Bodi ya mikopo tujaribu ubunifu zaidi baada ya nguvu bila maarifa

Mpogoro

JF-Expert Member
Dec 7, 2008
386
225
1568887043541.png

Siku chache zilizopita nilitumiwa picha ya frontpage ya gazeti moja likimnukuu Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu akisema "Wadaiwa Bodi ya Mikopo Kusakwa Majumbani Usiku" nikashtushwa kidogo nikasema nitakapopata muda nitajaribu kuweka bandiko moja hapa nitoe maoni yangu kuhusu ulipaji wa mikopo ilu tupate kujadiliana.

Kwanza niweke wazi mgongano wa maslahi hapa kwamba mimi ni mnufaika wa bodi ya mikopo ya elimu ya juu ambaye sijaanza kulipa mkopo wangu, kwamba tamko hili la Mkurugenzi la kufuatwa nyumbani usiku linanihusu moja kwa moja.

Changamoto kwenye ulipaji wa mikopo:

Changamoto kwenye ulipaji wa mikopo ni jambo la kawaida sana, bodi ya mikopo si taasisi pekee ambayo inakumbwa na changamoto hii. Tunaona taasisi za kifedha kama mabenki, ushirika mbalimbali zote hizi zinakumbwa na changamoto za namna hii.

Mara nyingi kushindwa kwa watu kulipa madeni husababishwa na mambo mengi ikiwa ni pamoja na suala zima la kipato, kukosekana kwa mifumo thabiti na rafiki ya ukusanyani wa marejesho ya madeni na wakati mwingine inaweza kuwa hulka tu ya mkopaji kutopenda kulipa madeni yake.

Inapokuja suala la ulipaji wa mikopo ya elimu ya juu nafikiri changamoto kubwa si hulka ya wakopaji kutopenda kulipa, nafikiri hili tuweke pembeni kabisa. Lakini pia sidhani kama kipato ni sababu hasa ya watu kukosa kulipa, nafikiri sehemu kubwa ya watu waliofaidika na mikopo pengine wanaweza kutoa kitu katika kujaribu kulipa haya madeni licha ya kwamba nchi yetu imekubigwa na tatizo kubwa la ajira.

Mimi naamini kuwa wanafunzi wengi waliofaidika na mikopo ya elimu ya juu ni wazalendo sana na wangependa kurejesha mikopo yao ili kuwezesha wengine pia wasome. Na nafikiri huu ndio uungwana, kwamba kama jamii yako imekuwezesha basi nawe unalazimika kufanya kitu kurudisha ili kuendelea kujenga jamii iliyokuwezesha.

Hivyo kwa mtazamo wangu nafikiri changamoto hasa inayosababisha matatizo kwenye ulipaji wa mikopo ni kukosekana na mifumo thabiti na rafiki ya ukusanyaji wa mrejesho ya mikopo toka kwa wadaiwa.

Kukosekana kwa mifumo thabiti na rafiki ya ukusanyaji wa marejesho ya mikopo:

1. Upatikanaji wa taarifa za madeni/marejesho:
Mpaka sasa upatikanaji wa taarifa ya madeni ni changamoto na wakati mwingine hata unapopata taarifa yenyewe unaitilia mashaka. Je, haiwezekani kuwekeza kwenye mfumo rafiki utakaowezesha upatikanaji wa taarifa hizi kirahisi zaidi?

Kwa upande mwingine kama mtu tayari amekwisha anza kulipia mkopo wake, bodi haiwezi kuweka mfumo ambao mtu anaweza kujua kiasi alicholipa na baki mara anapotaka?

Naona wizara ya ardhi kwa sasa inaruhusu watu kulipa ada za viwanja kwa njia ya mtandao, yaani si tu unaweza kujua kiasi unachodaiwa bali unaweza pia kulipia kwa mobile money na hata credit card. Ni ndugu na jamaa walio nje ya nchi ambao kila mwaka sasa wanaweza kulipia ada za viwanja vyao bila kumbugudhi mtu.

Bodi haiweze kujifunza toka kwa taasisi nyingine za serikali?

2. Matumizi ya sheria ya ulipaji wa mikopo:
Nafikiri kufuata sheria ni kitu kizuri sana lakini kufuata sheria tu bila kuangalia hali halisi ni upuuzi kabisa wakati mwingine. Sheria ya ulipaji wa mikopo sidhani kama ni rafiki, licha ya kwamba ulipaji bado ni changamoto bado sheria inataka kuwe na penalties na retention fees.

Sasa sikatai kuwepo kwa penalties na retention fees lakini je, haiwezekani bodi kuja na programu zitakazoweza kumfutia mdaiwa hizi gharama za ziada ikiwa anataka kulipa deni lake mara moja. So kwa mfano mtu alikopa milioni 10 lakini retention fees na penalties zinafanya mkopo wake huwe milioni 13, haiwezekani kutoa "incentive" kwa mtu ambaye yuko tayari kulipa 10 milioni yake na kusamehewa hiyo milioni 3 ya penalties na fees?

3. Ubunifu na matumizi ya teknolojia ya mawasiliano:

Wakati bodi inajikita kukata pesa toka kwa wadaiwa walio kwenye mfumo rasmi wa ajira, je, sisi ambao tulio kwenye mfumo usio rasmi wanatusaidiaje?

Siku hizi watu wanatumia simu kwa ajili ya kila kitu, bodi haiwezi kuleta mfumo utakaowezesha watu kulipia mikopo yao popote wawepo? Kwa mfano watu walio kwenye Diaspora, je wana njia rafiki za kufanya marejesho?

Nafikiri bodi inapaswa kuondokana na mtazamo tu kuwa matumizi ya nguvu na sheria ndiyo yatakayopelekea watu kulipa mikopo yako. Fikra ya kutumia nguvu bila maarifa na ubunifu ndiyo imeifikisha hapa ilipo.

Matamko haya ya kutisha wadaiwa nayo hayasaidii kabisa, yaani pengine ndio yanayochangia kuzorota kwa makusanyo. Pengine bodi ijikite kwenye ubunifu zaidi na matumizi zaidi ya teknolojia.

Ikiwa bodi itaweza kuwa na utaratibu hata wa kuwezesha mtu kuweka 50,000 kila mwezi inaweza kuwa na makusanyo makubwa zaidi hasa toka watu wasio kwenye mfumo rasmi wa ajira. Pia kuna nafasi kuwezesha kupata marejssho mengi toka kwa Diaspora.
 

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,447
2,000
Kwani hao walioajiriwa hawalipi KODI? sasa unawadai nini zaidi ya kuwasomesha upate kodi yako, UJINGA MWINGI AISSSEEE
 

Michibo

JF-Expert Member
Feb 16, 2015
1,870
2,000
Naona unajaribu kuwahadaa eti wadaiwa tuna uzalendo ishia huko huko, serikali yetu inazo hela nyingi kugharamia elimu ndiyo maana haihangaikii marejesho yenu.... kama unajiskia kulipa mkuu kalipe tu ila sio kama umetishwa na huo mkwara mbuzi.
Kuna kipindi walitoa majina yote eti wadaiwa sugu, unawasaka usiku kwenye kumbi za starehe ili uwapeleke wapi kwanza huna taarifa zao na wala sio waharifu (kama ni sheria mharifu ni wao waliovunja mkataba kutoka 8% to 15% kimabavu).... huo ni mkwara uchwara tu kama mikwara mingine.
Serikali inasomesha wananchi wake ili kupata miongoni mwake watumwa itakaowalipa kidogo na kuwakata kodi, wale waliobaki mtaani au nje ya mfumo rasmi basi sio sehemu ya mpango wa serikali.... wametunyima ajira baada ya kutupotezea muda wetu darasani tumekubali hilo basi nao wasitubughudhi.
 

BOB OS

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
3,332
2,000
dawa ya deni ni kulipa niliona mtandaoni jamaa moja yeye walimtumia SWAT kudai deni lao huko marekani,,,,
 

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,149
2,000
Hawa bodi ya mikopo hawafanyi kazi na wala hawafikirii.
Leo kuna sekondari na vyuo binafsi vimeajiri watu wanaodaiwa na hawajawahi kulipa hata senti tano.
Kuna taasisi zinazojulikana wazi pamoja na mashirika yanayolipa vizuri lakini wapo wameajiriwa humo na hawajawahi kudaiwa.
Ni kiasi cha kuomba takwimu ya waajiriwa kutoka taasisi hizo na bila shaka watapata wengi.
Au pengine naanza kuwa na wasi wasi kuwa hawa watu wanakula mlungula na kukwepa kuziwajibisha taasisi zinazoajiri bila kutoa taarifa ya wadaiwa wa bodi ya mikopo.Kwani adhabu ya faini ni kubwa kwa taasisi isiyotoa taarifa za wadaiwa.Taasisi zinawajua vema watu hawa.Nina uhakika na hili na hata kama wanahitaji tuwaambie tunaweza kuwaambia.Nionacho mimi hawana nia ya dhati kukusanya mikopo hii,ila wanafanya kazi kisiasa kelele nyingi magazetini,utendaji sufuri.
Mnampa kazi kweli Rais,atamaliza muda wake anang'oa watu wazembe tu na watu wamegoma kufanya kazi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom