Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ni Mradi wa serikali wa kukusanya mapato? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ni Mradi wa serikali wa kukusanya mapato?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Prisoner 46664, Jun 30, 2012.

 1. Prisoner 46664

  Prisoner 46664 JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 1,955
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  Salaam Jukwaa,

  Ni muda sasa nimekuwa nikikereketwa na jinsi ambavyo wizara yetu ya elimu ilivyoamua kushughulika na ugawaji wa mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wa vyuo hapa nchini na wengineo wanaokwenda kusoma nje.

  Uchunguzi wangu binafsi unaonesha kuwa hii bodi sasa imekuwa kama a bunch of robbers,yaani kundi la wanyang'anyi wanaotafuta means ya kuchukua pesa kwa watoto wa masikini bila kujali utu wa kuona haya.

  Imejulikana kwa muda sasa kuwa bodi hii imekuwa ikikaribisha maombi ya mikopo kutoka kwa vijana walio tayari kuingia kwenye elimu ya juu,ambapo wakati mwingine,kwa sababu yenye sura ya utapeli kabisa,imewaagiza vijana kujiandikisha kwa ajili ya kuomba mikopo hiyo kabla hata matokeo yao ya form six hayajatoka.Hii inamaanisha kuwa kijana anaweza kufeli mitihani lakini akawa ameshaichangia bodi hii Tshs 30,000 ambayo ni gharama ya kujiandikisha kwa kila aombaye mkopo.maana yake ni nini??

  Katika mwaka wa masomo wa 2011-2012 bodi ya mikopo,kama vile haitoshi,ikabuni mbinu nyingine ya kukusanya fedha za watoto wa maskini.Pamoja na kuwa waombaji mikopo wote walishalipa ada ya uombaji ya TShs 30,000 kila mmoja,bodi iliagiza wote wanaotaka kukata rufaa na kuomba tena mkopo walipe tena ada ya shilingi 5,000 kila mmoja.Ijulikane kuwa mara zote hizi asilimia zaidi ya 70 ya waomba mikopo wamekosa mikopo hiyo.

  Sasa kali zaidi imetokea hivi sasa,kwa wanafunzi wanaoomba mikopo kwa ajili ya mwaka wa masomo wa 2012-2013. Bodi kama ilivyo ada,imeagiza wanafunzi wote kulipa ada ya uombaji mkopo ya tshs 30,000 kila mmoja.Uombaji huu unatakiwa kufanyika kwa njia ya mtandao tu(yaani online loan application system-OLAS).Kitu cha kushangaza ni kuwa pamoja na kuwa wanafunzi wamelipa pesa hizo,database ya bodi,kwa kipindi chote cha kuanzia April 2012 mpaka leo tarehe 30 June ambapo ni mwisho wa kujiandikisha kwa ajili mikopo,imekuwa na matatizo yasiyoisha yaliyofanya wanafunzi washindwe ku-apply.Maana yake ni nini???

  Mimi kama mwathirika,ni shahidi tosha wa wizi huu wa bodi ulio dhahiri.Baada ya kulipa fedha ya kuomba mkopo,toka mwanzoni mwa April 2012,nimekuwa nikijaribu kila siku iendayo kwa Mungu kukamilisha uandikishaji kupitia website hii lakini mara zote kumekuwa na "system error",na tatizo jingine la kushindwa kusubmit form ambayo umeshajaza kama hatua moja wapo ya uombaji huu.Kwa hivi,pamoja na kuwa mimi na wenzangu wengi tumelipa hiyo pesa ya kuomba kuapply kwa ajili ya mkopo,tumelazimika kukubali kushindwa na kukubali hiyo pesa ipotee.Je huu si wizi wa mchana??

  Bodi hii inatupeleka wapi??ni juzi tu tumesikia ambavyo fedha zinatolewa bodi kama zinazopelekwa kwa wanafunzi wa vyuo lakini zikaishia mikononi mwa wajanja huku watoto wa masikini,wenye haja ya kusaidiwa wakiishia kuamua kudrop kutoka vyuo sababu ya kushindwa kumudu gharama(mimi ni shahidi wa hili).Kwanini bodi isiweke alternatives mbili ya kuapply kwa mikopo??yani kuwe na online system pamoja na manual system??nina uchungu sana na jinsi ambavyo sekta hii ya serikali imeendelea kujiendesha kama mradi wa wizi wenye lengo la kukusanya pesa badala ya lengo la awali la kusaidia watanzania.

  Je serikali imekuwa long-con artists??

  Inaniuma.
   
 2. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mimi hapo tu ndiyo huwa nashindwa kuendelea na haya madudu! bodi imeajiri watu na inapata budget yake ya kujiendesha.

  Pamoja na hayo yote, ipo kwa ajili ya kusaidia wanafunzi (watanzania) kwa nia nzuri kabisa lakini jinsi inavyoendeshwa utafikiri watu hawajaenda shule.

  Inakuwaje bodi inayotengewa mabilioni ya fedha kila mwaka ishindwe kuwa na active smart people wanaoweza kurespond haraka kwa wateja wao (watu wanaofanya applications)?.

  Why always problems with this Loan board? Nachelea kusema watu wanatumia hii bodi kama mradi kama mwanzisha uzi ulivyosema.
  Hivi wanafikiri wanamkomoa nani? Ni wizi wizi tu, ujanja ujanja, kupenda kupandia migongo ya walala hoi ndiyo inayotutafuna hili taifa. Pamoja na hayo, hakuna kukata tamaa!

  Mdau yeyote lazima uhangaike na usife moyo mpaka kieleweke, its your life and I believe through your education and talent, you may change the lifehood of milions of Tanzania.
   
 3. Prisoner 46664

  Prisoner 46664 JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 1,955
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  WA-UKENYENGE

  Ni udhaifu tu kila sekta mkuu..sasa kwa style hii watu wakisimamisha msafara wa rais na kuupiga mawe..watastahili lawama kweli??
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Serikali dhaifu ikiongozwa na mtu dhaifu huendeshwa kidhaifu na idara zake zote zikiwa dhaifu na matokeo yake ni udhaifu wa maendeleo ya nchi ambayo udhaifu wake utakuwa kitega uchumi kwa wale wanaotumia udhaifu wa mtu katika maendelo yao. PERIOD!
   
 5. CYBERTEQ

  CYBERTEQ JF-Expert Member

  #5
  Jun 9, 2013
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 7,451
  Likes Received: 207
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha sana kuona hii system ya online application inakuwa na matatizo kiasi cha kukatisha tamaa vijana. Ikumbukwe kuwa wengi wa hawa vijana wanaishi vijijini, na ili kujaza fomu hizi ni lazima watumie internet, hivyo wanalazimika kwenda mijini kwa ajili ya kufuata huduma hii, matokeo yake wanakuta mfumo unasumbua kuliko maelezo. Ni wiki nzima sasa server za HESLB zimeshindwa kuhimili wingi wa watu na vijana wanalazimika kupanga Guest House, huku wakizunguka na Bahasha zao kila siku kufuatilia fomu za mkopo. Syetem hii inasumbua sana, na hata muda wa usiku wa manane ambapo watumiaji wanakuwa wachache bado MPESA Transaction IDs zinasema hazitambuliki kwenye system kwa zaidi ya wiki sasa, na HESL wakipigiwa simu inachukua juhudi ya ziada kuwapata (nadhani mhudumuni mmoja au wawili), na hata wakipatikana hawana msaada zaidi ya kusema "jaribu baada ya masaa kadhaa"!! Haiingii akilini website yenye traffic kubwa mno kama JF, tena ya wajasiriamali binafsi inakuwa haisumbui, wakati huo OLAS ambayo naamini ilighalim pesa nyingi za walipa kodi inakuwa Janga kiasi cha kuwakatisha tamaa vijana, na hakuna anayeonekana kujali, kila mtu yuko kiimya kama hakuna kinachoendelea!!

  Kwa hakika ningependa kufahamu, hivi;
  1. OLAS ilitengenezwa na nani?
  2. OLAS ilitengenezwa kwa ghalama gani?
  3. HESLB wana mkakati gani wa kuboresha upatikanaji wa OLAS?
  4. Ni juhudi gani ambazo wanafanya ili kuwapunguzia usumbufu na gharama watu wa vijijini?

  ......Kweli Tanzania Bado Tuna Safari Ndeeefu!>>>>
   
 6. Queen Kan

  Queen Kan JF-Expert Member

  #6
  Jun 9, 2013
  Joined: Dec 26, 2012
  Messages: 3,424
  Likes Received: 4,129
  Trophy Points: 280
  Sina hata hamu nao! Wamekata hela zangu na hawajanitumia wala kunijibu chochote!
   
 7. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #7
  Jun 9, 2013
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,951
  Likes Received: 1,275
  Trophy Points: 280
  hela gani umelipa? Kama ni malipo ni M-pesa. Acheni kuwaonea kwa kutokujua kwenu
   
 8. wamogori

  wamogori JF-Expert Member

  #8
  Jun 9, 2013
  Joined: Mar 20, 2013
  Messages: 888
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mbaya zaidi hawatoi taarifa kuelezea kama ni atizo la kiufundi na kama linashughulikiwa au la, ni kama hawajali vile.
   
 9. CYBERTEQ

  CYBERTEQ JF-Expert Member

  #9
  Jun 9, 2013
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 7,451
  Likes Received: 207
  Trophy Points: 0
  Kama kweli umetuma kwa usahihi na umeangalia salio wamekata nakushauri uwapigie MPESA watakutumia hiyo sms bila mashaka yoyote, MPESA hawana usumbufu, tatizo ni hawa HESLB, kuna watu wametuma pesa wiki ya pili sasa wakiingiza hizo transaction ID zinagoma, wakipiga wanaambiwa jaribu baada ya masaa kadhaa! na hata kuwapata HESLB kwenye simu ni utata, nadhani wanaye mhudumu mmoja au wawili tu! Its a shame kwa kweli, lazima kuna kitu hakiko sawa hapa!
   
 10. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #10
  Jun 9, 2013
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,951
  Likes Received: 1,275
  Trophy Points: 280
  MAJIBU:
  1. IT specialists
  2. Muulize Zitto ndo m/kiti wa POAC
  3. Wakihamia ofisi mpya za Mwenge mwezi ujao
  4. Ingekuwa zamani wangekuja Dar
  Ushauri:
  jaza form usiku wakati watumiaji wachache
   
 11. Queen Kan

  Queen Kan JF-Expert Member

  #11
  Jun 9, 2013
  Joined: Dec 26, 2012
  Messages: 3,424
  Likes Received: 4,129
  Trophy Points: 280
  hao m-pesa ndio sitaki hata kuwasikia! Naomba niishie hapa
   
 12. CYBERTEQ

  CYBERTEQ JF-Expert Member

  #12
  Jun 9, 2013
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 7,451
  Likes Received: 207
  Trophy Points: 0
  :bange::bange::bange::bange::bange::bange:
  Na huo ushauri wako haumsaidii lolote yule anayekaa mpitimbi, au yule ambaye transaction ID inasema haiko kwenye system.
   
 13. Queen Kan

  Queen Kan JF-Expert Member

  #13
  Jun 9, 2013
  Joined: Dec 26, 2012
  Messages: 3,424
  Likes Received: 4,129
  Trophy Points: 280
  m-pesa wameniambia niende huko bodi ya mkopo
   
 14. CYBERTEQ

  CYBERTEQ JF-Expert Member

  #14
  Jun 9, 2013
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 7,451
  Likes Received: 207
  Trophy Points: 0
  Usikate tamaa dada, hebu funguka kidogo huenda nikakusaidia, ulifuata hatua zote za kutuma pesa KWA USAHIHI? au ulituma kama unamtumia mtu?
   
 15. Queen Kan

  Queen Kan JF-Expert Member

  #15
  Jun 9, 2013
  Joined: Dec 26, 2012
  Messages: 3,424
  Likes Received: 4,129
  Trophy Points: 280
  nilituma kwa usahihi
   
 16. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #16
  Jun 9, 2013
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  CEO wa bodi nasikia alikuwa misheni town, former employee wa NBC. Munaoijua NBC mutaelewa jinsi ilivyojaza wenye maajabu wengi. Watu wa direct employment na baadaye mafunzo kazini.
   
 17. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #17
  Jun 9, 2013
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  acha mambo ya kudadisi siku nzima the so called Bodi is another useless group of people naturing stupidity and corruption to toe. Wao ni kuiba tuuuuu tangu asubuhi hadi jioni.

  Full of stupidity unaamua kutumia M-pesa bila kujali kwamba wengine wana tigo-pesa, nk. what is special with M-pesa? Rushwa? what else can we say. can you franchise government procedures?

  Useless people!
   
 18. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #18
  Jun 10, 2013
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Kwakweli serikali haiko madarakani kwa ajili ya watu!! Iko kwa ajili ya group fulani la wachuuuzi!!
   
 19. Prisoner 46664

  Prisoner 46664 JF-Expert Member

  #19
  Jun 10, 2013
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 1,955
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  Tatizo la nchi hii ni la ki-mfumo kwa kweli,
  Kuna tabaka fulani la watu ambalo hufanya maamuzi huku likifikiri kuwa kila mwananchi ana hali kama yao ya kiuchumi,,..
  Hapa ndipo palipo na chanzo cha OLAS, Digitali, Kufukuza wamachinga wote jijini etc...
  Lakini pia waTanzania tunakosa moral authority ya kukemea utendaji huu mbovu kwa sababu tumeamua kwa makusudi kabisa kuwaachia wengine waamue future yetu...
  Tulidhihirisha hili pale tulipojiandikisha watu milioni 8 kupiga kura na hatimaye milioni 2 tu kati yetu kujitokeza vituoni..
   
 20. CYBERTEQ

  CYBERTEQ JF-Expert Member

  #20
  Jun 10, 2013
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 7,451
  Likes Received: 207
  Trophy Points: 0
  Post yangu ililenga kumsaidia huyo dada apate hiyo meseji ya Mpesa, au apotezee tu kwa sababu wote tunajua wanachofanya HESLB ni ufisadi? Labda atume pesa nyingine? Mwaka jana kulikuw ana options mbili, Airtel Money na M-Pesa lakini hali ilikuwa hiyohiyo!!!...! Wote tuna hasira, lakini wakati mwingine tusifanye hasira zetu zitusaidie kuwaza; tutashindwa.
   
Loading...