Bodi ya mikopo (heslb) na makato ya asilimia nane (8) ya mishahara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bodi ya mikopo (heslb) na makato ya asilimia nane (8) ya mishahara

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by AmaniGK, Aug 16, 2012.

 1. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2012
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Hapo Novemba mwaka jana Higher Education Students Loans Board Act ilirekebishwa katika Section 20 na ikawa inasomeka hivi "Deduct 8% of the basic salary for employee who is a loan beneficiary and remit the same to the Board in the manner as the Board shall describe".

  Natumaini marekebisho haya yalifanywa huku wawakilishi wetu bungeni wakiiona na kuiunga mkono. Mabadiliko haya ambayo yamechukua nafasi ya yale ya mwanzoni ambako wakopaji walitakiwa kurudisha deni lao kwa kipindi cha miaka kumi, yameongeza kiwango cha ukusanyaji kwa hali ya juu.

  Kwa maoni yangu: Makato haya ni makubwa ikizingatiwa viwango vya mshahara ambavyo wafanyakazi wanavyo, Pia tukizingatia karibia asilimia 30 ya mshahara huo huo yanapelekwa kwenye kodi, Asilimia 10 kuchangia kwenye mifuko ya jamii. Kwa maana hii sasa kwa wale waliokopa karibu asilimia 50 ya mapato yao ya mwezi yanaangukia kwenye makato haya ya lazima.

  Nadhani ipo haja ya hili kupigiwa tena kelele kama lile la Fao la kujitoa linavyopigiwa kelele.Makusanyo haya japo yatarudisha madeni kwa uharaka, lakini hayakuangalia kipato cha mfanyakazi wa kawaida.Kuna haja ya lazima kabisa kwa hili kupitiwa tena kwa undani zaidi.
   
 2. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  8% heslb + 10% nssf+paye +..............??????!!!!!!!
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Aug 16, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Cha msingi hapo ni kupunguza Paye tu,maana ni kubwa mno maana mie naona kama 32% hivi....wapunguze Paye iwe hata 10% na sie tupumue bwana! Watafute njia nyingine ya kuongeza mapato,kodi nakatwa nikiagiza gari nakatwa sasa mbona nalimwa tu kodi? Watupe TIN no ya ulipaji ili kuwe na max ya ulipaji kwa mwaka!!
   
 4. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Serikali iwe creattive kidogo, huwezi kuendesha nchi kwa kutegemea kukusanya pesa kutoka kwenye ushuru wa GX 110 wakati nchi hii ina resources kibao. Gas, maji, mabonde yenye rutba nk.
   
 5. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,472
  Likes Received: 463
  Trophy Points: 180

  Wao walisomeshwa bure sisi wanatusomesha kwa mkopo tena wenyewe kuupata mpaka kuandamana.
   
Loading...