Mpira wa kona
JF-Expert Member
- Nov 25, 2016
- 350
- 338
Nimekuwa nafuatilia matamko mbalimbali yanayotolewa Na Viongozi wa Bodi ya Mikopo.Naamini mkataba wa mkopaji Na Bodi unaeleza bayana namna mkopo utakavyolipwa. Sidhani kama kuna kipengele kinachosema mkopo utalipwa Kwa kupita Nyumba Kwa Nyumba.Nawashauri viongozi wa Bodi ya Mikopo hebu fuateni Sheria kudai mikopo vitisho Na njia zisizosahihi mtakwama.Wapeni muda wadaiwa wakio makazini wajiorodheshe Kwa hiari yao Kwa waajiri wao Na wasio Na ajira wasilianeni Na wadhamini wao mkubaliane namna mkopo utakavyolipwa.Hata mikopo ya Nchi Kwa Nchi haidaiwi hivyo ingekuwa hivyo nadhani Tanzania Tungenyang'anywa BANDARI,MBUGA ZA WANYAMA n.k.