alvinroley
Member
- Sep 30, 2016
- 71
- 251
Wakuu kazi haitakuwa ya Kitoto na tunatakiwa tuandae jopo letu la wataalamu na wanasheria vichwa n'a makini sana. Inasemekana Bodi ya Ushauri ya Kimataifa itakuwepo katika mazungumzo yajayo kati ya Barrick/Acacia n'a Serikali ya Tanzania. Kazi ya Bodi hii itakuwa ni kutoa Ushauri katika Mikataba iliyosainiwa zamani n'a pande hizo mbili. Sasa huenda katika mazungumzo hayo tukawashinda n'a tukapata pesa zetu au tukaambulia patupu kwa kuwa Mikataba tuliisaini wenyewe n'a makubaliano tuliingia. Na Nadhan watakuja na ushahidi wa picha, vielelezo na video.
Nisiende mbali, Hebu wajue wajumbe wa Bodi hii ya Ushauri ya kimataifa, tukiwajua itakuwa vizuri kujiandaa na kuwaandaa wataalamu wetu:
Bodi Ina members 12 ambapo wako Mawaziri Wakuu wastaafu wawili na mawaziri wengine wanne wa nchi nne tofauti na inaongozwa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Canada, Brian Mulroney. Pia kuna Waziri Mkuu wa zamani wa Hispania, Jose Maria Aznar na Spika wa zamani wa bunge la wawakilishi la Marekani, Newt Gingrich. Yumo aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, John Baird na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Marekani, William Cohen na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Shirikisho la Ujerumani, Karl-Theodor zu Guttenberg. Yumo aliyekuwa Mshauri Mkuu wa Margreth Thatcher na John Major kuhusu masuala ya nchi za nje. Pia yuko Mtanzania na mwafrika pelée Balozi Juma Mwapachu.