Tetesi: Bodi ya Ushauri ya Kimataifa Kuhudhuria Mazungumzo ya Barrick/Acacia na Serikali

Walituchukua utumwa, walitubagua,walitunyanyasa,walitufanya makoloni yao....sasa imetosha tufanye biashara win win hatuogopi tena..ndugu zangu watanzania tumuunge mkono rais magufuli.
can-stock-photo_csp2253564.jpg
Wao
69446014.jpg

Sisi
 
Dah!

Kwani hao nao si ni watu tu kama sisi!

Yaani tayari watu mshaonyesha hali ya kushindwa hata kabla ya kuanza kwa hayo mazungumzo kisa tu eti ya watu waliomo kwenye hiyo bodi ya hiyo kampuni!

Kwani tunaenda kushindana kurusha maroketi angani?

Bure kabisa!!!!!
watu wanaogopa wazungu
 
Miafrika ndo tulivyo!!! Huwa hatupendi kujiamini. Kwani hao wakija watabadilisha maandishi ya mikataba na uelewa wetu?
Hii issue ishafeli mkuu. Ni sawa na mtu umemkamata na vitu vyako, halafu unasema tufanye mazungumzo. Ni kitu ambacho hakiewezekani. Mwizi unamkaribisha IKULU? Na ulinzi mnampa km mgeni mheshimiwa.
Teh teh teh teh
Ningemuona Magu yupo serious km huyu bwana mkubwa wa Acacia angefikia mahakamani.
Hayo mazungumzo ya nn? Ndiyo huko huko ukifika yes yes yes yes hakijulikani kilichozungumziwa.
Unaweza kuniambia ikulu walizungumza nn? Na je wamekubali kulipa hizo trillion 110? Na ni lini watalipa?
 
Acheni Uoga Watanzania wenzangu, nawasihi sana, ushahidi tulionao sisi ni kama Mbuzi kafia kwa muuza supu, tulieni, nchi nzima si wajinga, wataalamu wetu si wajinga kama mnavyodhani, unajua mtanzania mmoja mmoja anavyojiona kuwa yeye ni tahira au kichwani hamna kitu au uwezo wake mdogo wa kielimu anadhani ndivyo ilivyo kwa timu zilivyochunguza na kutoa report..... tulieni vijana, sisi ni nchi masikini kwa kipato lakini tumejitahidi kusomesha watu wetu, hivo nawaomba sana msiwe na wasiwasi...

Hata vitani si askari wote wanapigana vita, wengine kazi yao ni kutunga nyimbo za kuwahamasisha na kuwatia moyo na ari wenzao ili waweze kupigana kwa nguvu kubwa, hivyo ni sawa na vita hii, ninyi wengine kwa sasa mtuunge tu mkono na kutoa ushauri mzuri, acheni wengine tuingie vitani...
 
Wa kumuonea huruma hapo ni Juma Volter Mwapachu; atkwepaje shutuma na mishale mikali mikali kwa kuihujuma nchi yake mwenyewe! Bila shaka anaijua siri ya mtungi!
 
Wa kumuonea huruma hapo ni Juma Volter Mwapachu; atkwepaje shutuma na mishale mikali mikali kwa kuihujuma nchi yake mwenyewe! Bila shaka anaijua siri ya mtungi!

Lazima atakaa kando kukwepa mgongano wa maslahi.
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Tunasikitisha sana kwa kweli.

Yaani toka juzi watu washaanza kukubali kushindwa kabla hata ya kuanza kwa hayo mazungumzo kisa tu wameona kuna majina ya wazungu flani flani.

Kwanza nani anajua kama hao watu ndo watahusika na hayo mazungumzo?

Na hata wakihusika, so what? So freakin' what?
Tatizo watakao urge kesi yetu
Je ni Masaju,Tulia ,Mwakyembe,Osoro Mruma"
Nani kati yao ana uwezo hata wa kujieleza?
 
Wakuu kazi haitakuwa ya Kitoto na tunatakiwa tuandae jopo letu la wataalamu na wanasheria vichwa n'a makini sana. Inasemekana Bodi ya Ushauri ya Kimataifa itakuwepo katika mazungumzo yajayo kati ya Barrick/Acacia n'a Serikali ya Tanzania. Kazi ya Bodi hii itakuwa ni kutoa Ushauri katika Mikataba iliyosainiwa zamani n'a pande hizo mbili. Sasa huenda katika mazungumzo hayo tukawashinda n'a tukapata pesa zetu au tukaambulia patupu kwa kuwa Mikataba tuliisaini wenyewe n'a makubaliano tuliingia. Na Nadhan watakuja na ushahidi wa picha, vielelezo na video.
Nisiende mbali, Hebu wajue wajumbe wa Bodi hii ya Ushauri ya kimataifa, tukiwajua itakuwa vizuri kujiandaa na kuwaandaa wataalamu wetu:

Bodi Ina members 12 ambapo wako Mawaziri Wakuu wastaafu wawili na mawaziri wengine wanne wa nchi nne tofauti na inaongozwa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Canada, Brian Mulroney. Pia kuna Waziri Mkuu wa zamani wa Hispania, Jose Maria Aznar na Spika wa zamani wa bunge la wawakilishi la Marekani, Newt Gingrich. Yumo aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, John Baird na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Marekani, William Cohen na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Shirikisho la Ujerumani, Karl-Theodor zu Guttenberg. Yumo aliyekuwa Mshauri Mkuu wa Margreth Thatcher na John Major kuhusu masuala ya nchi za nje. Pia yuko Mtanzania na mwafrika pelée Balozi Juma Mwapachu.
Vichwa vyote hivi jamani tutapona ?

Sina hakika kama unajua umeandika nini
Hao wote uliowataja ni body member wa Barrick Gold Mine
Mwenyekiti wao ni Prof John Thornton
Huyu aliyekuwa kuongea na mh Rais
 
Sina hakika kama unajua umeandika nini
Hao wote uliowataja ni body member wa Barrick Gold Mine
Mwenyekiti wao ni Prof John Thornton
Huyu aliyekuwa kuongea na mh Rais
Mleta Mada kibaraka mzawa wa wazungu wa accacia atakuwa na undugu na tundu lisu. Kutwa maandiko yake ni kutishia watanzania nyau. Ukome ukibaraka. Unaandika unarudia rudia wewe oh bodi ina vigogo wastaafu so what? Go to hell
 
Tatizo watakao urge kesi yetu
Je ni Masaju,Tulia ,Mwakyembe,Osoro Mruma"
Nani kati yao ana uwezo hata wa kujieleza?
Pale sio kelele kama za lisu na uwezo wa kuongea lugha ya mkoloni wa kiingereza pale ni facts na data. Ule sio mkutano wa bavicha kuwa anatakiwa domokaya anayejua kupanua domo na kuongea sana
 
watakuwa wanaiba sana na hawataki kuacha inawezekana tunaibiwa madini ya dhamani kubwa kuliko mafuta wanayo iba huko Libya na Iraq ndio maana wanataka kuwatisha ma professor wetu na siyo ajabu kila mmoja akaja na private jet kama alivyokuja nayo huyo tapeli mwingine aliyeitwa nani vile???
 
Back
Top Bottom