Bodi ya mikopo imetuokoa wanyonge

malimwengu

Member
Aug 29, 2011
21
12
Kama kuna kitu kilichonifurahisha mwaka huu ni vigezo vipya vya bodi ya mikopo. Yaani vimetukumbuka sisi wanyonge tusiokuwa na kitu ambao tunasomea shule duni na kila tukijitahidi kusoma kwa akili zetu tunaishia division three wakati wenzetu watoto wa matajiri wanasoma shule nzuri, tuition lukuki na kuiba mitihani wanapata wani halafu wanatesa na mikopo asilimia mia, wakifika vyuoni wanatanua tu. Sasa Bodi imewakomesha, hakuna wani wala nini, kama babako tajiri no Loan. Hureeee Bodi ya mikopo kazeni uzi.
 
Nyie wote machizi tuu! Mbona kuna waliosoma shule za serikali tena wakilipiwa na serikali na wana divsn 1 wamenyimwa mkopo. We ni kilaza ndo maana unafurahia ktendo cha kipuuzi, ila nitashangaa sana kama hauta disco wewe, na ujue huo mkopo lazma uurudishe. Kabla hujatoa mada angalia kwanza, kama ni kupewa mkopo furahia kimpango wako umepata mkopo ila sio kushadadia eti wenye division 1 wamekosa huo ni upuuzi.
 
Ha ha ha! kweli kuna watu na makatambüga! Kwa hyo maskini ndo huwa wanafeli sasa mbona shule zilizoongoza kufaulu ni za serikali.
 
Kuna watu punguani sana dunia hii, na huyu anayeisifia bodi ni wa kwanza kati watu wasiofikiri. Mimi nilisoma shule ya serikali tena kwa kuhangaika sana just imagine ada ya enzi hizo ya 35000/= ilinishinda nimelipa baada ya kumaliza chuo kikuu na kupata kazi. Sikuwahi kusoma tuition na nilipata divison 1 form form na Form 6,. Lakini kama ingekuwa ni uataratibu wa sasa hata asilimia 10 sikuwa na uwezo kulipa chuo halafu wewe unaisifia bodi tuliyoipinga sana inapoanza? akili za kuambiwa changanya na za kwako dogo ebo!!!!
 
kwa kukuonyesha unachoshabikia sio kweli mm binafsi nimesomashule zaserikali kuanzia std 1 mpaka 6 nimepata div one namkopo nimekosa. Nimewekwa kwenye kundi la Previous loanees wakati hata harufu ya chuo kikuu siijui.
Hebu nishawishi niifagilie hii bodi?!!!....
 
kuna mtoto wa dadangu naye amesoma shule ya serikali amepata div 1 amekosana loan na wazazi wake hawana uwezo kabisa kumpeleka chuo mtoto amechanganyikiwa kabisa
 
kuna mtoto wa dadangu naye amesoma shule ya serikali amepata div 1 amekosana loan na wazazi wake hawana uwezo kabisa kumpeleka chuo mtoto amechanganyikiwa kabisa
kanakurupuka tu haka katoto, wewe fikiria hata hakajaenda Chuo kanafikri maisha yapo simpo. Hakajui ukifika kule unafutilia hilo boom lenyewe mpaka mwezi mzima unapita. Ni utoto tu, kama umepata mkopo shukuru Mungu laikini usiwabeze waliokosa eti waliiba mtihani kisa wewe kilaza umefeli. Kwani Mzumbe, Illboru, Kibaha, Tosamaganga, Malangali, Msalato si shule za serikali? Nao wanaiba mitihani
 
kwa kukuonyesha unachoshabikia sio kweli mm binafsi nimesomashule zaserikali kuanzia std 1 mpaka 6 nimepata div one namkopo nimekosa. Nimewekwa kwenye kundi la Previous loanees wakati hata harufu ya chuo kikuu siijui.
Hebu nishawishi niifagilie hii bodi?!!!....
Ndugu yangu mimi nimesoma Ordinary Diploma nimeshangaa Bodi inakata ka-mshahara kangu et inanidai nimefuatilia weee had nimechoka!.Bodi ni wiz mtupu!!!!!!!!!!
 
Ha ha ha! kweli kuna watu na makatambüga! Kwa hyo maskini ndo huwa wanafeli sasa mbona shule zilizoongoza kufaulu ni za serikali.
<br />
<br />
Umeona kaka eeh?Jamaa hakufikiri vema kabla hajaanzisha thread..ni km alikuwa ana think out loud so hajachuja mawazo vizuri alipaswa afurahi tu kabahatika kupata mkopo with/or without merits na sio kuattack watu
 
Kama kuna kitu kilichonifurahisha mwaka huu ni vigezo vipya vya bodi ya mikopo. Yaani vimetukumbuka sisi wanyonge tusiokuwa na kitu ambao tunasomea shule duni na kila tukijitahidi kusoma kwa akili zetu tunaishia division three wakati wenzetu watoto wa matajiri wanasoma shule nzuri, tuition lukuki na kuiba mitihani wanapata wani halafu wanatesa na mikopo asilimia mia, wakifika vyuoni wanatanua tu. Sasa Bodi imewakomesha, hakuna wani wala nini, kama babako tajiri no Loan. Hureeee Bodi ya mikopo kazeni uzi.

Hii sasa itasababisha wazazi wengi kuwapeleka watoto wao kwenye shule za yebo yebo
 
Kama kuna kitu kilichonifurahisha mwaka huu ni vigezo vipya vya bodi ya mikopo. Yaani vimetukumbuka sisi wanyonge tusiokuwa na kitu ambao tunasomea shule duni na kila tukijitahidi kusoma kwa akili zetu tunaishia division three wakati wenzetu watoto wa matajiri wanasoma shule nzuri, tuition lukuki na kuiba mitihani wanapata wani halafu wanatesa na mikopo asilimia mia, wakifika vyuoni wanatanua tu. Sasa Bodi imewakomesha, hakuna wani wala nini, kama babako tajiri no Loan. Hureeee Bodi ya mikopo kazeni uzi.

Wewe ni miongoni mwa watanzania wabinafsi,kuna watu wengi tu wa hali duni lakini wamekosa mkopo.Acha ubunafsi
 
kanakurupuka tu haka katoto, wewe fikiria hata hakajaenda Chuo kanafikri maisha yapo simpo. Hakajui ukifika kule unafutilia hilo boom lenyewe mpaka mwezi mzima unapita. Ni utoto tu, kama umepata mkopo shukuru Mungu laikini usiwabeze waliokosa eti waliiba mtihani kisa wewe kilaza umefeli. Kwani Mzumbe, Illboru, Kibaha, Tosamaganga, Malangali, Msalato si shule za serikali? Nao wanaiba mitihani
<br />
<br />
duuh! Hapo kwenye Tosamaganga umenikuna mkuu,pamenitoa pale! Saiv natafuna pesa ya bum kama sina akili nzuri vile!
 
daaah kwel aliyeshiba amkumbuki mwenye njaa....hivi we dogo wa wapi unakurupuka tu na kuandika upuuzi bila research???? kwa hiyo umeona wale wenzako 15000 na zaidi wamesoma private na waliiba mitihan ndo maana wamekosa mkopo ????? kwanza una uhakika private wanaiba mitihani??? watu wana walimu wazuri na mazingira mazuri ya kusoma unataka wafeli sasa ??? wakifaulu wameiba mitihan wakifel hawana akili????? we dogo pumb******u.....by the way sio wote waliosoma private wana pesa wengne wamejikamua wakatafute elimu bora na sio hii yetu ya kufaulu mitihan usonge mbele.......daaah nataman ningekuona we dogo nna hasira hapa.....ahaaaaaaaaaaaaaaahhhhhhhhhh
 
hao waliomaliza form 6 na kupata one shule za serikali kama kasoma serikali mwanzo mwisho alitakiwa apate 90 au 80 na kama alimix private na gov alitakiwa 60 au 70 au 50 but imposible akose.

Je kwanini kakosa? Hapa ni mwanafunzi anaewajibika sio bodi maana kila lawama mwawatupia wao.

Now bodi ya mikopo ni computer ndio inaoselect wanafunzi wa mkopo kujaza details vibaya kwa asilimia kubwa kutapelekea we kukosa mkopo

kama ulikosa mkopo zamani poleni kwa wale walopata one na kukosa mkopo hivi karibuni waende ofisi za bodi am sure watapewa nshaona watu wanafanya hivi wanapewa nenda na barua wa dean of student wa chuo chako
 
mleta mada sijakuelewa,unasema unaishukuru bodi kwa kuwasikiliza watto wa masikini hvi umefatilia vizuri vijana wengine waliokosa mkopo au unaongea tu,mana wengine wamekosa mkopo na hawana wazazi wote wawili na wamesoma shule za kawaida sana,
 
Back
Top Bottom