Bodi ya mikopo wana fobia na teknolojia ya tehama?

inspectorbenja

JF-Expert Member
Oct 14, 2012
495
418
Nimesikitishwa sana na mwenendo mbovu na duni wa bodi ya mikopo katika matumizi ya tehama.

1.Mpaka leo deni halisi la bodi ya mikopo na salary slip vipo tofauti.Nashindwa kuelewa kuwa uongozi wa bodi ya mikopo umeshindwa kabisa kuwatumia watalaamu waliobobea teknolojia ya tehama kufanya link kati ya statement za bodi na salary slip. Je huu ni uzembe,kufanya kazi kwa mazoea au wameamua tu kupuuza

2.Kushindwa kutoa online statement.Kama wizara ya fedha wamefanikiwa kutoa salary slip online.

Bodi wanashindwa vipi kutoa statement online ambayo mtu ataitumia kupata huduma nyingine.Kitu pekee walichoweza ni kutengeneza website tena butu ambayo itakuonyesha salio ila wakikuambia statement utatumiwa kwenye email.Mfumo wao ni butu na ulishafeli,haujawahi kutuma statement.Wanashindwa hata kwenda kujifunza MOF.Kama wangekuwa wanamaanisha biashara wangetengeneza mfumo ambao ukiingia tu unapata statement online.

3.Email ya mawasiliano waliyoweka kwenye website yao ni non functional.Namba za simu walizoweka hazipatikani.Huduma ni mbovu na hakyna anayejali.Yaani mtu kama una tatizo mpaka upige namba binafsi ya mfanyakazi wa bodi.Je uongozi wa bodi umeoza kiasi hiki hili tatizo haulioni.

4.Ukienda kupata huduma kwenye ofisi zao.Kupata tu statement unajaza fomu leo unaambiwa unakuja kuchukua kesho. Kweli jamani statement kitu cha dk 1 au 2 ndo kinawekewa urasimu mkubwa wa namba hiyo.
Uongozi wa bodi nadhani aidha wanafanya makusudi kusababisha urasimu na kero hizi,aidha uongozi wa bodi una phobia na matumizi ya tehama

Ninaomba usalama wa taifa,wizara husika na vitengo vingine vya serikali viimulike bodi hii ya mikopo.

Kwanini hawataki kutatua changamoto hizi kwa teknolojia wanatesa watanzania kiasi hiki.

Shame upon uongozi mzima wa bodi ya mikopo.Zama hizi za teknolojia wanafanya kazi kizamani.

Aibu kwao tena kubwa.
 
Back
Top Bottom