Bodi ya mikopo yakamilisha uchambuzi wa maombi ya mikopo, 20,183 wapata kati ya 88,163 walioomba

muchekie huyu jmn mkopo s2227/0066/2010
1477498118937.jpg
 
Baada ya kukamilisha zoezi la Uchambuzi wa maombi ya Mikopo 88,163 yaliyopokelewa hadi kufikia tarehe 11 Agosti, 2016. Jumla ya Wanafunzi wapya 20,183 wamepangiwa Mikopo. Upangaji huu umezingatia vigezo vilivyomo katika mwongozo wa utoaji wa mikopo uliopitishwa na Bodi ya wakurgezi na kuidhinishwa na wizaya ya elimu sayannsi na teknoloji. Vigezo hivyo ni pamoja na:

I. Vipaumbele vya kitaifa vinavyoendana na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka mitano, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Mafunzo ambayo yatazalisha wataalamu wanaokidhi mahitaji ya kitaifa katika fani za kipaumbele ambazo ni;
• Fani za Sayansi za Tiba na Afya,
• Ualimu wa Sayansi na Hisabati,
• Uhandisi wa Viwanda, Kilimo, Mifugo, Mafuta na Gesi Asilia,
• Sayansi Asilia, na
• Sayansi za Ardhi, Usanifu Majengo na Miundombinu.

i. Uhitaji wa waombaji hususani wenye mahitaji maalum kama vile ulemavu na uyatima
ii. Uhitaji wa waombaji wanaotoka katika familia zenye hali duni ya kimaisha
o Wadahiliwa yatima waliopata mkopo 873
o Wadahiliwa wenye ulemavu wa viungo 118
o Wadahiliwa wahitaji wenye mzazi mmoja 3,448
o Wadahiliwa wahitaji waliofadhiliwa na taasisis mbali mbali 87
o Wadahiliwa wahitaji wanaosoma kozi za kipaumbele 6,159
o Wadahiliwa wahitaji wanaosoma kozi zingine 9,867
Jumla 20,183

Kiasi cha Fedha zinazohitajika
Bajeti iliyoidhinishwa kwa ajili ya ukopeshaji kwa mwaka wa fedha wa 2016/17 ni shilingi bilioni 483, kwa ajili ya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wapatao 25,717, na wanaoendelea na masomo wapatao 93, 295.

Hatua zinazofuata
I. Wanufaika wote wanaopungukiwa na sifa watachunguzwa kwa ajili ya kurekebishiwa au kuondolewa katika unufaika wa mkopo
II. Waombaji waliwasilisha taarifa zenye upungufu, taarifa zao zitahakikiwa, na wakibainika kuwasilisha taarifa za uongo watachukuiwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kufutiwa mikopo yao
III. Wanufaika wote watatakiwa kuhuisha taarifa kwa kujaza dodoso. Taarifa za ziada za kiuchumi za wazazi au walezi wao zitatumika kutanua uhalisia. Wale watakaokutwa na hadhi zisizo stahili, watapoteza sifa za kuendelea kupata mikopo na kulazimika kurejesha kiasi watakachokuwa wamepokea tayari.

IMETOLEWA NA:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Wanafunzi waliodahiliwa ni elfu 58 iweje wewe uandike waliomba mkopo ni elfu 88

Hivi unafiki mtaacha lini nyinyi chadema??
 
Mbona Ndalichako alisema ni wanafunzi 55,000 waliomba mkopo? Kwahiyo Bodi inadanganya au Ndalichako ndio alitudanganya?
 
Wanafunzi waliodahiliwa ni elfu 58 iweje wewe uandike waliomba mkopo ni elfu 88

Hivi unafiki mtaacha lini nyinyi chadema??
we jamaa acha ushamba unadhani hlo tangazo kajitungia ingia website ya HESLB utalikuta usikae unaandika pumba!!
 
Mbona Ndalichako alisema ni wanafunzi 55,000 waliomba mkopo? Kwahiyo Bodi inadanganya au Ndalichako ndio alitudanganya?
Ndalichako ndio aliokusudia kuudanganya umma tena mbele ya rais kwa kuwa maamuzi yanatoka juu hakuna litakaloharibika rejea ishu ya WANAFUNZI wa udom
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom