Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ( HESLB) imetengeneza chuki kubwa kwa riba ya asilimia 15%

Sasa inabidi watanzania tubadilike, tuanze kufungua akaunti za akiba kwa ajili ya watoto na siyo kusubiria mikopo. Mkopo uje uwe ni suluhisho la mwisho.

Ukijiwekea mpango wa akiba kwa kweli utapunguza machungu kwa kiasi kikubwa.

Waswahili wamesema: Haba na haba hujaza kibaba.
Au kuwakatia bima ya elimu. Ni nzuri
 
Wanabodi, Moja kati ya ukatili uliofanyika na kuwaumiza watumishi wa uma na sekta binafsi ni tamko la Kuongeza riba ya mikopo ya wanafunzi kutoka asilimia 8% mpaka 15%

Vyama vya wafanyakazi na wadau wapaze sauti kuhusu riba hii ya asilimia 15% kwa vijana wetu kushushwa.Haya maamuzi ya kupandisha yalifanywa na mtu mmoja bila kushirikisha wadau ambao ni waajiri na vyama vya wafanyakazi

Serikali hata ikiongeza mishahara watumishi wa uma ni sawa na sifuri kwa sasa. Kwani mshahara ukiongezeka na makato ya Bodi ya mikopo ya wanafunzi inaongezeka

Ni wakati muafaka Mama Samia kubadili ule uamuzi uliofanywa na mtangulizi wake kwa kupunguza riba ya mikopo ya wanafunzi

Hotuba ya Mama Samia hata akisema Bungeni ataongeza mishahara bado hilo ongezeko litakatwa riba ya asilimia 15% ya Bodi a ya mikopo

Kijana aliyeanza kazi na mshahara wa TZS 1,600,000 Graduate anakatwa karibu TZS 240,000 ya Bodi ya mikopo, Hapo bado kodi ya Paye, Bado NSSF. Hata ukimuongeza huyu kijana mshahara mpaka TZS 1,800,000 mambo ni yale yale tu

Tuwaunge mkono vijana wetu kupaza sauti wanaumia sana na riba ya asilimia 15%

Serikali ijaribu kushusha riba hii

Tamko lolote la Kuongeza mishahara kwa watumishi wa uma halitakuwa na maana kama bado deni la Bodi ya mikopo litabaki asilimia 15%
Hili la riba kwa HELSB ni sawa tu na kuwafanyisha kazi wafungwa ambao hawajashtakiwa kwa kifungo na kazi ngumu.

Mwendazake angefika mwaka 2023, Tanzania ingekuwa kama Zimbabwe, tumshukuru Mungu kwa kumpeleka Jehanam
 
Bodi ya Mikopo nikikundi cha wasumbufu,wazulumaji,wavunja mkataba kati yao na wateja. Hilo hata CAG amethibitisha katika ripoti yake
Bodi wanakata makato makubwa kwani baadhi ya waliowapa Mikopo wapo sekta binafsi na wengine wamejiajiri hivyo hakuna marejesho

Zaidi sana pale bodi wapo watumishi ambao hawana vigezo vya kua pale.
Mfano Mtoto mmoja anaitwa Jacobo na Dada mmoja pale mapokezi
Hawawasikilizi maskini,yatima na wenye malalamiko ya makato. Hayo ni majipuuuuuu
 
Back
Top Bottom