Bodi ya Mikopo(HESLB) waachia majina ya wadaiwa sugu kuanzia mwaka 1994 hadi 2014

Wakuu,
Nimeikuta sehemu hii:

UTARATIBU KWA WAAJIRI NA WAAJIRIWA KATIKA UREJESHAJI WA MIKOPO YA ELIMU YA JUU
Swali: Mwajiri anapaswa kufanya nini baada ya kuajiri wahitimu wapya?
· Kwa mujibu wa sheria Na. 9 ya mwaka 2004 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (kama ilivyorekebishwa), mwajiri anapaswa aijulishe Bodi kwa maandishi kuhusu waajiriwa wapya ambao ni wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu ndani ya siku ishirini na nane (28) tangu tarehe ambayo wahitimu hao wameajiriwa.

Swali: Nini kitafuata baada ya kuwasilisha HESLB orodha ya wahitimu walioajiriwa?
· Baada ya kupokea taarifa kutoka kwa waajiri, Bodi itabainisha wafanyakazi walionufaika na mikopo ya elimu ya juu.

Swali: Mwajiri ana wajibu gani baada ya kupokea orodha ya wadaiwa wa mikopo kutoka HESLB?
· Anapaswa kuhakikisha kuwa makato ya kila mwezi kutoka kwenye mishahara ya wadaiwa wa mikopo yanawasilishwa Bodi kama ilivyoelekezwa ndani ya siku kumi na tano (15) baada ya kila mwisho wa mwezi.

Swali: Nini kitatokea endapo mwajiri ataacha kukata mshahara wa mfanyakazi baada ya kuelezwa na HESLB kwamba mfanyakazi huyo ni mdaiwa wa mkopo?
· Iwapo mwajiri atashindwa kukata ama kukata mshahara wa mdaiwa wa mkopo na kushindwa kuwasilisha makato hayo Bodi ndani ya muda uliopangwa, atatozwa asilimia kumi (10%) ya kiasi cha deni lililopaswa kulipwa kwa kila mwezi ambao makato hayatawasilishwa.

Swali: Ni lini mnufaika wa mkopo anapaswa kuanza kurejesha mkopo wake?
· Mkopo huanza kulipwa unapomalizika mwaka mmoja wa neema baada ya kuhitimu masomo ya elimu ya juu au baada ya kusitisha masomo kwa sababu yoyote ile.

Swali: Je, ajira ya mdaiwa wa mkopo ni jambo linalozingaliwa katika urejeshaji wa mikopo?
· Wadaiwa wanapaswa waanze kurejesha mikopo muda unapofika bila kujali iwapo wameajiriwa ama la.

Swali: Ni asilimia ngapi hutozwa kama tozo la kutunza Thamani ya fedha kwa kila mdaiwa wa mkopo?
  • Madeni yote ya mikopo hutozwa asilimia sita (6%) kama tozo la kutunza Thamani ya Fedha (VRF) kwa mwaka.

Swali: Kwa nini HESLB inatoza tozo la kutunza Thamani ya Fedha (VRF) kwenye mikopo inayorejeshwa?
· Mikopo inatozwa tozo la kutunza Thamani ya Fedha ili kutunza thamani ya fedha dhidi ya mfumuko wa bei ambao unapaswa kuwa na thamani sawa wakati mkopo utakapotolewa kwa wanafunzi wengine wenye uhitaji katika siku zijazo.

Swali: Ni hatua zipi za kisheria zitachukuliwa kwa wadaiwa ambao hawatarejesha mikopo yao?
· Mdaiwa yeyote ambaye, bila sababu za msingi atashindwa kulipa mkopo atachukuliwa hatua za kisheria. Aidha, mambo yafuatayo yatafanyika:
(a) Atapata adhabu ya kulipa asilimia kumi (10%) ya mkopo wake wote.
(b) Taarifa zake zitawasilishwa kwenye taasisi zinazosimamia taarifa za wakopaji wanaotaka kukopa kutoka taasisi za fedha zinazotoa mikopo, ambapo watazuiliwa kukopa kutoka kwenye Taasisi za Fedha.
(c) Atazuiliwa kupata ufadhili wa Serikali kwa ajili ya masomo ya Uzamili au Uzamivu katika chuo chochote cha Elimu ya Juu ndani na nje ya nchi.
(d) Maelezo yao yatawasilishwa Wizara ya Mambo ya Ndani, Idara yaUhamiaji ambapo hawatapewa kibali kwa ajili ya kusafiri nje ya nchi

Swali: Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali(CAG) na kampuni zingine binafsi za ukaguzi wana wajibu gani katika urejeshaji wa mikopo?
· Jukumu la Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) na makampuni mengine binafsi ya Ukaguzi ni kuhakikisha waajiri wanatekeleza kwa kuwasilisha wahitimu Bodi ya mikopo na makato ya fedha kutoka kwa wadaiwa yanawasilishwa kama ilivyoelekezwa.

Swali: Mnufaika wa mkopo anapaswa kufanya nini ili kulipa deni lake?
· Mara baada ya kuhitimu masomo au kusitisha masomo yake kwa sababu yoyote ile, mnufaika anapaswa aitaarifu Bodi kwa maandishi mahali alipo na hali ya ajira yake ili kukubalina na Bodi juu ya ulipaji wa mkopo wake.

Swali: Makato huwasilishwaje HESLB?
· Kwa wanufaika waajiriwa, hukatwa asilimia nane (8%) ya mshahara wa kila mwezi.

Mnufaika anaweza kulipa kiwango cha chini cha shilingi 100,000/= kila mwezi kupitia Akaunti zifuatazo:
i. Benki ya Posta Tanzania CCA0240000032
ii. NMB Bank Akaunti 2011100205
iii. Benki ya CRDB Akaunti 01J1028467503

Kama unaswali, tuma email kwenda: repyament@heslb.go.tz ukitaja majina yako kamili, chuo, mwaka na kozi uliyosoma na namba yako ya mtihani wa Form IV. Wanakujibu fasta.
Kazi yote hyo ya nn? Mi cmtafti mtu wao watanitafta
 
Hivi njia rahisi ya kuangalia jina ni ipi?
1.Vip waliokufa?
2.Kuna watu wamejaza fomu kwa waajili but hawakatwi.
3.Inakuwaje 2013/2014 ni Sugu?
4.Na inakuwaje wengine hawakunufaika na wanakatwa nao waishtaki serikali na kulipwa?
Maajabu ya Tanzania.
Hawa jamaa hawako sereouse kabisa, sababu majina matatu kwa tanzania hii unaweza ukakuta hata watu 100 wanafanana jina la kwanza, ubini, na jina la ukoo, sasa kusema xxx wa mwaka xxx bila kuweka maelezo ya kujitosheleza kama chuo alicho kuwa akisoma, kozi aliyofanya, na mengine mfano wa hayo inakuwa ni sawa na kutoa majina hayo kuzima soo. Halafu yamechanganywa changanywa, si ange yapaste kwenye excel ayapange aaphabetical zoezi liwe rahisi.
Hapa kazi tuu.
 
Hiyo 6% inalinda thamani ya pesa kwani mkopaji hiyo pesa alienda kuizalisha au kuifanyia biashara?
Wana uchumi tusaidieni hapa
 
Kulipa mkopo ni nia ya dhati ya mdaiwa binafsi kulipa wala si kumlaumu muajiri kwani anaweza kuwa hajui hilo, ni wajibu wa mdaiwa wa mkopo kumwambia mwajiri kuwa nadaiwa....Tulipe ili wengine wasome jamani....
 
Dada mie ni ka degree kaukweli na sidaiwi na mtu yeyote.

Mliokopa fanyeni mlipe visingizio sio sababu. Raha ya deni ni kulilipa na sivinginevyo.
Kwanza mimi sio dada.
Kama HESLB hawakuhusu just kaa kimya kushabikia jambo lisilokuhusu wenzetu wa jinsia ya pili wanaitaga umbea.
Hao watu wa board hawana umakini na kazi zao
1. Wanadai watu ambao hawakuwahi kukopa wala kusoma degree

2. Hawajaweka details za wadaiwa kikamilifu
3. Wanataja watu kua wadaiwa sugu ilihali washalipa madeni yao
4. Wanafanya kazi under political pressure kwa sababu hata matamko wanayotoa hayatekelezeki mfn: eti watafuatilia wadaiwa after 30days mbona wameshindwa kufatilia tangu 1995? Au hapakua na serikali?
kituko kingine eti mdaiwa atafikishwa mahakamani na atalipa gharama za kesi wana uhakika gani kwamba watashinda kesi je wakishindwa?

Wanachaji 6% kulinda thamani ya pesa kwani kuna mtu kachukua ile pesa kufanyia business?
Na kwenye mkataba hapakua na hiyo 6% kama tozo.

Kwenye mkataba hapakua na sharti la muajiri kuijulisha board endapo muajiri atamuajiri mnufaika wa mkopo
Yaani ni full vituko kwenye Tanzania ya viwanda
 
maajabu haya utayaona Tanzania pekee...
mtu alishindwa kulipa ada ya chuo, akamaliza, hajaajiliwa, kamaliza hajakaa hata miaka miwili eti ni mdaiwa sugu!!
kamaliza 2013/2014 anakuaje sugu, huo usugu maana yake ni nini sasa??
haa haa kwel noma sana...
Weeeeee na tusha ambiwa ajira bana hamna kwanza uhakiki mbona balaaa aise
 
Serikali isomeshe watu wake sio kuwadai pesa.pesa kama hawana waende kwenye madini na gesi sio kukimbizana na vijimikopo
 
Bodi ya mikopo hii tabia ya kurupuka kwa taasisi kubwa kama hii ni hatari sana nilikua private na mpaka leo nina receipts zote nilizoliipia ada na accomodation..lkn jina langu liko kwenye orodha kama mdaiwa sugu they have to apologize kwa public if at all kama hawana data sahihi wakawaombe wadai sugu watawapatia,hawa loan board wana kichaa They want to solve political pressure siasa za maji taka zitawaua bongo Duplicates kibao za majina
Bila shaka mpunga wako walikuwa wanaukinga tu, yaani mkopo hewa.
 
Mkuuu
Serikali haijatoa ajira tangu mwaka Jana, na wahitimu tangu mwaka juzi hadi mwaka huu wapo kwenye hiyo list!
Sasa watalipaje na hawajaajiriwa? Hizo pesa za kulipa watoe wapi?
Au ndio Mzee Magu kaamua kukamua wananchi wake (kuanzia waathirika wa bukoba hadi jobless graduates ) ili aongeze ndege nyingine?

Mkuu embu tuache bla bla.....listi inaonyesha wadaiwa sugu kuanzia miaka ya nyuma mpaka 2014...15-16 hachana nao..watu walipe madeni ili wengine wapate mikopo.
 
Back
Top Bottom