Bodi ya mikopo elimu ya juu yatoa takwimu ya ulipwaji wa madeni ya mkopo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Kuanzia July 2015 hadi June 2016 Bodi ya Mikopo imetoa Tsh. Trilioni 2.5 kwa wanafunzi 330,801, idadi ya wanafunzi waliokopeshwa ni 379,179.

Asilimia 65 ya kiwango cha mikopo iliyokusanywa kimetoka kwenye sekta ya umma na asilimia 35 kwenye sekta binafsi' - Bodi ya Mikopo

Mwitiko mkubwa umetoka kwa watu ambao wamejiajiri wenyewe ambapo watu takribani 28,823 elfu walijitokeza kulipa madeni yao ambao wamerejesha kiasi cha bilioni 13.7 ndani ya mwaka mmoja tuu wa makusanyo wa fedha hizo za mkopo.

Zaidi ya Tsh Bil 13.7 zimerejeshwa kutoka kwa walionufaika na mikopo ya elimu ya juu, waliojiajiri wamejitokeza kwa hiyari kurejesha mikopo.

Chanzo: millad twitter

==========================================================

Zoezi la utafutaji, ufuatiliaji na ukaguzi wa wadaiwa sugu na ambao wamenufaika na mikopo ya elimu ya juu mahala pa kazi iliyoendeshwa na Bodi ya Mikopo ya Mikopo ya Elimu ya Juu katika kipindi cha mwaka mmoja, limefanikiwa kwa asilimia 46 na kupelekea makusanyo ya mikopo hiyo kuvuka lengo lililokusudiwa.

Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, kuhusiana na hali ya makusanyo ya mikopo kwa wanufaika wa elimu ya juu, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Bwana Abdulrazak Badru amesema walilenga kukusanya Shilingi Bilioni 76 lakini wamekusanya Shilingi Bilioni 116 ikiwa ni kiwango cha marejesho cha asilimia 46.

Bwana Badru amesema, hataacha kutumia mbinu ya ufuatiliaji mahala pa kazi huku akiwakumbusha wale ambao wanashindwa kurejesha mikopo kwa hiari sheria itafuata mkondo dhidi yao kwani fedha hizo hutumika kwa wanafunzi wa awamu mpya ya masomo.

Aidha, Bwana Badru ametoa onyo kali kwa waajiri ambao wameshindwa kuwasilisha majina ya waajiriwa wao ndani ya siku 28 kwa bodi hiyo, kuchelewesha makato baada ya kuwakata waajiriwa ama kuficha taarifa kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.


Chanzo: EATV
 
hii serikali naskia tuu mara mapato yameongezeka, mara faini za barabarani zikuwa ma billions, mara mtu karudisha pesa za escrow, na sasa watu wamerejesha mikopo,,,,sioni utofauti zaidi maisha ya mtanzania kuwa magumu ,,sijaelewa mpaka sasa izo pesa wanazotangaza nani anapewa na zinafanya nini,,bulshit
 
Back
Top Bottom