Bohari ya Dawa, MSD haina uwezo. Serikali okoeni jahazi msikae kimya

Mk54

JF-Expert Member
Dec 29, 2016
1,997
3,932
Sidhani kama huu ni wakati wa kuilamu Serikali kama ambavyo wengi wamekuwa wakifanya.

Ni wakati wa kuishauri Serikali njia sahihi na mbadala wa kupambana na hawa Virus wa Corona. Nimefuatilia hotuba ya Ummi Mwalimu na Mkurugenzi wa Bohari kwa kweli tunahitaji msaada kulinusuru Taifa.

Tahadhari ya Corona imeanza tangu mwezi January, lakini mpaka sasa hata ukienda kwenye Maduka ya Bohari hakuna Sanitizer na hakuna mkakati uliowekwa kuhakikisha kila Mtanzania anapata Sanitizer na Face Mask. Kinachoonekana ni Matangazo tu.

Tumewatuma ndugu zetu waliokuwa Tanzania matokeo yake wameambiwa waaandike namba za simu na watapigiwa simu.

Hivi hilo taifa nani alililoga, yaani hadi Sanitizer usubiri upigiwe simu? Seriously! Sanitizer ya 100Ml kwa matumizi binafsi nisubiri nipigiwe simu, are you kidding me or what!?

Waziri, Katibu Afya pamoja na Mkurugenzi - Bohari hawakuona hii tahadhari tangu mwezi January? Hivi taasisi za umma zina shida gani lakini?

Ni dhahiri kwamba Bohari ya Dawa Tanzania haina uwezo wa kusambaza nchi nzima hizo Sanitizer badala yake wanawachosha wananchi na kujiweka busy pasipokuwa na sababu za kuwa busy.

Serikali iingilie kati na kuongea na wazalishaji wa ndani, naamini wapo wengi, waitwe na wapewe Sifa za Kitaalam za Standard Sanitizer wafanye production haraka kwa kushirikiana na zianze kugaiwa hata bure au kuuzwa kwa bei ya chini kabisa ili hata mama ntilie aweze kumudu.

Hili sio suala la Bohari ya dawa, ni suala la kitaifa, nchi iamue kusuka au kunyoa.

Kuwe na Center maalumu kwa ajili ya kugawaa Sanitizer na sio kuitegemea Bohari yaa Dawa haina huo uwezo mtagombana na wananchi bure kuweni smart.

Kwanza Bohari ya Dawa inatoa hapo hapo nchini kwa kununua halafu na wao wanaenda kuuza.

Watu wameenda mpaka hicho kiwanda, wanachojibiwa eti Bohari ya Dawa imesema Sanitizer ziuzwe kwao tu halafu wao ndio wawauzie wananchi. Je, haya ni maagizo ya mamlaka za juu au? Hii ni fair? Kiwanda kiache kuokoa maisha ya watanzania kisa Bohari na ukienda Bohari hakuna kitu; serious,

Yaani kitu kama Sanitizer ndio ilipaswa kuwa muokozi kwa Mtanzania, lakini ni Watanzania wangapi wamepata kupitia MSD?

Tanzania kuweni seriously tuache hizi swaga za ajabu ajabu kila kitu kuwa kisiasa na kuita makamera.

Sanitizer wala sio kitu amazing, ni mchanganyiko wa pombe tu, acheni kujipa class!

Serikali kupitia waziri wa Afya; ingilia kati na tambua Bohari haina huo uwezo wa kusamabaza Sanitizer nchi nzima hata kama ikitaka.

Wasilianeni na Viwanda vya ndani haraka, hata Mo anazalisha Sanitizer na wengineo na muweke Center maalumu ya kugawa hizi Sanitizer, kwa kasi ya maambukizi huu sio muda wa kuanza kukimbizana na wahudumu, ni Muda wa kukimbizana kugawa Sanitizer vinginevyo mnaua Watanzania.
 
Watanzania bhana!!! hutaki ilaumiwe serikali kwani kazi hiyo ya nani? Nyie mnataka serikali ifanye kila kitu lakini ufanisi wake ni shida na wewe unajua lakini mnataka wasifiwe tu. Basi tumsifu mtukufu jiwe kwa kutuletea korona tunakoelekea watu wooote wameshatumbuliwa amini nakwambia Jiwe atajitumbua mwenyewe.

Kwa taarifa yako corona yenyewe haijatua hizi ni rasha rasha subiri itue sasa si mnaimboea, we umeiona serikali ya china hatua inazochukua.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom