Tetesi: Bodi ya Ushauri ya Kimataifa Kuhudhuria Mazungumzo ya Barrick/Acacia na Serikali

alvinroley

Member
Sep 30, 2016
70
400
Wakuu kazi haitakuwa ya Kitoto na tunatakiwa tuandae jopo letu la wataalamu na wanasheria vichwa n'a makini sana. Inasemekana Bodi ya Ushauri ya Kimataifa itakuwepo katika mazungumzo yajayo kati ya Barrick/Acacia n'a Serikali ya Tanzania. Kazi ya Bodi hii itakuwa ni kutoa Ushauri katika Mikataba iliyosainiwa zamani n'a pande hizo mbili. Sasa huenda katika mazungumzo hayo tukawashinda n'a tukapata pesa zetu au tukaambulia patupu kwa kuwa Mikataba tuliisaini wenyewe n'a makubaliano tuliingia. Na Nadhan watakuja na ushahidi wa picha, vielelezo na video.
Nisiende mbali, Hebu wajue wajumbe wa Bodi hii ya Ushauri ya kimataifa, tukiwajua itakuwa vizuri kujiandaa na kuwaandaa wataalamu wetu:

Bodi Ina members 12 ambapo wako Mawaziri Wakuu wastaafu wawili na mawaziri wengine wanne wa nchi nne tofauti na inaongozwa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Canada, Brian Mulroney. Pia kuna Waziri Mkuu wa zamani wa Hispania, Jose Maria Aznar na Spika wa zamani wa bunge la wawakilishi la Marekani, Newt Gingrich. Yumo aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, John Baird na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Marekani, William Cohen na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Shirikisho la Ujerumani, Karl-Theodor zu Guttenberg. Yumo aliyekuwa Mshauri Mkuu wa Margreth Thatcher na John Major kuhusu masuala ya nchi za nje. Pia yuko Mtanzania na mwafrika pelée Balozi Juma Mwapachu.
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
85,585
2,000
Dah!

Kwani hao nao si ni watu tu kama sisi!

Yaani tayari watu mshaonyesha hali ya kushindwa hata kabla ya kuanza kwa hayo mazungumzo kisa tu eti ya watu waliomo kwenye hiyo bodi ya hiyo kampuni!

Kwani tunaenda kushindana kurusha maroketi angani?

Bure kabisa!!!!!
 
Musoma Yetu

JF-Expert Member
Mar 11, 2016
2,626
2,000
!

Kwani hao nao si ni watu tu kama sisi!

Yaani tayari watu mshaonyesha hali ya kushindwa hata kabla ya kuanza kwa hayo mazungumzo kisa tu eti ya watu waliomo kwenye hiyo bodi ya hiyo kampuni!

Kwani tunaenda kushindana kurusha maroketi angani?

Bure kabisa!!
Miafrika ndo tulivyo!!! Huwa hatupendi kujiamini. Kwani hao wakija watabadilisha maandishi ya mikataba na uelewa wetu?
 
ngugi wa thiongo

Senior Member
Aug 22, 2013
106
225
Dah!

Kwani hao nao si ni watu tu kama sisi!

Yaani tayari watu mshaonyesha hali ya kushindwa hata kabla ya kuanza kwa hayo mazungumzo kisa tu eti ya watu waliomo kwenye hiyo bodi ya hiyo kampuni!

Kwani tunaenda kushindana kurusha maroketi angani?

Bure kabisa!!!!!
we we we hapo ni hatari mjomba!!!hyo lugha ya hapo kwanza watu wataumwa mafua ya ghafla!!!!
 
Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
21,266
2,000
Wakuu kazi haitakuwa ya Kitoto. Inasemekana Bodi ya Ushauri ya Kimataifa yenye wajumbe 'vichwa' itakuwepo katika mazungumzo yajayo kati ya Barrick/Acacia n'a Serikali ya Tanzania. Kazi ya Bodi hii itakuwa ni kutoa Ushauri katika Mikataba iliyosainiwa zamani n'a pande hizo mbili. Sasa huenda katika mazungumzo hayo tukapata pesa zetu au tukaambulia patupu kwa kuwa Mikataba tuliisaini wenyewe.
Nisiende mbali, Hebu wajue wajumbe wa Bodi hii ya Ushauri ya kimataifa:

Bodi Ina members 12 ambapo wako Mawaziri Wakuu wastaafu wawili na mawaziri wengine wanne wa nchi nne tofauti na inaongozwa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Canada, Brian Mulroney. Pia kuna Waziri Mkuu wa zamani wa Hispania, Jose Maria Aznar na Spika wa zamani wa bunge la wawakilishi la Marekani, Newt Gingrich. Yumo aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, John Baird na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Marekani, William Cohen na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Shirikisho la Ujerumani, Karl-Theodor zu Guttenberg. Yumo aliyekuwa Mshauri Mkuu wa Margreth Thatcher na John Major kuhusu masuala ya nchi za nje. Pia yuko Mtanzania na mwafrika pelée Balozi Juma Mwapachu.
Vichwa vyote hivi jamani tutapona ?

Unaabudu sana Wazungu wewe, kwa mfano huyo Waziri wa Ulinzi (zamani) wa Ujerumani Gutenberg, alifukuzwa kazi ya Uwaziri kwa sababu alifoji PhD thesis yake, na hao wengine ni hivyo hivyo,!
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
85,585
2,000
Miafrika ndo tulivyo!!! Huwa hatupendi kujiamini. Kwani hao wakija watabadilisha maandishi ya mikataba na uelewa wetu?
Tunasikitisha sana kwa kweli.

Yaani toka juzi watu washaanza kukubali kushindwa kabla hata ya kuanza kwa hayo mazungumzo kisa tu wameona kuna majina ya wazungu flani flani.

Kwanza nani anajua kama hao watu ndo watahusika na hayo mazungumzo?

Na hata wakihusika, so what? So freakin' what?
 
Jozi 1

JF-Expert Member
Aug 16, 2015
6,202
2,000
Wakuu kazi haitakuwa ya Kitoto. Inasemekana Bodi ya Ushauri ya Kimataifa yenye wajumbe 'vichwa' itakuwepo katika mazungumzo yajayo kati ya Barrick/Acacia n'a Serikali ya Tanzania. Kazi ya Bodi hii itakuwa ni kutoa Ushauri katika Mikataba iliyosainiwa zamani n'a pande hizo mbili. Sasa huenda katika mazungumzo hayo tukapata pesa zetu au tukaambulia patupu kwa kuwa Mikataba tuliisaini wenyewe.
Nisiende mbali, Hebu wajue wajumbe wa Bodi hii ya Ushauri ya kimataifa:

Bodi Ina members 12 ambapo wako Mawaziri Wakuu wastaafu wawili na mawaziri wengine wanne wa nchi nne tofauti na inaongozwa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Canada, Brian Mulroney. Pia kuna Waziri Mkuu wa zamani wa Hispania, Jose Maria Aznar na Spika wa zamani wa bunge la wawakilishi la Marekani, Newt Gingrich. Yumo aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, John Baird na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Marekani, William Cohen na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Shirikisho la Ujerumani, Karl-Theodor zu Guttenberg. Yumo aliyekuwa Mshauri Mkuu wa Margreth Thatcher na John Major kuhusu masuala ya nchi za nje. Pia yuko Mtanzania na mwafrika pelée Balozi Juma Mwapachu.
Vichwa vyote hivi jamani tutapona ?
Ninavyokuona hapa, we ungekuwepo enzi za ukoloni sidhani kama hata ungethubutu kufungua mdomo kudai uhuru.
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
12,776
2,000
Dah!

Kwani hao nao si ni watu tu kama sisi!

Yaani tayari watu mshaonyesha hali ya kushindwa hata kabla ya kuanza kwa hayo mazungumzo kisa tu eti ya watu waliomo kwenye hiyo bodi ya hiyo kampuni!

Kwani tunaenda kushindana kurusha maroketi angani?

Bure kabisa!!!!!
Ndugu yangu yaani inaonekana kuwa "Mzungu" tu kwa Africa ni bonge moja la CV
 
sblandes

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
4,563
2,000
Tatizo si wazungu tatizo ni kile kilichowekwa mezani mwanzoni na serikali yetu,hadi kupelekea kusaini mikataba.
Kwa mfano mwelekezaji anakuja na mshahara wa mfanyakazi dola 1500,lakini wawakilishi wa serikali yetu anasema mbona ni nyingi mno muwalipe dola 50 tu kwa mwezi.
Swali la pili linakuwa rahisi zaidi kwa mzungu anapanga mihamala 20%ya serikali lakini wawakilishi wa serikali wanasema 3% inatosha sana kinachobaki chao binafsi,makofi na mkataba unasainiwa.
Usifikiri wazungu ni wajinga,wanaweza kuwa na video za mjadala hadi makubaliano,wachokeze uone kasheshe kwenye CNN,BBC
 
Nzi

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
13,831
2,000
Dah!

Kwani hao nao si ni watu tu kama sisi!

Yaani tayari watu mshaonyesha hali ya kushindwa hata kabla ya kuanza kwa hayo mazungumzo kisa tu eti ya watu waliomo kwenye hiyo bodi ya hiyo kampuni!

Kwani tunaenda kushindana kurusha maroketi angani?

Bure kabisa!!!!!
Chifu, ni ukweli mchungu kwamba hata jinsi negotiations za mikataba mbalimbali ya uwekezaji hapa nchi, timu zetu uenda kinyonge. Niliwahi kuhudhuria public consultation ya sera ya madini. Yaani wale wataalamu walikuwa wanaongea kuonyesha kwamba Tanzania kama nchi masikini haina voice mbele ya hao wawekezaji wanaokuja na pesa zao. Nikauliza, lakini sisi kama nchi si ndiyo tuna rasilimali? Kwani msiwe na equal powers, ama zaidi? Nilikuwa nikiulizia jinsi sera ilivyo vague kwenye CSR. Ndiyo maana makampuni makubwa ya uwekezaji unaona yanatoa madawati kama sehemu ya CSR. Niliwaambia kwanini sera isielekeze kwamba CSR itokane na matatizo ya msingi ya kijamii kwenye eneo husika? Mfano, kama ni uwekezaji kwenye gesi Mtwara, kwanini wawekezaji wasiambiwe part ya CSR ni kujenga world class hospital; ama kuweka miundombinu mikubwa ya barabara, maji, umeme n.k.

Hivyo kilichosemwa na mtoa mada, ndiyo uhalisia wa negotiation teams zetu! Inasikitisha, lakini ndiyo hali halisi!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom