Kuna kiini macho kikubwa sana ambacho waTanzania hatujakigundua katika utoaji wa mikopo kutoka Bodi ya Mikopo.
Anayepewa mkopo huo ni Mwanafunzi lakini tathmini ya uhitaji wa kumpatia mkopo Mwanafunzi huyo anafanyiwa mzazi wake. Hii ni sawa na kusema kuwa Mzazi ndiye alipaswa kuomba huo mkopo kwa niaba ya mwanaye na sio Mwanafunzi mwenyewe.
Wazazi wengine ambao wanaonekana wana uwezo wamekuwa ni chanzo cha wanao kukosa mikopo hiyo. Sidhani kama mzazi mwenye uwezo angeruhusu mwanae kukopeshwa na hivyo mwanae anapoomba mkopo na kisha tathmini ya uwezo wa huyo mzazi inapotumika kumnyima huyo mtoto mkopo inakuwa ni uonevu na ubaguzi wa hali ya juu sana.
Wazazi ambao ni wafanyakazi wa Serikalini wengi watoto wao wamekuwa wakikosa mikopo sababu tu ya wao kuwa Serikalini. Hii imesababisha watoto hawa kusoma kwa shida sana - wazazi wamekuwa wakiomba wanao wahurumiwe na karo kulipwa kidogo kidogo ili angalau wanao wasome hizo shahada. Machuoni watato ambao wanasemwa ni wanatoka kwenye familia maskini wamekuwa wakipata mikopo kwa urahisi sana na hivyo kusoma kwa raha wakishuhudia wenzao wanaotoka familia zinazosemwa na za wazazi wenye uwezo wakisota.
Mkurugenzi wa mikopo wa Bodi Bi. Nyahende ameshindwa kabisa kutambua kuwa jambo hili linaleta ubaguzi katika jamii. Mtoto wa kakangu mie ambaye anasoma udaktari amenyimwa mkopo kwa sababu baba yake yupo Serikalini anasimulia kila leo kuhusu wenzao wanavyosoma kwa raha na bila stress kwa kuwa mikopo wanapata kiurahisi tu. Watoto hawa hawafanyiwi tathmini ya uhitaji wao wenyewe lakini vinatumika vigezo vya uwezo wa wazazi.
Ninashauri Bodi iangalie utaratibu mpya kuliko huu wa uwezo wa wazazi kwa sababu siku za mbeleni utakuja kuleta matabaka. Ni viongozi wachache tu ambao wanao wanapata mikopo kwa kuzingatia nafasi zao kubwa maofisini. Kaangalie mtoto wa Rais au wa Waziri wa Elimu kama kweli aliwahi kunyimwa mkopo? Bodi yenyewe mna upendeleo na ndiyo mnaoanzisha ubaguzi - ipo siku wanenu au kama sio wanenu hata wajukuuu wenu pia watakuja kubaguliwa! Mtoto wa kakangu amekosa mkopo lakini anamfahamu vema Badru na hata Madam Nyahende - tupo nchi hiii hii na historia hujiandika! Acha wapate watoto wenu wapate mikopo sasa lakini watoto wenu nao watakuja kuwa na watoto! MBOWE SIO GAIDI!