uonevu na kinyume cha hapo,

Ndio maana tukawekeana utaratibu wa rufani.
 
Vyovyote iwavyo Mungu hapangiwi,wala kukumbushwa namna ya kumuadhibu muovu wake.

Lissu anatakiwa arudi nyumbani,kuliko kudhurula kwa kigezo cha kuhubiri habari mbaya za serikali ya tz,hawa jamaa ambao mnadhani ni wabaya wake,wanaweza kufanya chochote,popote,muda wowote kama wakitaka.
 
MIMI si Muislamu lakini sasa naanza kuamini katika imani hii. Baada ya Tundu Lissu kushambuliwa na watu wasiojulikana Wazee wa Kiislamu Pemba, Unguja, Tanga, Bwagamoyo na Dar es salaam walisoma kinachoitwa "al-badir". Ninaambiwa ikisomwa hii basi aliyetenda jambo la unyama kwa siri wanapatwa na madhara. Wanaweweseka, wanaweza kuongea wenyewe kama vichaa, na wengine wanaweza hata kujiua au kuumbuka. Kwa mbali na karibu naona dalili za matokeo ya "al-badir".

Imenichukua muda kuamini macho yangu na masikio yangu. Nimetafakari na kujiuliza hatimaye nimejiundia majibu kuwa Tundu Lissu amehukumiwa kifo na watu wasiojulikana kwa gharama na namna yoyote. Ninaumia mno! Nashindwa kuamini kama hii ni Tanzania au Rwanda!

Kitendo cha Mawakili wa Serikali kupeleka ombi mahakamani Kisutu ili afutiwe dhamani ili aandikiwe Hati ya Kukamatwa popote alipo chini ya jua ni jaribio la kifo lililoshindwa kama risasi 16. Inaumiza mno. Lissu ameikosea nini nchi hii kiasi cha kumtakia kaburi? Kwa nini tumefikia hatua mbaya namna hii? Imefikia hatua dunia iitazame Tanzania kwa jicho lisilo la kawaida.

Lissu amepigwa risasi 16 mwilini. Mwili wa Lissu aijuaye ni mkewe lakini mwenyewe anasema "umechanwachanwa". Mifupa imevurugwa. Lissu ana maumivu makali. Lissu amesahau hata tendo la ndoa maana nyonga haifai. Lissu amepona kichwa tu. Yuko kitandani Ubelgiji. Mnaitana, mnakaa chini, anakuwepo mwenyekiti, hoja inatolewa, "sasa tunamfanyaji Lissu". Hatimaye mnaafikiana kuwa afutiwe dhamana ili tumkamate mgonjwa huyu, badala ya kulala wodini akalale Segerea kusiko hata na panadoli ya kutuliza maumivu. Hii ni nini kama siyo kutaka Lissu afe?

Ninatamani kuwaona kwa macho mawakili hawa kwa macho yangu. Niwaulize ni dini gani? Wana familia? Wamewahi kuumwa au kuuguza? Ni binadamu kama sisi? Wana nyama na damu kama sisi? Nani aliwatuma kufanya jaribio ovu hili? Walilipwa shilingi ngapi kwa jaribio hili?

Hakimu Simba Mungu akubariki. Mungu akuzungushie fensi ya Moto. Umeongozwa na Mungu kutupilia mbali jaribio hilo la shetani uliposema "HUO SI UBINADAMU". Najua umewaudhi mno waliopanga jaribio hilo. Umejiweka hatarini. Mungu akutetee! Thawabu yako ni kubwa mno!

Inawezekana baada ya jaribio hili kushindwa kikao kitakaa tena kutafuta Lissu afanywe nini? Maana Hakimu Simba amenawa kama Herode kwa Yesu. Lakini bado kuna sauti za asulubiwe?

Natoa wito kila mtu kwa imani yake tumuombee Lissu. Mungu awatie upofu wote wanaopanga "kummaliza". Mungu mtetee maana anakusudi naye!

Tumeshindwa kumdhibiti Lissu kwa hoja sasa tunataka afe gerezani. Mungu shuka! Kama hiyo ndiyo Tanzania mpya, basi siitaki. Mturudishie Tanzania yetu iliyokuwa imejaa watu wenye huruma, upole, upendo, udugu, umoja, amani na raha!
#AchaWoga 2020
kwa jinsi nchi ilivyopasuka vipande vipande...nakwambia ikiibuka vita na nchi jirani kuna uwezekano wa informers wa adui wakawa ni Watanzania wenyewe....and who will blame them kwa hii chuki ya kishetani iliyopo sasa hivi hapa nchini?

kama tunamjua huyu shetani aliyetusababishia yote haya ni wakti sasa umefikia kwa Watanzania kusema "basi imetosha sasa - tulitoe joka pangoni!!"
 
Acha hizo kama wanaweze kumfanya chochote basi wasingesubiri azunguke kila kona...maana kujibu hoja mmetoka kapa kummalizia mmeshindwa sasa iweje useme wanaweza kumfanya chochote?? TULIA DAWA IZAME NDANI UPONE
Vyovyote iwavyo Mungu hapangiwi,wala kukumbushwa namna ya kumuadhibu muovu wake.

Lissu anatakiwa arudi nyumbani,kuliko kudhurula kwa kigezo cha kuhubiri habari mbaya za serikali ya tz,hawa jamaa ambao mnadhani ni wabaya wake,wanaweza kufanya chochote,popote,muda wowote kama wakitaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawawezi, washamba Hawa wa karne ya 17 hawana uwezo huo.Ndiyo maana wanamtaka arudi kwa udi na uvumba!!!
 
Vyovyote iwavyo Mungu hapangiwi,wala kukumbushwa namna ya kumuadhibu muovu wake.

Lissu anatakiwa arudi nyumbani,kuliko kudhurula kwa kigezo cha kuhubiri habari mbaya za serikali ya tz,hawa jamaa ambao mnadhani ni wabaya wake,wanaweza kufanya chochote,popote,muda wowote kama wakitaka.
Ubavu wanao hapa tu ndo maana wanataka arudi..kule hawawezi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vyovyote iwavyo Mungu hapangiwi,wala kukumbushwa namna ya kumuadhibu muovu wake.

Lissu anatakiwa arudi nyumbani,kuliko kudhurula kwa kigezo cha kuhubiri habari mbaya za serikali ya tz,hawa jamaa ambao mnadhani ni wabaya wake,wanaweza kufanya chochote,popote,muda wowote kama wakitaka.
Kama alishindwa kulindwa hapa kwetu halafu unamshauri arudi hukuhuku aliposhindwa kulindwa, saa unategemea na huu ni ushauri au njama za mauaji? Kifo hupangwa na Mungu iwe kwa risasi au kwa kitu chochote acheni porojo
 
Back
Top Bottom