Bodi ya Mikopo watafungua lini mtandao wao?

Mbona muda unazidi kwenda? Hata guidebook hawajaeka

Ushauri kwa wanaotarajia kuomba mkopo kwa 2016/2017

Muda wowote kuanzia sasa, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) itatangaza kupitia vyombo vya habari ikiwemo tovuti yake (www.heslb.go.tz) kuanza kupokea maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Tangazo hilo litatoa mwongozo wenye maelezo ya yanayojumuisha sifa za mwombaji, vigezo vitakavyotumika, katika utoaji mikopo, muda wa kuwasilisha maombi na mambo mengine muhimu.

Hivyo, basi, ni wajibu wa waombaji mikopo watarajiwa kusoma kwa makini tangazo hilo na kujipima kama wana sifa au hapana kabla ya kufanya malipo ya ada ya maombi na kufanya maombi ya mikopo.
Wito huu unatokana na uzoefu wa miaka iliyopita ambapo waombaji walipata usumbufu usio wa lazima kutokana na kutokuwa makini kabla ya kuomba mikopo.

Kundi la kwanza ni la waombaji wasio na sifa zilizoainishwa kwenye tangazo lakini walilipa ada ya maombi, wakawasilisha maombi yao na baadae kukosa mikopo na kulalamika.

Kundi la pili ni la waombaji wenye sifa zilizoainishwa lakini hawakuwa makini na hivyo kushindwa kutimiza matakwa ya mwongozo uliotolewa.

Maombi ya mkopo wa elimu ya juu ni kama maombi ya kazi au mtihani. Kwa kazi, mwombaji anapaswa kusoma sifa zilizoanishwa na utaratibu wa kuwasilisha ombi lake. Hivyo basi, ikiwa nafasi ya kazi inahitaji msomi wa shahada ya kwanza, mtu mwenye stashahada hatakuwa na sifa ya kuomba.

Aidha, mwanafunzi akiwa kwenye chumba cha mtihani, ana wajibu wa kusoma masharti ya mtihani kabla ya kuanza kujibu maswali. Asipofanya hivyo, si ajabu akajikuta anajibu sivyo na kushindwa vibaya mtihani husika.

Mwaka jana, kwa mfano, Bodi ilipokea maombi zaidi ya 68,000 ya mikopo. Kati ya hayo, fomu za waombaji wa mikopo 7,788 zilizopokelewa na kuhakikiwa ziligundulika kuwa na upungufu na waombaji waliokosea walipata gharama za kufika ofisi za HESLB jijini Dar es Salaam ili kufanya marekebisho.

Fomu hizo zilikosa taarifa muhimu kama sahihi za waombaji, nakala za vyeti vya kuzaliwa vya waombaji, sahihi na picha za wadhamini na baadhi ya fomu za maombi kutosainiwa na waombaji wenyewe au wanasheria na maafisa wa serikali za mitaa kama mwongozo wa uombaji mikopo unavyotaka.

Nimalizie kwa kuwasihi wadau wote, hususan watu wanaotarajia kuomba mikopo HESLB kwa mwaka wa masomo 2016/2017, kusoma kwa makini mwongozo utakaotolewa na kuuzingatia wakati wa kufanya maombi ya mkopo kuondoa usumbufu usio wa lazima.

Tuandikie: info@heslb.go.tz au tutembelee kwenye ukurasa wetu wa
 
Form6 kashika smart4n sasa ni sheeder..!!
Kuhusu guidebook bado sana mpaka matokeo yakitoka na wanaohusika na kutoa guidebook ni TCU na sio loan board, kuhusu app za mkopo subr kidogo tu ndio mida yenyewe hii, BTW karibu kwenye ulimwengu wa course work na sup
 
Form6 amepewa smartphone ni shidaa anaona muda unaendA na tena ana uhakika wa kufaulu basii daah safi sanA
 
subira yavuta heri.........vijana msi-panic,,,,,mambo yatakuwa vizuri soon......no need to worry......
 
Subiri bajeti ya wizara ya elimu isomwe na kisha kupitishwa na wabunge nadhani j3 watu wanaanza kuomba bodi
 
mpaka lini kwani leo ni tarehe 25/5 na tarehe 1-5/6 wanatakiwa JKT.
 
Back
Top Bottom