Bodi ya mikopo kuwatolea nje watoto wa wakulima hawa kwa upupu huu?

Also me

Member
Aug 17, 2011
67
10
katika harakati zangu za pimbi leo cnikafongua website ya wanaojiita wakopeshaji nimekutana na upupu huu hapa; MAOMBI YA MIKOPO KWA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA ELIMU YA JUU KATIKA AWAMU YA PILI (SECOND SELECTION) KATIKA MWAKA WA MASOMO 2011/2012 1.0 UTANGULIZI Kufuatia kutolewa kwa matokeo ya udahili kwa awamu ya pili na Tume ya Vyuo Vikuu, kumekuwepo na wanafunzi wanaofika kwenye ofisi za Bodi ya Mikopo kuulizia juu ya upatikanaji wa mikopo. Kutokana na hali hii, Bodi inapenda kutoa maelezo kwa wanafunzi hao na Umma kwa ujumla juu ya suala hili kama ifuatavyo: 2.0 UTOAJI MIKOPO KWA WANAFUNZI KATIKA MWAKA WA MASOMO 2011/2012 Bodi ya Mikopo, kwa mwaka wa masomo 2011/2012, imekwishapanga kutoa mikopo kwa wanafunzi 24,628 kati ya wanafunzi 37,924 wa mwaka wa kwanza waliodahiliwa katika duru ya kwanza (First selection). Hivyo, Bodi inapenda kuwataarifu wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza na Umma kwa ujumla kuwa bajeti ya ukopeshaji kwa mwaka wa masomo 2011/2012 imekatikia kwa idadi ya wanafunzi waliofanikiwa kupata mikopo kutoka kwenye kundi la "First selection" ambamo pia takriban wanafunzi 13,296 hawakuweza kupata mikopo. Hivyo, hakuna tena fedha za ukopeshaji kwa wanafunzi wengine. 3.0 HITIMISHO Waombaji hao wa mikopo na Umma kwa ujumla wanataarifiwa kuwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya elimu ya juu katika duru ya pili au watakaochaguliwa katika duru nyingine zitakazofuatia kuwa hakuna mikopo itakayotolewa kwao kutokana na fedha za ukopeshaji kuishia kwa wale wa duru ya kwanza. Aidha, wakati wa udahili wao, wanafunzi hao wa duru ya pili na duru zilizofuatia, walielezwa bayana na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kwamba hawatahusika na mikopo na hivyo udahili wao ni kwa njia ya kujigharamia wenyewe. Hivyo, wanafunzi husika wanashauriwa kuzingatia maelekezo hayo ya TCU na kuacha kuizonga Bodi kwa kufuatilia mikopo ambayo haitaweza kupatikana kwa mwaka huu wa fedha kutokana na bajeti ya ukopeshaji kuisha. IMETOLEWA NA: MKURUGENZI MTENDAJI BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU Last Updated on Wednesday, 12 October 2011 10:00
 
CCM CCM CCM,wewe unataka bodi ya mikopo ifanye nini ? jukumu lao ni kukopesha kiasi walichopangiwa,kama kimekwisha wafanyeje na watoto wa wakulima ambao ndiyo hufanya juhudi kubwa huko mashambani kuibakiza CCM madarakani. ukipenda boga penda na ua lake. Wanaipenda CCM wayapende na yatokanayo na utawala wa CCM. ACHA MASHAMBULIZI YASIYOKICHWA WALA MIGUU KWA BODI ILI KUFICHA UPUUZI NA UDHAIFU WA SERIKALI YA CCM.
 
Ikiwakuta wataijua kua sisiemu ndio adui namba moja kwa mlalahoi,hasa mkulima wa kijijini anaendekeza ushabiki badala ya kwenda na wakati.hivi ndio kusema kuwa huko maeneo kama igunga hakuna wanaofaulu na kunyimwa mikopo ambayo ni stahili yan?im out!
 
Mi ni m1 kati ya waathilika wa ukosefu mikopo vyuo vikuu! Wanatuhimiza tusome had chuo kikuu alaf ndo wanatubwaga! Tatizo lina anzia juu, yaan rais na selikal yake. Wamehalibu kabisa feature yangu.
 
King kilipa. . . . .
na mimi ni mwathirika , inauma sana a Haki ya nani tuko weng tuliofyekwa ka nyasi then kukwanyagwa pasipo na huruma hata kidogo kwa hii serikali yetu ya ccm kwa sisi maskini kusoma tusahau kabisaaa a a a a tutakaa sana nyumbani na kushika jembe na kulipa kodi na wengind wafaidi jasho la kodi zetu
 
katika harakati zangu za pimbi leo cnikafongua website ya wanaojiita wakopeshaji nimekutana na upupu huu hapa; MAOMBI YA MIKOPO KWA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA ELIMU YA JUU KATIKA AWAMU YA PILI (SECOND SELECTION) KATIKA MWAKA WA MASOMO 2011/2012 1.0 UTANGULIZI Kufuatia kutolewa kwa matokeo ya udahili kwa awamu ya pili na Tume ya Vyuo Vikuu, kumekuwepo na wanafunzi wanaofika kwenye ofisi za Bodi ya Mikopo kuulizia juu ya upatikanaji wa mikopo. Kutokana na hali hii, Bodi inapenda kutoa maelezo kwa wanafunzi hao na Umma kwa ujumla juu ya suala hili kama ifuatavyo: 2.0 UTOAJI MIKOPO KWA WANAFUNZI KATIKA MWAKA WA MASOMO 2011/2012 Bodi ya Mikopo, kwa mwaka wa masomo 2011/2012, imekwishapanga kutoa mikopo kwa wanafunzi 24,628 kati ya wanafunzi 37,924 wa mwaka wa kwanza waliodahiliwa katika duru ya kwanza (First selection). Hivyo, Bodi inapenda kuwataarifu wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza na Umma kwa ujumla kuwa bajeti ya ukopeshaji kwa mwaka wa masomo 2011/2012 imekatikia kwa idadi ya wanafunzi waliofanikiwa kupata mikopo kutoka kwenye kundi la "First selection" ambamo pia takriban wanafunzi 13,296 hawakuweza kupata mikopo. Hivyo, hakuna tena fedha za ukopeshaji kwa wanafunzi wengine. 3.0 HITIMISHO Waombaji hao wa mikopo na Umma kwa ujumla wanataarifiwa kuwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya elimu ya juu katika duru ya pili au watakaochaguliwa katika duru nyingine zitakazofuatia kuwa hakuna mikopo itakayotolewa kwao kutokana na fedha za ukopeshaji kuishia kwa wale wa duru ya kwanza. Aidha, wakati wa udahili wao, wanafunzi hao wa duru ya pili na duru zilizofuatia, walielezwa bayana na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kwamba hawatahusika na mikopo na hivyo udahili wao ni kwa njia ya kujigharamia wenyewe. Hivyo, wanafunzi husika wanashauriwa kuzingatia maelekezo hayo ya TCU na kuacha kuizonga Bodi kwa kufuatilia mikopo ambayo haitaweza kupatikana kwa mwaka huu wa fedha kutokana na bajeti ya ukopeshaji kuisha. IMETOLEWA NA: MKURUGENZI MTENDAJI BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU Last Updated on Wednesday, 12 October 2011 10:00

Sa' upupu hapo upo wapi?! Bodi wana bajeti; na kwa bahati mbaya bodi hii haina chanzo chake cha mapato zaidi ya kile kinachotolewa na serikali. Na wao wanasema fedha walizopewa na serikali zimeisha; so ulitaka wafanye nini?! Tangazo kama hilo ni muhimu ili kwa watu wanaoweza ku-fight waanze kutafuta source zingine za ku-fund studies zao badala ya kuendelea kukanyaga lami hadi bodi. Nazani waliokosa mikopo ni kheri wakaandamana hadi wizarani kushinikiza bodi ipewe fedha nyingine(kama ipo) kuliko kwenda bodi ambao hawana chanzo cha mapato!! But all in all, ifikie wakati tukubali haitakuja kutokea serikali ikatoa mikopo ya elimu ya juu kwa 100% ya wahitaji wake--labda kwenye nchi za mafuta!
 
'Haiwezekani' NENO LINALOPATIKANA KWENYE KAMUSI YA WAPUMBAVU... bila aibu unaona haiwezekani,kwa uwepo wa watu wa mtazamo wako katika jamii yetu,tuamini tuko kwenye ncha ya maendeleo kwa upeo huo.
 
dah nami nimefyekwa ndg ila kuna njia ya kulipiza kisasi ni kujipanga kuingia msituni kukomboa watu masikini maana kila wazari anayekuja anakuaja na sera zake na si kpaumbele cha nchi ambacho ni elimu sayansi na technologia kumbuka wadau baget ilipita na hayo mapungufu hayakuepo so kawambo hatakia wat wasome coz wakwere wa kwao wanapenda kucheza ngoma na kuvaa msuri,kawambo ni kimeo ndg.
 
Back
Top Bottom