Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) yakosea kuchapisha mtihani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) yakosea kuchapisha mtihani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TUMBIRI, Nov 2, 2011.

 1. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wakuu,
  Leo saa tatu kasorobi asubuhi nimeenda kufanya mtihani wangu wa kwanza wa 'Final stage Model F' somo la 'Contemporary Issues in Accounting pale ukumbi wa Karume ndani ya Viwanja vya SABASABA, mitihani ambayo inaratibiwa na Bodi yetu ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA). Wanafunzi wote baada ya kuingia ndani ya chumba cha mtihani, tuligawiwa mtihani huo lakini hatukuruhusiwa kuufungua hadi hapo msimamizi wa mtihani atakaporuhusu.

  Mara ikatolewa tangazo tuzikusanye karatasi zote za maswali kwa kuwa zilikuwa ni za somo lingine ambalo si ratiba yake kwa wakati huo. Baada ya kukusanya tulikaa kama dakika ishirini hivi tangazo lingine likatolewa kwamba karatasi ya maelezo (Instructions) ya maswali zilizokuwa zimegawiwa awali zilikuwa zimeandikwa jina la mtihani wa 'Financial Reporting II' badala ya 'Contemporary Issues in Accounting'. Lakini wamefanya mawasiliano na Bodi na maelekezo waliyoyapata kutoka huko ni kuwa ingawa karatasi ya maelezo ya maswali inaonyeshesha mtihani huo ni 'Financial Reporting II', maswali yaliyopo ndani ni ya mtihani wa 'Contemporary Issues in Accounting'.

  Kwa msingi huo tukarudishiwa karatasi za maswali tukaambiwa tusi-konside karatasi ya kwanza ambayo ni ya maelezo 'instructions' kwa kuwa imekosewa kuchapishwa jina la mtihani. Lakini maswali yaliyomo ndani ni ya mtihani husika yani 'Contemporary Issues in Accounting'. So tukaambiwa tuanze kufanya mtihani na Bodi ya Taifa ya Wakaguzi na Wahasibu inaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

  My concern:
  Imekuwaje Bodi yetu NBAA inayoheshimika kuliko hata Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) ikafanya kosa hili kubwa la kiufundi. Naomba Mkurugenzi Mtendaji awawajibishe waliohusika na tukio hili kwani limelishushia heshima Bodi kwa umakini uliokuwa nao toka ilipoanzishwa. Ikishindikana basi yeye Mkurgenzi Mtendaji ajiuzulu.
   
 2. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Wewe si mtihani wa somo la leo umefanya? Huu muda wa kulalama huko ungejiandaa kwa paper ingine.
   
 3. l

  laun Senior Member

  #3
  Nov 2, 2011
  Joined: Sep 5, 2011
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ungeandikwa cont....accointing halafu ukakuta maswali ni ya financial repoting c ndo ungetaka bodi ivunjwe
  Kwa accountant hiyo ni immaterial ,sio jambo la kulalama kihiivyo
  Hongera kwa kufanya module F coz ni hatua kubwa
   
 4. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #4
  Nov 2, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,482
  Likes Received: 5,554
  Trophy Points: 280
  Mkuu hii haijawahi kutokea! Na pengine ni indicator flani kuwa umakini umepungua!
   
 5. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #5
  Nov 2, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Risks are always there
   
 6. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #6
  Nov 2, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,482
  Likes Received: 5,554
  Trophy Points: 280
  utoah aliwahi kuchanganyikiwa kwa tetesi tu kuwa paper imevuja Arusha.NBAA wanasifika kwa umakini na quality ya professional exams lakini tembo akisifiwa sana....
   
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Mkuu hii Bodi ilikuwa enzi hizoooooo! Wakati huo kulikuwa hakuna tetesi za fake lakini miaka kama minne iliyopita kumekuwa na tetesi za fake!! NBAA haina umakini wowote siku hizi. Kwanza nilisikia inatakiwa kupunguziwa majukumu kianzishwe chombo kingine cha kusimamia mitihani lakini naona bado.
   
 8. howard

  howard Senior Member

  #8
  Nov 2, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hiyo ni immaterial issue komaa maliza final stage yako achana na makosa hayo ya kiufundi bahati mbaya na halijawahi kutokea hata siku moja
   
 9. Shakazulu

  Shakazulu JF-Expert Member

  #9
  Nov 2, 2011
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 940
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  This shows that they are not serious in what they do. Quality assurance is lacking.

  Wakati JK anapokea hundi yenye maneno na tarakimu tofauti alishambuliwa sana hapa kuwa yeye na watu wake hawako makini sasa why should this be any different?

  If you start entertaining such mistakes then they will one day result in more serious ones na hapo sijui mtamlaumu nani. Cha msingi ni kwamba wajifunze kutokana na makosa yao and make sure it does not happen again.
   
 10. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #10
  Nov 2, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,887
  Likes Received: 6,071
  Trophy Points: 280
  hii comment yako nimeipenda kwa kweli na inaonyesha ni jinsi gani watu wako addicted na social networks!
  Lakini cha msingi hapa wanasema (wenzetu walioadvance kwenye masuala ya elimu na ujuzi) kuwa baada ya globalization ambayo ime-'unseal' vikwazo vya mawasiliano, wanatest uelewa wa watahiniwa/wanafunzi na sio uwezo wao wa kukariri. Nimeona hata Dr. (lecturer) mmoja anaemphasis katika suala hili lakini hapa bongo bado watu wanakazana na mambo yasiyo ya msingi katika kuelimishana. Wanadhani bado kusoma ni hadhi tu na ndio maana wanaamini kuwagawia watu PhD za 'juu kwa juu'!
  Anyway, poleni maana katika hali ya kawaida hito inapoteza concentration kwa elimu ya kitanzania
   
 11. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #11
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Mkuu umenena sawia!! Quality assurance ni muhimu sana. Ina maana wao hawakufanya review na kujiridhisha kabla ya kutoa hiyo mitihani. NBAA wanasisitiza sana mambo ya assurance lakini wao leo wanaboronga. Hii issue haiwezi kuwa immaterial hata kidogo!!
   
 12. Ikwanja

  Ikwanja JF-Expert Member

  #12
  Nov 2, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,988
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Jamani mi naungana na mleta mada, maana wamewaharibia watu mudi ya kufanya mtihani, lazima wajuuzulu
   
 13. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #13
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Una point ya maana sana hapa. Huu ni uzembe wa hali ya juu sana. Ina maana hakuna mtu anayepitia hiyo mitihani baada ya kuchapishwa ili kuhakikisha kuwa kila kitu kiko sawa?

  Mkurugenzi mkuu inabidi aeleze wanachama wa NBAA na wadau wengine ambao wana imani kubwa na NBAA ni kitu gani kimesababisha hili kutoa. Kuna mtu hapa inabidi awajibike.

  Mimi mwenyewe kama mhasibu niliyepitia mitihani ya NBAA kwa kweli hili jambo limenikera na kunistua sana. Nina pata wasiwasi na umakini wa uongozi wa hii bodi kwa sasa.

  Please, we need clear and detail explaination.
   
 14. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #14
  Nov 2, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,482
  Likes Received: 5,554
  Trophy Points: 280
  haya makosa yafanyike kwenye test za vichochoroni siyo NBAA! What's wrong with Mr Maneno and Dr Assad!!
   
 15. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #15
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kumbe Dr Assad naye anashughulika na NBAA? Huyu jamaa aliponifundisha pale Mlimani nilimuona kuwa ni mtu makini. Sasa naomba awe wa kwanza kutuambia sisi wanachama wa NBAA ni kitu gani kimetokea. Hatutaki uzembe kwenye hii board yetu. Kwani kama kutakuwa na uzembe kwenye mambo ya NBAA, professional uhasibu nayo itapata maradhara makubwa sana.
   
 16. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #16
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Tangia maneno aingie pale mambo ya NBAA yamekuwa hovyoooo!! Tatizo lingine ni kwamba NBAA ni chombo cha serikali na wala si chombo cha wanachama. Ingekuwa chombo cha wanachama ingebidi mpige kura ya kutokuwa imani na hao viongozi ili muwafute kazi lakini hao ni wateule wa Rais!!! Hivi ACCA wanaendeshaje mambo yao? ACCA ni chombo cha nani? Kuna upuuzi kama huo kweli?
   
 17. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #17
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Dr. Mussa Assad ndiye Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA!
   
 18. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #18
  Nov 2, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,482
  Likes Received: 5,554
  Trophy Points: 280
  Alafu NBAA na Bodi ya kenya na Rwanda wamesaini mkataba CPA(T),CPA(K) CPA(R) wafanye kazi kwenye nchi zao bila masharti magumu! Unafikiri Nchi gani itafaidika hapo!!
   
 19. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #19
  Nov 2, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,506
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Tanzania bwana kila kitu ni upupu tu...imefikia hadi huku? fikiria mtihani haujatungwa jana wala juzi ni ulitungwa siku nyingi na kuna pannel zikakaa kufanya editing na kuupitisha...jamani hawakuona hilo? ndio maana siku hizi inapoteza credit kabisa hii bodi inachakachuliwa sana na pilitics.


  hii ni aibu kwa bodi ya Uhasibu
   
 20. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #20
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 453
  Trophy Points: 180
  Wafanyakazi wa Bodi nao ni binadamu kama wewe!! Wakosee madaktari wa kuasua kichwa badala ya mguu sembuse hayo maandishi tu.
   
Loading...