Kuna watu hawajui kama kuna nchi inaitwa Tanzania duniani mkuu.Leo hii ukisema hata Tanzanite inapatikana Kenya Dunia itaamini japo jina tu linaakisi origin yake. Wazungu ni mazuzu na wavivu wa kufikiri, wanadanganywa kizembe
View attachment 367710
Kama ni uvivu sisi watanzania tumezidisha.
Hii ni mara ya pili huu mlima kukosewa kwamba upo nchini Kenya.
Tujitahidi kivitangaza hivi vivutio jamani.
hawa TTB c juzi juzi tu walikataa kushiriki kwenye maonesho ya utalii UK hasa wanacholia lia ni nn??
Dawa yao ni kuzuia watalii kupanda mlima kwa kutokea Kenya ni lazima waingie Tz kwa visa na wanatakiwa wajue sasa wanaingia Tz tena wakati wanaingia wanatakiwa wapatikane watanga vivutio vyetu wawaambie kila kivutio kilichopo Tz
Kwa kweli hii TTB ifumuliwe tu iundwe upya na wawe wsnapewa target kabisa. Siyo TTB tu ingia website ya Ngorongoro utakutana na vi data vya mwaka 2012 tu. Sasa nashangaa kwa dunia ya leo tunategemea kufanikiwa kimiujiza?? We have to work hard otherwise tutaishia kukemea vyombo vya kimataifa bure tu.Jamani eehh huko duniani Tanzania inajulikana nawale waliofika tz ama kutembelewa na wa tz. Kwa ujumla inajulina east africa maana yake Kenya. TTB ikarabatiwe maana haina muamko wa tourism. Nilifika Miami nikiulizwa unatoka wapi nasema Tanzania, East Africa. Anayeuliza ana jibu tena yeye aah Kenya kama vile east africa yote ni Kenya. Balozi zetu ziwe active. Nime furahi mheshimiwa Masillingi kuanza kujinadi Seattle huko Marekani kwani itawakumbusha Boeing kuwa kuna nchi inaitwa Tanzania.