Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu kilema cha maisha kwa vijana wa Tanzania

muzi

JF-Expert Member
Jun 17, 2016
1,038
1,448
FAHAMU KIDOGO KUHUSU LOAN BOARD NDUGU!

Bodi ya Mikopo imewanufaisha watanzania wengi sana ikiwa ni pamoja na kuwajengea watanzania misingi ya kielimu kwa ajili ya future katika maisha yao. Aidha, Asilimia 80 ya wanufaika wa mikopo ya bodi ni wale kina KAYUMBA, yaani watoto wa maskini.

Sheria ya mwaka 2016 ya bodi ya mikopo iliyofanyiwa marekebisho ni sheria ANGAMIZI kwa watoto maskini.

Sheria imeweka wazi (Watanzania wengi hawana tabia ya kujisomea) kuwa marejesho ya mkopo yatakuwa ni kwa 15% KWA KILA MWEZI, na deni hilo litakuwa linaongezeka kila mwaka wa fedha kwa asilimia 6% ya deni halisi la mwanzo.

Kwa mfano:

Daktari ambaye amesomeshwa na bodi, asilimia kubwa deni lao huwa kati ya mil 25 mpaka 30. Basic salary yake ni 1.5 Mil.

Makato ya mshahara wake ni kama ifuatavyo:

HESLB 225,000 TSH
PAYE 295,090 TSH
NHIF 42,420 TSH
Pension 80,000

Total deduction 642,510 TSH
Take home yake ni 857,590 TSH — ana watoto na anasomesha!

Kwa sheria ya bodi ya mikopo, huyu bwana kwa mwaka ataweza kulipa 2.7Mil (225,000x12)

Hivyo katika deni lake la 30Mil, atakuwa amepunguza deni lake hadi 27,300,000 TSH ikifika mwisho wa mwaka wa fedha.

Mtu huyu atapaswa kuanza mwaka wa fedha mpya akiwa na deni la 27,300,000 TSH.

Lakini sheria ya bodi inasema hapana, unatakiwa kuongezewa 6% ya 30 mil ambayo ni 1.8 Mil

Hivyo deni analopaswa kuanza nalo ni 27,300,000 + 1.8 Mil sawa na 29,100,000 TSH.

Kwa mwaka unaofuata tena, atafanikiwa kuipunguza hiyo 29,100,000 Mil hadi 26,400,000 Mil na ndiyo ni kianzio cha deni lake kwa mwaka mpya uliofuata.

Sheria ya bodi itasema hapana, hii 26,400,000 lazima iwekwe 6% ya 30Mil ambayo ni 1.8

Hivyo 26,400,000 + 1.8 Mil.
Deni jipya kwa mwaka mpya uliofuata itakuwa ni 28,200,000Mil badala ya 26,400,000 and the list goes on
.

Yaani utakuwa unakwenda mbele na kurudi nyuma mpaka unastaafu.

Sheria ya mwaka 2016, inazidi kusema kuwa, ikiwa muhusika mpaka anastaafu, hajafanikiwa kumaliza deni lake, basi pension yake itafidiwa.

Yaani, ikiwa una pension ya 15 Mil, na deni lako lilibaki 20 Mil , Bodi itakula zote 15 Mil na itakudai 5 Mil na hiyo 5 mil itazidi kuongezeka kadiri miaka inavyokwenda mbele, ni hatari sana na mbaya zaidi watumishi wengi hawajui hii sheria.

Ikitokea pension yako imeliwa yote na bodi, maana yake unazeeka ukiwa huna kitu.

I just can't figure it out, ni sheria kandamizi dhidi ya mtoto maskini iliyopitishwa na wabunge wetu tukufu.

Ni kwamba mtoto wa maskini hatoweza kumaliza hili deni, ni deni la maisha hasa waliosoma kozi za sayansi kama udaktari, Nesi, famasi, na injinia na wale waliosoma nje ya nchi. Hawa wote madeni yao si chini ya 25 Mil or so. It is a detrimental to these poor people, and Unfair.

MAPENDEKEZO:

1. Serikali ipitie upya hii sheria, na ifutilie mbali hiyo incremental ya 6% kwa kila mwaka, it is not even practical, watu wengi wanakufa na hayo madeni tena bado yakiwa makubwa mno.

2. Irudishwe asilimia 8% au 10% badala ya 15% ya makato ya bodi, kwa sababu watumishi wa umma ndiyo wanufaika wa hii mikopo, na wengi wanaangamia hali zao malikiti sokoni.

3. Bodi ya Mikopo itoe elimu redioni juu ya utaratibu wa urejeshwaji wa haya makato. Watanzania wengi hawajui kitu kuhusu mambo ya sheria.

4. Sheria ya kuchukua pension ya watumishi walioitumikia serikali hadi kustaafu iondolewe kwa sababu ni mateso makubwa yatakuwa kwa hawa watu na hii ni jamii yetu inayoitumikia serikali ya Jamhuri miaka nenda rudi.

Watumishi wa umma wengi wanastaafu wakiwa maskini na fukara, uwachukulie tena hizo pesa za pension, kweli? Doh, tutapata laana katika nchi.

USHAURI:

1. Kwa wazazi ambao wanajiweza, achaneni na mambo ya kuwasukumizia watoto wenu kwenye mikopo mpaka muelewe vyema sheria ya marekebisho. Hiki ni kilema cha maisha kwa wale ambao deni lao ni above 20Mil.

2. Pia wahusika hakikisheni mnaipitia hii sheria na muelewe marejesho yake. You need to take precaution. Kama huelewi mtafute Mwanasheria akueleweshe, ni hatari sana. Fuatilieni haya mambo.

Pongezi kwa Mchambuzi!
 
asante kwa taalifa..
 
Sasa hata ikipunguzwa kwa 8% au 10% wadaiwa hawatokufa na madeni makubwa? au pension zao hazitakatwa wakistaafu?
Mkuu hujui excitement tunayoipata deni likikaribia kuisha. Mi naona iendelee hiyo ili tumalizane na hayo madeni.
 
Yaan huo ni wizi wa waz waz ,ukipiga mahesabu hapo ni sawa unalipa laki Tisa kwa mwaka kupunguza deni

Hii sheria haifai na kandamiza sanaaa pia wakati watu wanapata mkopo haikuwepo

Jaman jaman tuungane kukemea hilii kila sikuu
 
Sasa hata ikipunguzwa kwa 8% au 10% wadaiwa hawatokufa na madeni makubwa? au pension zao hazitakatwa wakistaafu?
Mkuu hujui excitement tunayoipata deni likikaribia kuisha. Mi naona iendelee hiyo ili tumalizane na hayo madeni.
Nafikiri hoja kubwa sio 15% tu, ukisoma vizuri hizo hoja utaona kuna kitu hapo kinaitwa retention fees na hicho ndio kinalalamikiwa zaidi ukiachilia hiyo 15%
 
nmependa post hii mana wengi hawaelewi haya mambo. daaah yan kwel hii nchi ya wanyonge asee.
BTW, naomba nielekeze n wapi ntapata haya marekebisho ya sheria mf,,sheria za kodi,,sheria za makosaa ya jinai,uwiz wa kuaminika,, n.k mana mambo kama haya mfano mambo ya HESLB huez yakuta kwny katiba lakn unaambiwa tu kuna marekebisho yalifanyika mwaka fulani
 
Sasa hata ikipunguzwa kwa 8% au 10% wadaiwa hawatokufa na madeni makubwa? au pension zao hazitakatwa wakistaafu?
Mkuu hujui excitement tunayoipata deni likikaribia kuisha. Mi naona iendelee hiyo ili tumalizane na hayo madeni.
Mkuu jitahidi kuasoma na kuelewa vizuri, kuna vitu vinne:
Kwanza tozo ya administration fee
Pili kuna tozo ya penalty
Tatu kuna 15% makato ya kila mwezi
Nne kuna tozo ya 6% value retention fee (VRF) ambayo inaongezeka kila mwaka ya kwa kiasi cha mkopo uliobaki. Sasa mada hii inazungumzia tatu na nne.
 
Obviously kuna errors kwenye sheria ama tafsiri..

Muhimu ni kuwepo na sheria mpya
Na makato yapunguzwe
 
Not fair sema no way Kama kwenu Amna nguvu ya kusomeswa bila loan..
Ndomaana watu wengi wanaomba kupata mkopo ili ndoivo n shida badae.
 
Washenz hawa hata mpaka sasa Rais kaitoa hiyo VRF bado walaleta longongo
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom