Bodi ya Mikopo(HESLB) yakanusha taarifa za kuishiwa fedha

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu HELSB imekanusha vikali taarifa iliyonea katika mitandao ya kijamii kuwa imeishiwa fedha za kuwalipa wanafunzi watakaojiunga na vyuo vikuu mwaka huu.

Taarifa ya kuishiwa fedha ilienea katika mitandao ya kijamii ikidaiwa kuwa Taasisi hiyo muhimu ambayo ni mkombozi kwa wanafunzi wa vyuo Vikuu hapa nchini imeishiwa fedha ndio maana fedha za mikopo zinachelewa kuwafikia.

Kwa mujibu wa Kurugenzi ya Mawasiliano HESLB imebainisha kuwa taarifa hizo ni za upotoshaji na zina lengo ya kuleta taharuki miongoni mwa wanafunzi suala ambalo halina ukweli wowote.

“Si kweli kwamba Bodi haina fedha, ila ni kweli kwamba kumekuwa na ucheleweshaji wa kufikisha fedha za wanafunzi vyuoni kutokana na zoezi la kuhakiki wanafunzi wanaonufaika na mikopo linaloendelea vyuoni hivi sasa.”Imesema taarifa ya Bodi hiyo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa maandalizi ya malipo hayo yameshafanyika na ‘pay sheets’ zimeshapelekwa vyuoni tayari kwa wanafunzi wanaonufaika na mikopo kusaini.

Bodi inatarajia wakati wowote wiki ijayo baada ya zoezi la uhakiki kukamilika; itapeleka fedha hizo vyuoni.
 
Huyo mkurugenzi ni jipu, hivi kuna uhakiki gani unafanyika vyuoni mbona wanafunzi wanakataa hawajahakikiwa na mbona vyuo vingine vilipata pesa mapema huo uhakiki kwa baadhi ya vyuo au?
 
Kwa udsm kipindi wanapelekewa pesa walihakikiwa mbona hawakuwai hakikiwa na vyuo kibao tuu wamepewa pesa bila kuhakikiwa
 
Mbona nilishema tangu siku ile kuwa watakuja kukanusha tu, huu utamaduni mpya sijui unatoka wapi
 
HUWEZI KANUSHA UKWELI NA MALA ZOTE UKWELI HUJITENGA NA UONGO TAARIFA ZENU ZOTE KUTOKA KWA WAKURUGENZI WAANDAMIZI KI KUWA PESA HAKUNA IWEJE LEO MTU ANAIBUKA NA KUDAI KUWA TAARIFA HIZO NI UONGO? What does it mean by truth?

Ogopa KUDANGANYA MTU ambae TAYARI anataarifa kamili juu ya UHAKIKI. Hakuna dhambi kubwa kama dhambi ya kumnyonga mnyonge kwa kigezo eti hajahakikiwa. Na kimusingi kama kweli kuna swala la kumchulia hatua mkurugenzi huyo alietoa taarifa ambayo ni ya kiukandamizaji kwa Watoto wa walipa kodi , Basi aburuzwe mahakamani. Taifa gani hili ambalo hata maafisa wake wa serikali hawaogopi dhambi hi ya udanganyifu. Kimsingi na kwa mujibu wa JPM jipu ni mutu anae enda kinyume na utaratibu Mbona majipu kama hayo kwa upande wa maafisa hawashughulikiwi. Kumbukeni wasomi wote wanajifunza about Universal education na hivyo mnavyochelewesha kuwalipa pesa zao za kujikimu mtegemee hivihivo kulipwa kwa kuchelewa sana na wakati mwingine kupokea dhuruma kabisa maana mpango wenu ni mbaya sana ambao pia ni wa ukurupukaji. Tujitahidi kuweka balance maana human being are in dependence>>>. we depend from one another for our survival..

Nidhahiri kwa mh. Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania anaendelea kuifanya kazi yake ya kuipigania taifa lake na la watanzania kwa ujumla ili kuhakikisha mambo yote yanakuwa sawa na watu wanakuwa na furaha.
Kiufupi hali ya furaha kwa wanafunzi wa chuo kikuu CHA MTAKATIFU MIHAYO TABORA (amucta) imepungua kama kuporomoka kwa poromoko la hali kiuchumi na dollar kwa nchi YA Uingreza (after Britain’s momentous vote on June 23rd to leave the EU, many in Brussels and London want to know how it will be implemented. Since the Lisbon treaty came into force in 2009 there has been only one legal mechanism: the country that wants to leave must invoke Article 50, which sets out how it happens.)
Wanafunzi wakaa njiapanda kimawazo juu ya mstakabali wa maisha yao sambamba na ufaulu wa masomo yao. Hii ni baada ya pesa yao ya kujikimu (BOOM) toka serikalini Kuchelewa sana mno na kusababisha wengi wao kujiingiza katika shughuli za utafutaji hasa kwa kufanya vibarua na shughuli ndogondogo ili mkono kwenda kinywani katika kipindi hiki kigumu.

Swali serikali kupitia bodi ya mikopo imesahau kama kuna wanafunzi chuo kikuu cha Tabora? Think, get answers;...........http.afrapaul.com


HABARI RASMI TOKA MKOANI TABORA.......................
 
Pale nit mi miezi sasa wanafunzia hawajapewa hela zao za kujikimu!!
 
Back
Top Bottom