Bodi ya Mishahara Kenya yapinga Wabunge kuongezwa pensheni

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,078
10,023
Bodi ya mishahara nchini Kenya imepinga mpango wa kuongeza pensheni kwa wabunge 375 wa zamani.

Mkuu wa bodi hiyo, Lyn Mengich, amesema iwapo wabunge wataongezewa pensheni wafanyakazi wengine wa ofisi za Umma watataka mishahara yao iongezwe pia.

Wiki hii wabunge nchini humo walipitisha muswada ambao unataka sheria ipitishwe kwa wabunge waliohudumia taifa hilo kati ya mwaka 1984 mpaka 2001- kupata $926; kama pensheni ya mwezi.

Kiwango hicho kitakuwa kimeongezeka kutoka dola 330 wanazopokea kwa sasa. Wabunge wa zamani watapokea pensheni za kila mwezi kama rais atapitisha sheria hiyo.

Wabunge wa Kenya ni miongoni mwa wabunge wanaolipwa kwa kiwango cha juu zaidi duniani na wakosoaji wanasema kuongeza kiwango cha pensheni kutaongeza kiwango cha mshahara ambao wanapata sasa
 
Eeeh Mungu tusaidie na hii bodi itoke Tz
Maana pension ya walimu ni salary ya miezi 3 ya mbunge
 
Back
Top Bottom