Bodi ya Mikopo(HESLB) waachia majina ya wadaiwa sugu kuanzia mwaka 1994 hadi 2014

Ivi miaka yote hiyo Board ya mikopo walikuwa wapi kuwatafuta wadaiwa? tatizo sio wadeni sugu tatizo ni board.Kufanya kazi kwa mazoea
Presha ya Mzee wa kaya inawanyima usingizi....kuna yule bwana aliekataa uded unadhani alikuwa mjinga!?
 
Kuweni serious japo kidogo, badala ya kulipa deni unarukaruka tu, wahimize na wenzio.
Alaf kuna majina yamerudiwa zaidi ya Mara 3, hii ina maana ya idadi wadaiwa ni ndogo tofauti na iliyotolewa na bodi
 
Kuna rafiki wa kike nimeona jina lake kwenye list nikamtonya akanijibu hajawahi kuomba mkopo kwani alilipiwa na baba yake asiependa kuwatwisha wanawe madeni, alipo ulizia vizuri bodi ya mikopo anadaiwa 11 milioni. Wajanja wamekula pesa za umma sasa wanabambikia kila jina wanalokutana nalo.
 
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inatangaza orodha ya majina ya Wadaiwa Sugu ambao wamehitimu katika Vyuo mbalimbali vya Elimu ya Juu kuanzia mwaka wa masomo 1994/1995.

Wasugu hao wanapewa siku 30 kulipa madeni yao ndani ya muda huo kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa na wahusika kulazimika kulipia gharama za kuwasaka na kuendesha kesi.


Chanzo: Tovuti ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu..

Wakuu,
Nimeikuta sehemu hii:

UTARATIBU KWA WAAJIRI NA WAAJIRIWA KATIKA UREJESHAJI WA MIKOPO YA ELIMU YA JUU
Swali: Mwajiri anapaswa kufanya nini baada ya kuajiri wahitimu wapya?
· Kwa mujibu wa sheria Na. 9 ya mwaka 2004 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (kama ilivyorekebishwa), mwajiri anapaswa aijulishe Bodi kwa maandishi kuhusu waajiriwa wapya ambao ni wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu ndani ya siku ishirini na nane (28) tangu tarehe ambayo wahitimu hao wameajiriwa.

Swali: Nini kitafuata baada ya kuwasilisha HESLB orodha ya wahitimu walioajiriwa?
· Baada ya kupokea taarifa kutoka kwa waajiri, Bodi itabainisha wafanyakazi walionufaika na mikopo ya elimu ya juu.

Swali: Mwajiri ana wajibu gani baada ya kupokea orodha ya wadaiwa wa mikopo kutoka HESLB?
· Anapaswa kuhakikisha kuwa makato ya kila mwezi kutoka kwenye mishahara ya wadaiwa wa mikopo yanawasilishwa Bodi kama ilivyoelekezwa ndani ya siku kumi na tano (15) baada ya kila mwisho wa mwezi.

Swali: Nini kitatokea endapo mwajiri ataacha kukata mshahara wa mfanyakazi baada ya kuelezwa na HESLB kwamba mfanyakazi huyo ni mdaiwa wa mkopo?
· Iwapo mwajiri atashindwa kukata ama kukata mshahara wa mdaiwa wa mkopo na kushindwa kuwasilisha makato hayo Bodi ndani ya muda uliopangwa, atatozwa asilimia kumi (10%) ya kiasi cha deni lililopaswa kulipwa kwa kila mwezi ambao makato hayatawasilishwa.

Swali: Ni lini mnufaika wa mkopo anapaswa kuanza kurejesha mkopo wake?
· Mkopo huanza kulipwa unapomalizika mwaka mmoja wa neema baada ya kuhitimu masomo ya elimu ya juu au baada ya kusitisha masomo kwa sababu yoyote ile.

Swali: Je, ajira ya mdaiwa wa mkopo ni jambo linalozingaliwa katika urejeshaji wa mikopo?
· Wadaiwa wanapaswa waanze kurejesha mikopo muda unapofika bila kujali iwapo wameajiriwa ama la.

Swali: Ni asilimia ngapi hutozwa kama tozo la kutunza Thamani ya fedha kwa kila mdaiwa wa mkopo?
  • Madeni yote ya mikopo hutozwa asilimia sita (6%) kama tozo la kutunza Thamani ya Fedha (VRF) kwa mwaka.

Swali: Kwa nini HESLB inatoza tozo la kutunza Thamani ya Fedha (VRF) kwenye mikopo inayorejeshwa?
· Mikopo inatozwa tozo la kutunza Thamani ya Fedha ili kutunza thamani ya fedha dhidi ya mfumuko wa bei ambao unapaswa kuwa na thamani sawa wakati mkopo utakapotolewa kwa wanafunzi wengine wenye uhitaji katika siku zijazo.

Swali: Ni hatua zipi za kisheria zitachukuliwa kwa wadaiwa ambao hawatarejesha mikopo yao?
· Mdaiwa yeyote ambaye, bila sababu za msingi atashindwa kulipa mkopo atachukuliwa hatua za kisheria. Aidha, mambo yafuatayo yatafanyika:
(a) Atapata adhabu ya kulipa asilimia kumi (10%) ya mkopo wake wote.
(b) Taarifa zake zitawasilishwa kwenye taasisi zinazosimamia taarifa za wakopaji wanaotaka kukopa kutoka taasisi za fedha zinazotoa mikopo, ambapo watazuiliwa kukopa kutoka kwenye Taasisi za Fedha.
(c) Atazuiliwa kupata ufadhili wa Serikali kwa ajili ya masomo ya Uzamili au Uzamivu katika chuo chochote cha Elimu ya Juu ndani na nje ya nchi.
(d) Maelezo yao yatawasilishwa Wizara ya Mambo ya Ndani, Idara yaUhamiaji ambapo hawatapewa kibali kwa ajili ya kusafiri nje ya nchi

Swali: Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali(CAG) na kampuni zingine binafsi za ukaguzi wana wajibu gani katika urejeshaji wa mikopo?
· Jukumu la Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) na makampuni mengine binafsi ya Ukaguzi ni kuhakikisha waajiri wanatekeleza kwa kuwasilisha wahitimu Bodi ya mikopo na makato ya fedha kutoka kwa wadaiwa yanawasilishwa kama ilivyoelekezwa.

Swali: Mnufaika wa mkopo anapaswa kufanya nini ili kulipa deni lake?
· Mara baada ya kuhitimu masomo au kusitisha masomo yake kwa sababu yoyote ile, mnufaika anapaswa aitaarifu Bodi kwa maandishi mahali alipo na hali ya ajira yake ili kukubalina na Bodi juu ya ulipaji wa mkopo wake.

Swali: Makato huwasilishwaje HESLB?
· Kwa wanufaika waajiriwa, hukatwa asilimia nane (8%) ya mshahara wa kila mwezi.

Mnufaika anaweza kulipa kiwango cha chini cha shilingi 100,000/= kila mwezi kupitia Akaunti zifuatazo:
i. Benki ya Posta Tanzania CCA0240000032
ii. NMB Bank Akaunti 2011100205
iii. Benki ya CRDB Akaunti 01J1028467503

Kama unaswali, tuma email kwenda: repyament@heslb.go.tz ukitaja majina yako kamili, chuo, mwaka na kozi uliyosoma na namba yako ya mtihani wa Form IV. Wanakujibu fasta.
 
Kwani mdaiwa sugu ni yupi? Nami kwenye list hiyo nimo ya wadaiwa sugu. Nilianza kukatwa marejosho na bodi mwaka mmoja baada ya kuhitimu chuo. sasa hivi nakaribia kumaliza mkopo wao afu naanikwa hadharani kama mdaiwa sugu.
Hii kaman sio kudhalilishana ni nini? Ninapanga kuwaburuza hawa jamaa mahakamani kwa kunivunjia heshima na hadhi yangu mbele ya jamii. Kama wapo wengine kama mimi tafadhali ni pm tuchukue hatua stahiki. Nimepitia haya majina kwa umakini sana, nimegundua kuwa wengi wa majina haya ni wale ambao tayari wameanza kulipa na Bodi inawakata.
Kuna watu wangu kadhaa wa karibu ninawafahamu wamemaliza vyuo miaka mingi kadhaa hawajawahi kulipa wala kukatwa japo walikopeshwa mikopo. Na bado kwenye orodha hii hawakuorodheshwa kabisa.

Kama kweli orodha hiii imetoka HESLB, basi nashawishika kuamini kwamba Bodi hii haina takwimu sahihi za nani anadaiwa na nani hadaiwi na nani kamaliza kulipa na nani anaendelea kulipa deni.
Kama ndivo,watapata hasara badala ya faida. NI hatari saana hii!
Kimsingi Bodi ya Mikopo (HESLB) haina takwimu za kutosha wala takwimu sahihi mathalani kwenye taasisi yetu tulitumiwa barua ya kuanza kukatwa mwaka 2013 ila cha ajabu kulikuwa na wenzetu wapatao 3 ambao hawakuwahi kukopa mpaka leo wanatumiwa barua za eti walipe mkopo. Hapo ndio utajua kuwa Bodi ya mikopo vilaza
 
Kimsingi Bodi ya Mikopo (HESLB) haina takwimu za kutosha wala takwimu sahihi mathalani kwenye taasisi yetu tulitumiwa barua ya kuanza kukatwa mwaka 2013 ila cha ajabu kulikuwa na wenzetu wapatao 3 ambao hawakuwahi kukopa mpaka leo wanatumiwa barua za eti walipe mkopo. Hapo ndio utajua kuwa Bodi ya mikopo ******
Hata leo ukiwauliza fulani anadaiwa kiasi gani, Bodi hawawezi kupatia jibu. Hili filamu linaelekea pazuri sana. Waliokula ya mbuzi safari hii lazima waote mapembe!
 
heslb...wangewaongeza nguvu ili wadaiwa sugu watafutwe, wengi sana wana ajira lakini bodi haifatilii...Wajue kua waTanzania hawana tabia ya kuogopa mkopo..unaweza mfata hata mpka chumbani lakini kama hana hana tu, kujisalimisha ni ngumu.
 
Unasemaje gharama za kesi zitalipwa na mdaiwa wakati kesi haijaamuliwa? Gharama za kesi hulipwa na anayeshindwa.
Eti bana kwanza Hiyo haipo kwenye mkataba..wapige faini yao watulie, hatukusaini kulipia gharama za kesi ..
 
Tukutane mwambaniiii... Wao si wavuvi banaaa.... Watoe tena majina na bei wanazodai bila ya hapo ni kelele tuu hizoo
 
Wanaacha kudai ela kama escro...meremeta ela za polisi kodi za migodi wanakuja kudai wanafuzi?
 
Nawezaje kuangalia kwenye ile list ya majina ambayo hayajawekwa alphabetically.
 
Nawezaje kuangalia kwenye ile list ya majina ambayo hayajawekwa alphabetically.
Download kwenye format ya PDF kisha nenda kwenye kitufe/kialama cha search hapo utaandika jina unalolitaka. Watakuletea yanayofanana utaenda next mpaka ulikute. Kama unatumia kompyuta bonyeza Ctrl+F kisha weka jina unalotaka.
Nadhani ntakua nimekusaidia kiasi.
 
Download kwenye format ya PDF kisha nenda kwenye kitufe/kialama cha search hapo utaandika jina unalolitaka. Watakuletea yanayofanana utaenda next mpaka ulikute. Kama unatumia kompyuta bonyeza Ctrl+F kisha weka jina unalotaka.
Nadhani ntakua nimekusaidia kiasi.
Asante mkuu nitafanya hivyo.
 
Back
Top Bottom