Bodi ya Mikopo ongezeni tozo walau ifike 20%

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,042
20,404
Bodi ilianzishwa mwaka 2005 kwa lengo zuri kabisa la CCM ya KIKWETE kusaidia wanyonge. Wakurugenzi wengi walipita, Nyatega ambaye baadaye alitumbuliwa alikuwa mtu mzuri na pia alipata kashfa ya kuweka fedha hizo kwenye FIXED account kabla ya kuwapatia wanafunzi, maandamano hayakuisha na Kikwete hakuelewa sababu ya wanafunzi kuandamana wakati fedha ilishatoka hazina.

Mwaka 2015 lipoingia Magufuli kwa Mbwembwe ikajulikana mambo yatabadilika, lakini Bodi Mpya ikiongozwa na:

1. Madina Mwinyi, Richard Masika, Prof Anangisye, Abdul Razak Badru, Suzan Urion na Frank Mgetta wao hawaumizi kichwa ni vikao tu kudai fedha toka hazina lakini hawahangaiki na kukusanya fedha zilizopo nje pamoja na kwamba wamekuwa wakijulishwa hivyo mara nyingi tu na wasamaria wema.

Mh. Magufuli, sisi wanufaika tunaomba mje kuchukuwa hela, tunazo, tunataka watoto wetu wasome na marejesho yetu

1. Wanasheria wote, kabla ya kupata uwakili apewe invoice yake, aanze kulipa 20%

2. Wahasibu, na wengineo. Wanasheria wanakuja mahakamani, wana kesi za fedha nyingi lakini anakwambia halipi maana hakuna anayemfuatilia.

Kwakuwa BODI YA HESLB imelala na ina m-subotage Mpendwa wetu Magufuli, basi kama ikimpendeza, aitumbue, aweke wachapa kazi, waje mtaani tuwataje waliokopa na tulio wadhamini maana tunawajua, lakini hata watoto wetu wanataka kulipa la BODI haina mpango kabambe.

Kwa sasa tunalipa 15% ambayo ni ndogo kulinganisha na tunachopata kwa Mwezi na Tanzania imekuwa nchiya uchumi wa kati, basi wapandishe mpaka 20% na pia tuwekewe e mail ya kutuma majina ya wanufaika, namba zao za simu na walipo.

 
We umelewa au chuo chenyewe hujasoma.
Wanakata 15% we unasema 8%

Unaomba waongeze iwe 20%, unajua kwamba hiyo 15% ni ubabe sio mkataba tuliosaini?
Au unataka kujipendekeza kwa nani?
Unajua kama value retention fee inaumiza watu na deni haliishi?

Katika siku umeandika mambo ya kipuuzi ni leo
 
We umelewa au chuo chenyewe hujasoma. Wanakata 15% we unasema 8%

Unaomba waongeze iwe 20%, unajua kwamba hiyo 15% ni ubabe sio mkataba tuliosaini? Au unataka kujipendekeza kwa nani?
Unajua kama value retention fee inaumiza watu na deni haliishi? Katika siku umeandika mambo ya kipuuzi ni leo.
Mkataba unaweza kubadilishwa, hata mikataba ya Madini ya Mkapa imebadilishwa na mpendwa wetu Magufuli, na Wamelipa mabilioni ya kodi, huo wa Bodi itashindikana nini?
 
Nimekuelwa lakini unawakejeli watu hapa ndugu yangu
Nimerekebisha, hiyo 15% ni ndogo mkuu, wale wenye sababu maalum waandike barua, ambapo najua hawapo, vijana wengi wakimaliza chuo hata kama hama kazi ananunua ka gari, gheto la kisasa, nguo kama msanii, lakini halipi hata 20% alichokopeshwa na wanyonge? its totally unfair, tumuunge rais mkono kwenye mambo ya elimu kama BODI YA HESLB imeshindwa.
 
Hebu tulia kwanza, mbona una mhemko sana, 8% ni sawa kabisa, we kama unalipwa milion10 sawa wengine tupo kwenye mashirka makubwa lakini tunachezea around 2m_3m bado makato, bado mikopo binafsi tuliochukua tukiwa kazini yenye makato miaka saba ambayo makato ni laki 5 kwa mwezi,

Ukiwa unasemea nafsi yako binafsi angalia majority watakua affected kwa kiasi gani, 8% ni very fair, sasa wewe unataka 20%, wakikata hiyo 20% 1/3 nitashindwa hata kuchukua salary advance.
 
Back
Top Bottom