Bodi ya Mikopo (HESLB) yatolea ufafanuzi juu ya Maombi ya Mikopo kwa mwaka wa masomo 2020/2021

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,746
11,877
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imefafanua kuhusu taarifa zinazosambaa mitandaoni kuhusiana na utaratibu wa kupata majibu ya maombi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu katika mwaka wa masomo 2020/2021.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu (Oktoba 19, 2020) na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru amesema HESLB bado haijatoa orodha ya wanafunzi waliopangiwa mkopo na kuwa kwa sasa, kazi ya uchambuzi wa maombi ya mkopo yaliyowasilishwa inaendelea.

Badru amesema taarifa hizo zisizo sahihi zinazosambaa mitandaoni zinawaelekeza waombaji mikopo kupakua mfumo (application) katika simu zao utakaowawezesha kuona orodha ya wanafunzi waliopangiwa mkopo kwa mwaka 2020/2021.

“Taarifa rasmi kuhusu HESLB, zikiwemo zinazohusu wanafunzi wanaopangiwa mkopo zitatolewa kuanzia Novemba 10, 2020 kupitia akaunti walizotumia kuomba mkopo inayofahamika kama SIPA – Student’s Individual Permanent Account,’’ amesema Badru katika taarifa yake.

Badru ameongeza kuwa taarifa kuhusu wanafunzi waliopangiwa mikopo pia zitatolewa kupitia vyombo vya habari, tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz (HESLB | Web)) na mitandao ya kijamii ya HESLB ambayo ni twitter, instagram na facebook kwa jina la ‘HESLB Tanzania’.

Serikali imetenga kiasi cha Tsh Bilioni 464 katika mwaka wa masomo 2020/2021, zinazotarajia kusomesha jumla ya wanafunzi 145,000 wakiwemo wanafunzi 54,000 wa mwaka wa kwanza na wanafunzi 91,000 wanaoendelea na masomo katika taasisi mbalimbali za elimu ya juu nchini.

Na Mwandishi Wetu,
HESLB
Dar Es Salaam
19.10. 2020
 
Du, wanafunzi 54,000 mwaka wa kwanza. Mwaka wa pili, tatu na baadhi mwaka 4 na 5(madaktari) ni jumla ya wanafunzi 91,000 ( wastani wa wanafunzi 22,750 kila mwaka. Kwanini mwaka wa 2 hadi wa tano idadi ni ndogo sana ukilinganisha na mwaka wa kwanza?

Wenye IQ kubwa karibunu mfafanue!!!!!!!!!! Kama hawajatendewa haki hivi!
 
Me nionavyo ni kwamba kuna factor nyingi zinasababisha hii idadi ya wanachuo mwaka wa 2 na kuendelea kuwa ni chache sana ukilinganisha na mwaka wa kwanza(wanaooanza)

1. Kudisco, ungekuwa na idadi ya wanafunzi wanaodisco Mara baada ya kuanza mwaka wa kwanza na semester ya kwanza ni kubwa mno, pia hata mwaka wa pili kupanda juu bado wapo wanaodisco pia

2. Matatizo ya kiafya na vipo pia.

3. Postpones za masomo kwa wanafunzi
4.Absconds
5.Pia kumbuka idadi hyo si kwa wanafunzi wote bali ni idadi ya wanafunzi wanafaika wa mikopo wanaotambuliwa na bodi.. So fahamu kuna wanafunzi wengi wanaojisomesha wenyew kwa gharama zao au mashirika ya umma au binafsi(NGO) hao wote hawajahesabiwa
Zawadi Ngoda
 
Kuna maneno kuntu aluwahi kusema mmoja wa Wagombea wa Nafasi ya Urais katika Uchaguzi Mkuu huu wa 2020 kwamba, kwa upande wake anaona kuwa, Serikali ingewashukuru wazazi waliojifunga mkanda na kusomesha watoto wao katika shule binafsi kwa kuwapatia watoto wao mikopo badala ya hili linalifanyika hivi sasa la kusema, mtoto aliyesomeshwa shule private asipewe mkopo!!! Mimi binafsi nilikubaliana na msimamo wa mgombea yule ingawa siyo chaguo langu katika upigaji kura!

Iwapo wazazi tunaosomesha watoto shule binafsi tusingefanya hivyo, idadi ya Wanafunzi katika shule za Serikali invekuwa kubwa sana na kuzidi uwezo wa Shule zengewe. Hivyo kitendo cha mzazi kujifunga mkanda na kusomesha mtoto katika shule binafsi amesaidia kupunguza pressure kwa Serikali. Pili, ikumbukwe kuwa, mzazi analipia gharama zote za mtoto akiwa private school! gharama ambazo angesoma katika shule za Umma kiasi kama siyo chote kingebebwa na Serikali!! Mzazi huyu kwa upande wangu nasema anastahili kupongezwa na Serikali na kupewa msaada walau wa kusomeshewa mwanae kwa mkopo akifikia Chuo (elimu ya juu).

Mzazi aliyesomesha mtoto wake private kuanzia Chekechea hadi Kidato cha sita, anakuwa amechangia kiasi kikubwa cha Uchumi wa nchi hivyo anastahili kutambuliwa mchango wake na kupewa fursa ya mwanaye kufaidi mgunda ya Uchumi wa nchi kwa kupata mkopo wa kusomesha mwanae elimu ya juu. Tuige kwa Rais George Wear wa Liberia ambaye anafanya elimu ya Juu kuwa bure kuongeza munkari wa vijana katika ngazi za Primary na Sekondari kuongezeka sana na kukuza ufaulu.

Tafakari wahusika kisha chukua hatua, hata kama ni kumshauri aliyezuia wasipate mikopo sawa tu ashauriwe na huenda akaliona kama tunavyoliona sisi.
 
Naunga mkono hoja,,,.,.,.,.,.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom