Bodi ya wakurugenzi wa LHRC wamethibitisha kuchaguliwa kwa Dr Slaa kupata tuzo!

Kagemro

JF-Expert Member
Jan 11, 2010
1,433
633
Bodi ya wakurugenzi wa LHRC,imethibitisha kuchaguliwa kwa Dr Wilbroad Peter Slaa kupata tuzo ya majimaji kwa kuwa Mbunge aliyetoa mchango mkubwa katika utawala bora na haki za binadamu 2005 - 2010.

Award itatolewa tarehe kumi December siku ya haki za binadamun chini.

Tuzo hii awali ilikuwa itolewe mwishoni mwa mwezi wa Tisa lakini nafikiri kutokana na uwoga wa watu wetu ambao bado hawajakomaa kinidhamu (wana nidhamu ya uwoga) wakaamua kuhairisha mpaka siku ya kesho.

Ndugu wana JF tulio na mapenzi mema labda kwa upande mwingine tunathamini mchango wa ndugu huyu nahisi tunaweza kushiriki maana siku hii inasherehekewa na watu wote.
 
Slaa kanyaga Twende hakuna kurudi nyuma. Na Madiba alihangaika hivihivi: Angalia quotes za Mzee Mandela:

....I have cherished the ideal of a democratic and free society in which all persons live together in harmony and with equal opportunities. It is an ideal which I hope to live for and to achieve. But if needs be, it is an ideal for which I am prepared to die.
Nelson Mandela - April 20, 1964

There are many people who feel that it is useless and futile for us to continue talking peace and non-violence - against a government whose only reply is savage attacks on an unarmed and defenseless people. And I think the time has come for us to consider, in the light of our experiences at this day at home, whether the methods which we have applied so far are adequate. Nelson Mandela Interview (1961)
 
Kama mbunge anastahili! Dr. mchango wake utakumbukwa daima, mbinu za majambazi kumuingiza choo cha kike zilaaniwe milele
 
Mimi mgeni katika site hii, hiyo sherehe itakuwa wapi na tunashiriki vp? ahsante. col.
 
Kama mbunge anastahili! Dr. mchango wake utakumbukwa daima, mbinu za majambazi kumuingiza choo cha kike zilaaniwe milele

Congratulations Dr Slaa, the most daring and straight politician of our time, ofcourse vying for president has made you more popular and it has delivered more opposition MP's than ever before in Tanzania Bara history!

Your campaigns alone drawed people of all walks of life, yes BURN didnt like you and yes some Tanzanians didnt, but those who truly voted for you did and the same is true for KIKWETE there are those who hated him and watake wasitake ndio rais , i just dont see the importance of generalizing all TZ that didnt like him for he had a % of their votes..however its absurd to hang on to the bruises that happened nov 1st, if we had risen above that, we shall truly conquer, kuna madudu mengi sana i just want to shout them loudly but i so fear for my security, if this man dared..salute sir !
 
Tunashukuru kwa taasisi hii kuonesha kuthamini mchangowa Dr. Slaa.

Nina imani, kwa siku zijazo ataendelea kupata nishani nyingi zaidi kwa falsafa yake ya Haki ya Kupata Elimu Bora kwa Kila Mtanzania, Haki ya Makazi Bora, Umuhimu wa Serikali kutumia Mapato yake Kwa Maendeleo ya Wananchi badala ya Anasa za Watawala, n.k.
 
Kama mbunge anastahili! Dr. mchango wake utakumbukwa daima, mbinu za majambazi kumuingiza choo cha kike zilaaniwe milele
Mod naomba huyu jamaa anayejiita burn afungiwe. Kwa nini tunaruhusu watu wasiokuwa na akili sawasawa hapa jamvini. TUNAHITAJI WATU AMBAO WATATOA MAONI NA MICHANGO YAO KULETA MANUFAA KATIKA JAMII.
 
mm kama kustahiki naona zitto anafaa zaidi ila sijui kwa nn hawakumfikiria au kulikoni ?
 
QUOTE=mfarisayo;viva Dr.(PHD)

It's PhD not PHD. Husifanye kama wale wanaoandika PH scale badala ya pH scale.
 
mm kama kustahiki naona zitto anafaa zaidi ila sijui kwa nn hawakumfikiria au kulikoni ?

Zito alikuwa mtu wa 156 katika kuchangia Bungeni Dr. Slaa alikuwa wa Kwanza akifuatiwa na wabunge wawili wa CCM. So Dr (PhD) Slaa ni haki yake.

Moyo wangu umefurahishwa sana na hilo. Nitakuwepo Lazima. Lakini hafla itaanza saa ngapi?
 
Bodi ya wakurugenzi wa LHRC,imethibitisha kuchaguliwa kwa Dr Wilbroad Peter Slaa kupata tuzo ya majimaji kwa kuwa Mbunge aliyetoa mchango mkubwa katika utawala bora na haki za binadamu 2005 - 2010.

Award itatolewa tarehe kumi December siku ya haki za binadamun chini.

Tuzo hii awali ilikuwa itolewe mwishoni mwa mwezi wa Tisa lakini nafikiri kutokana na uwoga wa watu wetu ambao bado hawajakomaa kinidhamu (wana nidhamu ya uwoga) wakaamua kuhairisha mpaka siku ya kesho.

Ndugu wana JF tulio na mapenzi mema labda kwa upande mwingine tunathamini mchango wa ndugu huyu nahisi tunaweza kushiriki maana siku hii inasherehekewa na watu wote.

Pongezi za dhati kwa Dr. Slaa na kwa LHRC kutambua mchango uliotukuka na wa kishujaa wa Dr. Slaa. Mambo aliyoyaibua bungeni yalikuwa mazito sana na yenye kutetea masilahi ya taifa letu. Mchango wake si tu tunaukumbuka na utakumbukwa na watu wote wenye mapenzi mema bali pia umewapa ujasiri watu wengi zaidi kuweza kuingia katika ulingo wa kutetea nchi yetu. Hongera sana Dr. Slaa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom