Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu mnawaibia wadaiwa wenu

papa anayevutia

Senior Member
Sep 5, 2012
153
52
Tunashukuru sana loans board kwa kutupatia mkopo ambao ulisaidia kulipia karo na michango mingine ya elimu ya juu.

Tunatambua fika kwamba ni wajibu wetu kurejesha mkopo huo. Lakini mimi nina lawama.

1. Je, mkopo wenu una riba? Na kama una riba, kwanini hamkuwataarifu wahusika juu ya riba hiyo?

2. Na riba hiyo ni kiasi gani?

3. Na riba ya mkopo wenu inapanda kwa rate gani per year?

4. Naomba kujua; inakuwaje mnaonesha viwango tofauti vya kurejesha kwa watu wenye mkopo sawasawa? Mfano; mtu alipewa asilimia 80 (80%) sawa na mtu mwingine aliyepewa pia 80%. Inakuwaje watu hawa wawili wanatofautina sana kwenye mrejesho wao? Unakuta mtu mmoja anadaiwa million 6.3 na mwingine anadaiwa million 12 wakati wote walipata 80%-kozi moja,darasa moja, mwaka mmoja na chuo kilekile?

5. Kuna baadhi ya vyuo hawakupata pesa za field na wala hawakwenda kabisa fied. How comes kwenye statement zao mmejumuisha kudaiwa pesa za field? Tena kwa viwango tofauti tofauti kwa watu wenye asilimia sawa?

6. Na tena kwanini hata wale waliopata; mfano mtu alipata 500000Tsh ila cha kushangaza kwenye statement zenu inasoma kapewa 1,000,000Tsh? Ukijumlisha na riba yenu ambayo haieleweki unakuta mtu anadaiwa 2 million?

7. Na kama mnataka uwazi, kwanini kwenye tovuti yenu hamjaweka section ambazo zinamruhusu mtu kupata taarifa zake za kudaiwa?

8. Inakuwaje aliyepata?
Nina wasiwasi kwamba, bodi ya mikopo mlitumia pesa za bodi kujinufaisha wenyewe, na kwa kipindi kile hamkuwa na mtu anaye wafuatilia. Sasa mnataka kurudisha pesa hizo kwa kuwabambikizia watu wengine.

Hilo nalo Jipu.
 
Hapa kuna jipu.bodi ichunguzwe.hizo fedha zilitafunwa na wajanja
 
Tatizo hakuna mwanasiasa wa kujitokeza kuwatetea wahitimu. Wote wanawatetea wanafunzi waliopo vyuoni
 
Bodi ya mikopo ni busha, kulitumbua hadi mdau apiwe nusu kaputi Mimi kila mwezi nakatwa 50400 lakini tangu mwaka juzi 2014 PESA haipungui kwenye salary slip inasoma mil. 8 kama kawaida kila mwaka. Magufuli tumbua hili............
 
Umefuatilia lakini maana hilo ni tatizo .
 
Hawa jamaa ni wezi, mimi mwenyewe jumla ya mkopo wangu ulikuwa kama 5.1 million, cha ajabu wakaniletea 8.4 million, nilipofuatilia majibu walionipa ni ya mkato kuwa "kuna check zinaonyesha zimepelekwa kwenye akaunt yangu ya benki. Wakaniambia nipeleke benk statement na nikawapelekea. Tangu niwapelekee hawajawahi kunijibu barua yangu, ukiwafuata ofisini wamekaa kama miungu mitu, hawana ushirikiano wamejaa dharau kama watu walioridhika sana, poor customer care.
Yawezekana kuna hela wanaiba kisha wanawawekea madeni madaiwa.
 
Kitu nilicho na uhakika nacho kinachoweza kutofautisha marejesho ya wadaiwa waliopewa mkopo wenye kufanana kuanzia asilimia mpaka kozi na mwaka wa masomo na chuo, ni muda ambao mdaiwa alienda kuripoti Bodi ya mikopo kuwa anadaiwa. Kuna kipindi walitangaza watu wakajiandikishe kuwa wanadaiwa na waanze kulipa mikopo...sisi tulioenda tulionekana 'punguani'...ila kadri muda ulivyokuwa onaongezeka kwenda kuripoti ndivyo penati ilivyokuwa inaongezeka...!
 
Tatizo hakuna mwanasiasa wa kujitokeza kuwatetea wahitimu. Wote wanawatetea wanafunzi waliopo vyuoni
Hapa wabunge wa UKAWA ingekuwa ndiyo kete yao ya kuibana hii Bodi, badala ya kung'ang'ania posho na mshahara wa Rais Magufuli!
 
Kitu nilicho na uhakika nacho kinachoweza kutofautisha marejesho ya wadaiwa waliopewa mkopo wenye kufanana kuanzia asilimia mpaka kozi na mwaka wa masomo na chuo, ni muda ambao mdaiwa alienda kuripoti Bodi ya mikopo kuwa anadaiwa. Kuna kipindi walitangaza watu wakajiandikishe kuwa wanadaiwa na waanze kulipa mikopo...sisi tulioenda tulionekana 'punguani'...ila kadri muda ulivyokuwa onaongezeka kwenda kuripoti ndivyo penati ilivyokuwa inaongezeka...!
hawa niliowatolea mfano wameenda pamoja mkuu na wakaikuta hali hivyo..si suala la kuripoti mapema
 
Kitu nilicho na uhakika nacho kinachoweza kutofautisha marejesho ya wadaiwa waliopewa mkopo wenye kufanana kuanzia asilimia mpaka kozi na mwaka wa masomo na chuo, ni muda ambao mdaiwa alienda kuripoti Bodi ya mikopo kuwa anadaiwa. Kuna kipindi walitangaza watu wakajiandikishe kuwa wanadaiwa na waanze kulipa mikopo...sisi tulioenda tulionekana 'punguani'...ila kadri muda ulivyokuwa onaongezeka kwenda kuripoti ndivyo penati ilivyokuwa inaongezeka...!
pia penalty ni ndogo ukisoma statement yao..issue ni utofauti kuwa mkubwa kiasi hicho..unataka kutuambia millioni 4+ ni penati?
 
Hiyo tofauti itakuwa ni balaa kama wata-declare kama ni penalt.Binafsi sijui System za HESLB zinafanyaje kazi maana wateja wanamalalamiko mengi sana.Na kitu kinachotakiwa hawaweki ID za wanafunzi walizokuwa wanazitumia katika vyuo vyao na madeni wanayodai pamoja na wale wanaolipa ingebidi mlipaji akiingiza ID yake aone kiasi kilichobaki.Sasa sijui wanafikiria nini maana matawi yao yapo machache sana.They are too disorganized institute.
 
Loan board nijipu kubwa sana mi nimesibir nikienda Dar niwatimbie pale ofisini kwao. Tulipomaliza chuo tuliletewa invoice za madeni yetu ambapo nilikuwa nikidaiwa jumla milioni 11 pamoja na riba yao ambayo wameipa neno flani nimesahau. Cha kushangaza kwenye salary slip yangu nimeandikiwa milioni 12 na ushee hivi. Kitu kingine ni kuona watumishi wengine wanufaika wa hyo bodi hawakatwi kwenye mishaara alafu wengine tunakatwa huu ni ubaguzi wa hali ya juu sana. Na walimu ndo tunafatiliwa sana kuliko watumishi wengine pamoja na mishaara yetu kuwa kiduchu sana.
 
Kitu nilicho na uhakika nacho kinachoweza kutofautisha marejesho ya wadaiwa waliopewa mkopo wenye kufanana kuanzia asilimia mpaka kozi na mwaka wa masomo na chuo, ni muda ambao mdaiwa alienda kuripoti Bodi ya mikopo kuwa anadaiwa. Kuna kipindi walitangaza watu wakajiandikishe kuwa wanadaiwa na waanze kulipa mikopo...sisi tulioenda tulionekana 'punguani'...ila kadri muda ulivyokuwa onaongezeka kwenda kuripoti ndivyo penati ilivyokuwa inaongezeka...!
Sasa mbona ambao hawajaenda hawafuatiliwi mpaka sasa wanajisifu sana kwamba wao hawakatwi? Wataanza kifatiliwa lini?
 
Loan board nijipu kubwa sana mi nimesibir nikienda Dar niwatimbie pale ofisini kwao. Tulipomaliza chuo tuliletewa invoice za madeni yetu ambapo nilikuwa nikidaiwa jumla milioni 11 pamoja na riba yao ambayo wameipa neno flani nimesahau. Cha kushangaza kwenye salary slip yangu nimeandikiwa milioni 12 na ushee hivi. Kitu kingine ni kuona watumishi wengine wanufaika wa hyo bodi hawakatwi kwenye mishaara alafu wengine tunakatwa huu ni ubaguzi wa hali ya juu sana. Na walimu ndo tunafatiliwa sana kuliko watumishi wengine pamoja na mishaara yetu kuwa kiduchu sana.
mkuu wameiita "loan retention fee"
 
Back
Top Bottom