Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa vyuo(HESLB); Taasisi ya Serikali iliyorasimishwa kuwatapeli wanyonge

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,684
2,157
TAASISI ILIYORASIMISHWA KUWATAPELI WANYONGE

Bodi ya Mikopo imewanufaisha watanzania wengi sana ikiwa ni pamoja na kuwajengea watanzania misingi ya kielimu kwa ajili ya future katika maisha yao . Aidha, Asilimia 80 ya wanufaika wa mikopo ya bodi ni wale kina KAYUMBA Yaani watoto wa maskini.

Sheria ya mwaka 2016 ya bodi ya mikopo iliyofanyiwa marekebisho ni sheria ANGAMIZI kwa watoto maskini.

Sheria imeweka wazi ( Watz wengi hawana tabia ya kujisomea) kuwa marejesho ya mkopo yatakuwa ni kwa 15%, na deni hilo litakuwa linaongezeka kila mwaka wa fedha kwa asilimia 6% ya deni halisi la mwanzo.

Kwa mfano.
Daktari ambae amesomeshwa na bodi, asilimia kubwa deni lao huwa kati ya mil 25 mpaka 30.

Basic salary yake ni 1.5 Mil
Makato ya mshahara wake ni kama ifuatavyo,

Helsb 225, 000 TSH
PAYE 295,090 TSH
NHIF 42,420 TSH
Pension. 80, 000

Total deduction 642, 510 TSH
take home yake ni 857,590 TSH —ana watoto na anasomesha!
-----------------------------

Kwa sheria ya bodi ya mikopo, huyu bwana kwa mwaka ataweza kulipa 2.7Mil ( 225,000X12)

Hivyo katika deni lake la 30Mil , atakuwa amepunguza deni lake hadi 27, 300,000TSH ikifika mwisho wa mwaka wa fedha.

Mtu huyu atapaswa kuanza mwaka wa fedha mpya akiwa na deni la 27, 300, 000 TSH.

Lakini sheria ya bodi inasema hapana, unatakiwa kuongezewa 6% ya 30 mil ambayo ni 1.8 Mil

Hivyo deni analopaswa kuanza nalo ni 27,300,000+ 1.8 Mil sawa na 29, 100, 000 TSH.

Kwa mwaka unaofuata tena, atafanikiwa kuipunguza hiyo 29,100,000 Mil hadi 26,400,000 Mil na ndiyo ni kianzio cha deni lake kwa mwaka mpya uliofuata.

Sheria ya bodi itasema hapana, hii 26,400,000 lazima iwekwe 6% ya 30Mil ambaye ni 1.8

Hivyo 26,400,000+ 1.8 mil

Deni jipya kwa mwaka mpya uliofuata itakuwa ni 28,200,000Mil badala ya 26,400,000 and the list goes on.

Yaani utakuwa unakwenda mbele na kurudi nyuma mpaka unastaafu.

Sheria ya mwaka 2016, inazidi kusema kuwa, ikiwa muhusika mpaka anastaafu, hajafanikiwa kumaliza deni lake, basi pension yake itafidiwa.

Yaani, Ikiwa una pension ya 15 Mil , na deni lako lilibaki 20 Mil , Bodi itakula zote 15 Mil na itakudai 5 Mil na hiyo 5 mil itazidi kuongezeka kadiri miaka inavyokwenda mbele, ni hatari sana na mbaya zaidi watumishi wengi hawajui hii sheria.

Ikitokea pension yako imeliwa yote na bodi,maana yake unazeeka ukiwa huna kitu.

I just can't figure it out , ni sheria kandamizi dhidi ya mtoto maskini iliyopitishwa na wabunge wetu tukufu.

Ni kwamba mtoto wa maskini hatoweza kumaliza hili deni , ni deni la maisha hasa waliosoma makozi ya sayansi kama udaktari, Nesi, famasi , na injinia na wale waliosoma nje ya nchi.hawa wote madeni yao si chini ya 25Mil or so. It is a detrimental to these poor people, and Unfair.

Mapendekezo

1. Serikali ipitie upya hii sheria, na ifutilie mbali hiyo incremental ya 6% kwa kila mwaka, it is not even practical, watu wengi wanakufa na hayo madeni tena bado yakiwa makubwa mno.

2. Irudishwe asilimia 8% au 10% badala ya 15% ya makato ya bodi, kwa sababu watumishi wa umma ndiyo wanufaika na hii mikopo, na wengi wanaangamia hali zao malikiti sokoni.

3. Bodi ya Mikopo itoe elimu maredioni juu ya utaratibu wa urejeshwaji wa haya makato WaTZ wengi haijui kitu kuhusu mambo ya sheria.

4. Sheria ya kuchukua pension ya watumishi walioitumikia serikali hadi kustaafu itolewe kwa Sababu ni mateso makubwa yatakuwa kwa hawa watu na hii ni jamii yetu inayoitumikia serikali ya Jamhuri miaka nenda rudi.

Watumishi wa umma wengi wanastaafu wakiwa maskini na fukara, uwachukulie tena hizo pesa za pension, kweli ? Doh tutapata laana katika nchi.

USHAURI.

1. Kwa wazazi ambao wanajiweza, achaneni na mambo ya kuwasukumizia watoto wenu kwenye mikopo mpaka muelewe vyema sheria ya marekebisho, hiki ni kilema cha maisha kwa wale ambao deni lao ni above 20Mil.

2. Pia wahusika hakikisheni mnaipitia hii sheria na muelewe marejesho yake, you need to take precaution. Kama huelewi mtafute Mwanasheria akuelewesheni ni hatari sana fuatilieni haya mambo.

C&P

Huo ni mfano wa Daktari tu anayepokea mshahara angalau Mil.1.5. Mfikirie Mwalimu mwenye deni Kama hilo (hasa waliosona private University au sayansi) anayeanza na mshahara wa Tsh.760,000/-(TGTSD)
 
Ndugu walimu wenzangu na wanufaika wote waliosomeshwa kwa fedha ya serikali yaani BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU (HESLB),

Juzi Jumatatu tarehe 28.12.2020 niliomba LOAN STATEMENT ya deni langu kutoka Bodi ya mikopo ili niweze kuclear deni baki ambalo kwa mujibu wa SALARY SLIP yangu ya 31.12.2020 Deni linasomeka Tsh. Mil 4.65.

Aidha, cha kushangaza na kushtua jana HESLB wakanitumia kwa njia ya email statement ya deni langu ambapo Deni langu linasomeka nadaiwa Tsh. Mil 12.087 wakati kwenye Salary slip ya mwezi deni ni Tsh. Mil 4.65.

Kiukweli nilichanganyikiwa nikawatumia ujumbe Bodi ya mikopo kuomba ufafanuzi wa hiki na leo Jumatano asbh nikajibiwa kuwa hakuna kilichokosewa kwenye statement waliyonitumia jana.

Baada ya kuona sielewi imelazimika nisafiri hadi Halmashauri kuonana na AFISA UTUMISHI ili aweze kunipa ufafanuzi wa jambo hili.

Nilipofika akampigia simu AFISA kutoka makao makuu ya HESLB ambaye ndo anashugulika na makato ya fedha zote kutoka kwa wanufaika wote nchini, alimpigia palepale mbele yangu na akaweka Loud speaker yule Afisa wa Bodi akaeleza mambo mengi sanaa kuhusiana na fedha hii.

Kiujumla amesema kwamba watumishi wote tunaokatwa kupitia mishahara yetu deni tunaloliona kwenye hizo salary slip kama linapungua sio deni halisi bali deni halisi analodaiwa mnufaika wanalo wao Bodi kwenye mfumo wao ambao mfumo wao hauna mahusiano yyte na Mfumo wa Lawson.

Hivyo deni letu halisi huwa haliwi updated kwenye salary slip ndo maana tunaona kila mwezi linapungua ila kiuhalisia ni hapana

Akaendelea kusema mtumishi yyte akitaka ajue deni lake halisi analodaiwa basi aombe Loan Statement kutoka Bodi hapo ndo anaweza kujua deni lake halisi ambalo ni tofauti sanaaa na linaloonekana kwenye Salary slip zetu

Akasema tena deni lililopo kwenye salary slip linapokwisha mtumishi anaweza akaona kama vile kamaliza deni, kumbe kuna deni kule bodi bado wanamdai.

Hivyo akasema sasa hv wapo kwenye mchakato wa kuandaa barua kuwatumia waajiri wote nchini madeni mapya ya wale wote ambao washakamilisha kulipa deni la kwenye salary slip ili makato yaendelee kama kawaida

Mwisho Afisa huyo akamuomba Afisa Utumishi anipatie mimi namba yake ili kama kuna mahali nitakuwa sijamuelewa vzr niweze kumpigia wkt wwte kwa maelezo ya kina

Hivyo ndug watumishi na walimu wenzangu ambao ni wahanga wa hili tusijipe matumaini ya kuclear hili deni tunaweza hata kustaafu nalo.

Tupambane kutafuta hela ili watt wetu tuwanusuru na kuingia kwenye hili janga la Bodi ya mikopo ili tuwasomeshe kwa fedha zetu hata kwa kujibana maana inauma sana.

Yeyote atakayehitaji namba ya simu ya huyu Afisa kutoka HESLB kwa ajili ya maelezo ya ziada anaweza kunitafuta inbox nikamtumia.
Asante

Copy &paste
 
Kuna wakati nachukia kweli kutupwa huku chaka ila kuna muda tena huwa namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniweka niishi huku kijijini maana kwa mambo kama haya kama ndo upo nao karibu unaweza jikuta umewazomea au umevurumishia mawe nyumba zao na magari yao ukaswekwa ndani uozee jela!

Alhamdulillah, EVERYTHING IS PLANNED
 
Uyu mwalimu anadaiwa Ela ya kujengea STANDADI GEJI
JamiiForums1313044769.jpg
 
Back
Top Bottom