Bodi za Taasisi za Umma ni Magenge ya Wezi - JK Vunja Zisukwe Upya. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bodi za Taasisi za Umma ni Magenge ya Wezi - JK Vunja Zisukwe Upya.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kanga, Aug 1, 2012.

 1. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #1
  Aug 1, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Katika kufanya uchambuzi wa usimamizi na uendeshaji wa mashirika na taasisi za umma nimegundua kuwa bodi hizo hazifanyi kazi kama inavyotakiwa bali bodi hizo zimegeuka kuwa magenge ya wezi na majambazi wa mali ya umma.Bodi zimeshindwa kusimamia uawala bora wa uongozi wa raslimali watu na fedha katika taasisi hizo, hivyo kusababisha matumizi mabaya ya madaraka,rushwa na ufisadi wa kutisha.Namshauri JK rais wa nchi ambaye amekuwa akiteua wenyeviti wa Bodi kufanya yafuatayo.

  1.kuvunja mara moja bodi za wakurugenzi wa taasisi nyingi ambazo zimekuwa zikitawaliwa na matumizi mabaya ya raslimali.
  2.Kuagiza ukaguzi maalum kwenye matumizi ya bodi na wajumbe wake hasa bodi za mazao zote,TANAPA,MIFUKO ya JAMII yote, mamlaka ya Ngorongoro ,TPA
  3.Kuhakikisha mjumbe wa bodi anawakilisha bodi siyo zaidi ya moja. kuna watu wanakaa kwenye bodi zaidi ya moja kama akina Prof. Luhanga,Eve Sinare,Juma Kaboyonga,Jenerali Mboma..............................
  4.Wabunge kukoma kuwa wajumbe wa bodi yoyote ya taasis ya umma.
  5.Waraka wa malipo ya wajumbe wa Bodi yanawekwa rasmi kisheria kwa bodi zote kuwa sawa kuliko ilivyo sasa ambapo yanatofautiana sana

  RAISI WANGU LAZIMA UCHUKUE MAAMUZI MAGUMU ILI KULINDA RASLIMALI ZA NCHI.

  Haiwezekani mashirika yanakusanya fedha lakini hayatoi gawiwo kwa serikali iliyotoa mtaji bali fedha zinazolishwa zinaliwa tu na wafanyikazi na Bodi. Tazama Bandari wanakusanya fedha nyingi lakini hata miundo mbinu kwenye bandari ni dhaifu sana ,barabara kupitia kule Malawi cargo ni mbaya lakini watu wanatafuna fedha.Bodi za mazao wakulima wanalia tu lakini bodi za mazao hasa Kahawa,Pamb,korosho wajumbe wanalipana mamilion ya fedha in xpense of mkulima , lazima tukomeshe UMAFIA HUU WA BODI NA NI JK TU TUNAKUTUMA.

  Wabilahh Tawfiquh
   
 2. e

  ezra1504 Member

  #2
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa hapo nani anamvunja mwenzake? Hao wezi wamewekwa na JK huyohuyo then unamwambia avunje hizo board ht akivunja atawaweka rafiki zake walewale na watafanya km hawa waliopo. Tatizo sio viongozi wa board ila serikali kwa ujumla!
   
 3. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #3
  Aug 1, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  ezra wakati mwingine JK anauziwa mbuzi kwenye gunia na wasaidizi wake.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #4
  Aug 1, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Well said.. Ndugu zake usalama wa taifa wapo humu watamfikishia ujumbe
   
 5. H

  Hon.MP Senior Member

  #5
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 142
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli ifanyike tathmini nawasioweza kazi waachie ngazi mara moja. Watendaji bora wanajulikana na wababaishaji pia wanajulikana hata ukiuliza watoto wa shule!
   
 6. W

  We know next JF-Expert Member

  #6
  Aug 1, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Jamani mie nina swali moja tu, hivi hapa Tanzania tunanyadhifa au positions ngapi (Numbers) ambazo ni za kuteuliwa na Rais?
   
 7. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #7
  Aug 2, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  We know next ,Rais katika nchi hii anateua kila kitu hata muonja chumvi, dawa ni katiba mpya kuziba mianya ya ovyo hiyo.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #8
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,109
  Likes Received: 1,499
  Trophy Points: 280
  tatizo sio bodi tatizo ni watu wanaofanya uteuzi wamegeuza hizo sehemu kuwa za kulipana fadhila sio kila mtu ana uwezo wa kuingia kwenye bodi kwa wale waliosomea taaluma ya uhasibu namaanisha (proffesional)wanaelewa hata kama utamaliza kwa kiwango cha juu bado huwezi kuwa kwenye bodi mpaka umepita kwenye ngazi mbalimbali na unapofikia hatua ya kuruhusiwa kuwa kwenye bodi tayari unakuwa na uwezo wa kutoa mchango unaostahili.Sasa hivi tunashuhudia wastaafu,wabunge watu ambao hawana hawana hata taaluma husika ndio wanakuwa kwenye bodi ndio maana wajumbe wa bodi wanashindwa kugundua wizi,kuendesha shuguri kwa ufanisi CAG aliwahi kutoa pendekezo la wabunge wasiwe wajumbe wa bodi lakini kwa kiburi cha serikai haya ndio tunaoyaona.Mashirika yanapofanya vizuri au vibaya wahusika wakuu ni bodi hivyo tuangalie je wanaoteuliwa kwenye bodi wanakidhi sifa
   
Loading...