Bodi ya Uratibu wa NGOs yatahadharisha NGO kutojihususha na masuala ya kisiasa

mnyalilungulu

Senior Member
Sep 27, 2019
170
114
Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini imeyatahadharisha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutojihususha na masuala ya kisiasa bali wasimamie Katiba zao katika kutekeleza majukumu yao ya kuisadida jamii ya watanzania.

Mwenyekiti wa Bodi Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini Dkt. Richard Faustine Sambaiga ametoa tahadhari hiyo mkoani Mwanza alipokutana na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiseikali mara baaada ya kutembelea baadhi ya Mashiria hayo kujionea utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Mashriika ya mkoa wa Mwanza

Dkt. Sambaiga amesema kuwa katika kipindi cha uchaguzi wadau wengi wa NGOs wanahama katika majukumu yao na kuanza kupeperusha bendera za watu wengine na sio kuihudumia jamii inayowazunguka kama Katiba zao zinavyoelekeza.

Pia amewataka wadau wanaofanya kazi za kutoa elimu kwa wapiga kura kutumia fursa ya uchaguzi Mkuu ujao kuchangamkia fursa hiyo na kuwataka kutoa elimu ya kupiga kura na sio kampeni za kisiasa. “Kama unaona unataka kujiingiza katika masuala ya kisiasa achana na kazi za NGOs simama wewe kama wewe na sio kuitumia NGO kwa ajili ya kufanya kampeni au kuwafanyia watu kampeni za kisiasa” alisema Dkt. Sambaiga

Dkt. Sambaiga ameyataka Mashirika kujiendesha kitaasisi na sio kuendesha Mashirika hayo kwa maslahi ya mtu mmoja au kikundi cha watu bali watekeleze majukumu kwa mujibu wa Katiba yao waliosajili Shirika. “Tumetembelea Shirika moja osi zipo nyumbani kwa Mkurugenzi tukaomba mikataba ya fedha hana sasa hili Shirika linaendeshwaje na mtu mmoja na lina wajumbe zaidi ya kumi”alisisitiza Dkt. Sambaiga Kwa upande wake Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Vickness Mayao amesema kuwa Osi yake imeamua kutembelea Mashirika mkoani Mwanza kufuatilia miradi ianyotekelezwa na Mashirka hayo kwa jamii. “Tumekuja kwenu kwa lengo la kujionea miradi mnayoitekeleza katika jamii na kuona kwa uwazi na uwajibikaji wa Mashirika yenu kwa jamii ikiwemo Jamii husika kujua miradi inayotekelewa na gharama zake” alisema Bi. Vickness. Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini imetembelea na kukagua utekelezaji wa miradi inayofanya na Mashirika yaliyopo mkoani Mwanza kwa lengo la kujiridhisha juu ya miradi hiyo na manufaa yake katika jamii.
 
Hivi kujihusisha na mambo ya siasa ni nini? Kwani taasisi yoyote, ikijitokeza na kukemea uovu unaofanyika kwenye jamii hasa unaohusiana na viongozi, wanaambiwa wanajihusisha na siasa!!! Ila hao hao wakijitokeza na kukemea wapinzani kuwa ni hatari kwa taifa, wanapongezwa kuwa ni wazalendo!!! Hao hao wakimsifia kiongozi mwana siasa aliyopo madarakani, watasifiwa!! Africa bwana!!!
 
Hii bodi inasaidia vip haya mashirika kupata fedha za kutekeleza miradi?
 
Back
Top Bottom