Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Wamulikeni Watu Hawa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Masulupwete, Oct 30, 2012.

 1. Masulupwete

  Masulupwete JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 15, 2012
  Messages: 552
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Kumekuwa na kundi la vijana wake kwa waume kati ya 10 hadi 15 wanaweka meza pale ubungo darajani karibu na mitambo ya umeme ya songas na kujifanya wanachezesha kamari. Sina tatizo na mantiki ya mchezo huu kwa sababu nafaham ni mchezo unaokubalika kama unaendeshwa kwa kufuata sheria na taratibu zake. Tatizo ni namna wahusika hawa wanavyochezesha mchezo huu. Mara kadhaa nimekuta wakidhulumu watu kwa mbinu za ujanjaujanja na hata kukwapua pochi za watu wanaojaribu bahati yao kwa kucheza mchezo huu. Sina shaka, hawa si wachezesha kamari, bali ni kikundi cha wahuni wanaopaswa kuchukuliwa hatua badala ya kuachwa hapo wakiendelea ‘kuliza watu’.
   
Loading...