Bodi ya maziwa yazindua mpango wa unywaji maziwa kwa wanafunzi na watumishi wa serikali ili kuboresha afya za Watanzania

waziri2020

Member
May 31, 2019
58
125
Bodi ya maziwa yazindua mpango wa unywaji maziwa kwa wanafunzi na watumishi wa serikali nchini.

Wizara ya mifugo na Uvuvi kupitia Bodi ya Maziwa Tanzania, imeanza utekelezaji wa mpango wa unywaji wa maziwa kwa wanafunzi wa shule za msingi sanjari na ofisi za serikali ukiwa na malengo kuboresha Afya za wanafunzi pamoja na watumishi wa serikali nchini.

Akizungumza katika kikao cha kusaini makubaliano ya utekelezaji wa mpango huo Mkoani Arusha, Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania Noel Byamungu, alisema kuwa mpango huo kwa Sasa umeanza kwa majaribio kwa kuzihusisha shule 13 za msingi za Serikali (9)na binafsi (4)zenye zaidi ya wanafunzi 10,000 ambapo watatekeleza mpango huo kwa miezi 12.

Byamungu alisema kuwa shule zilizochaguliwa kuanza mpango huo wa unywaji maziwa,shuleni hizo zinatoka katika Halmashauri za wilaya za Arusha Jiji (8)Arumeru(2) na Longido 3.

''Shule hizo ni Upendo friends,Uhuru ,Longido,Namanga, Nalopa, Kaloleni, Meru, Shalom, Makumbusho, Usa River, Leganga, Tengeru English medium na St. Theresa zote ziko mkoani Arusha na makadirio ya wanafunzi elfu kumi ''Alisema.

Kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya maziwa ya Kilimanjaro Fresh ya jijini Arusha,Irfhan Virji ambao ndio watekelezaji wa mradi huo alisema kwamba malengo yao ni kuboresha afya za watanzania na kusaidia kukuza soko la uzalishaji wa maziwa nchini.

Virji,alisema kwamba mbali na kusambaza huduma ya maziwa mashuleni pia wanataraji kuweka friji mbalimbali za maziwa yao katika ofisi za serikali pamoja na mabenki kama njia mojawapo ya kutanua huduma wanayozalisha.

Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha David Lyamongi, alisema kuwa mipango huo ni fursa kwa wafugaji na wenye viwanda vya maziwa kujiongezea kiapato na kukuza Uchumi wa viwanda Nchini.

Lyakurwa alisema kuwa mpango huo umelenga kuwajengea watoto utamaduni wa kunywa maziwa, ili baadae kuwe na kizazi ambacho kutakuwa kinatumia maziwa na bidhaa zake, Kama sehemu ya maisha yao yao ya kila siku na kujenga Afya ya Akili na mwili.

Kwa upande wake mwanasheria kutoka bodi ya maziwa Tanzania Edwin Bantulaki, alisema kuwa Bodi ya maziwa nchini ndiyo chombo kikuu Cha kudimamia Tasnia ya Maziwa nchini hivyo imeamua kuingia makubaliano na kiwanda Cha Galax Food Beverages LTD kuuza maziwa shuleni.

Alisema kuwa malipo hiyo muuzaji atalipwa na kamati ya shule,atakuwa na jukumu la kupeleka maziwa shuleni pia atalipwa punde atakapokabidhi maziwa au atakapokabidhi maziwa awamu nyingine.

"Endapo shule husika itashindwa kulipa maziwa kwa muda uliokubaliwa kwa wamu mbili mfululizo Basi shule husika itahesabika kuwa imevunja makubaliano na itawajibika kulipa gharama zoye ambazo muuzaji atakuwa ameishia kw awakati huo" alisema mwanasheria wa Bodi ya maziwa Tanzania.

Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa shule waliopo kwenye mradi huo mwalimu Mwl.Mkuu wa shule ya msingi Longido Charles Efatha Mbando alisema kuwa wameupokea kwa mikono miwili, na kuwashirikisha wazazi kwa kutambua kuwa maziwa ni sehemu ya mlo kamili kwa watoto.

Mbando alisema kuwa kutokana na mpango wa unywaji maziwa kwa wanafunzi mashuleni, wanatarajia kwa mwaka 2021 idadi ya ufaulu kwa wanafunzi itakuwa juu kwani maziwa yanajenga Afya uelewa wa wanafunzi mashuleni.

Aidha mpango huu Mkoani Arusha ulianza tarehe 14 Januari 2021, wakati timu ya Bodi ya maziwa iliookutana na wataalam kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa Afisa (Mifugo, Afisa Elimu, Afisa Ustawi wa Jamii na Afisa Lishe) na wadau wa Elimu. Wazazi, wakuu wa shule na kamati ya Chakula ya Shule).

91F2B465-370A-48A5-9724-E17F98DD559F.jpeg
9C433245-6A12-4DA5-9289-FE6871049555.jpeg
45DBDCBD-0175-4638-B3CF-7354A307A073.jpeg
 
Joseverest

Verified Member
Sep 25, 2013
43,871
2,000
GOOD NEWS ILA WATULETEE MAZIWA OG (FRESH) SIO MNAYAPITISHA KIWANDANI, YANAPOTEZA UBORA WAKE KWA KUYAWEKEA MAKEMIKALI YA KUYATUNZA
 
Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
6,362
2,000
Summary:

Bodi ya Maziwa ikishirikiana na wafanya biashara wa Maziwa wana mpango wa kuwasogezea (na kuwalazimisha) wanafunzi na wafanyakazi wa serikalini wanunue na kunywa maziwa.

Mpango huu ni endelevu utasogezwa kwenye mabank, Mahospitali, Stendi na sehemu mbalimbali za mkusanyiko.

No free lunch in London.
 
jiwe angavu

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
2,789
2,000
Kuna bodi zingine sionagi faida yake kama hii..ingeunganishwa ikawa chini ya taasisi ya lishe..huu ni utawanyaji wa pesa tu za umna.

#MaendeleoHayanaChama
 
Root

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
38,823
2,000
GOOD NEWS ILA WATULETEE MAZIWA OG (FRESH) SIO MNAYAPITISHA KIWANDANI, YANAPOTEZA UBORA WAKE KWA KUYAWEKEA MAKEMIKALI YA KUYATUNZA
Umekariri
Maziwa packed hayawekewi kemikali. Yakipita kiwandani yanao dolewa vijidudu vyote kwa kutumia UHT
 
maruudaniel

JF-Expert Member
Dec 19, 2020
245
500
Bodi ya maziwa yazindua mpango wa unywaji maziwa kwa wanafunzi na watumishi wa serikali nchini.

Wizara ya mifugo na Uvuvi kupitia Bodi ya Maziwa Tanzania, imeanza utekelezaji wa mpango wa unywaji wa maziwa kwa wanafunzi wa shule za msingi sanjari na ofisi za serikali ukiwa na malengo kuboresha Afya za wanafunzi pamoja na watumishi wa serikali nchini.

Akizungumza katika kikao cha kusaini makubaliano ya utekelezaji wa mpango huo Mkoani Arusha, Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania Noel Byamungu, alisema kuwa mpango huo kwa Sasa umeanza kwa majaribio kwa kuzihusisha shule 13 za msingi za Serikali (9)na binafsi (4)zenye zaidi ya wanafunzi 10,000 ambapo watatekeleza mpango huo kwa miezi 12.

Byamungu alisema kuwa shule zilizochaguliwa kuanza mpango huo wa unywaji maziwa,shuleni hizo zinatoka katika Halmashauri za wilaya za Arusha Jiji (8)Arumeru(2) na Longido 3.

''Shule hizo ni Upendo friends,Uhuru ,Longido,Namanga, Nalopa, Kaloleni, Meru, Shalom, Makumbusho, Usa River, Leganga, Tengeru English medium na St. Theresa zote ziko mkoani Arusha na makadirio ya wanafunzi elfu kumi ''Alisema.

Kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya maziwa ya Kilimanjaro Fresh ya jijini Arusha,Irfhan Virji ambao ndio watekelezaji wa mradi huo alisema kwamba malengo yao ni kuboresha afya za watanzania na kusaidia kukuza soko la uzalishaji wa maziwa nchini.

Virji,alisema kwamba mbali na kusambaza huduma ya maziwa mashuleni pia wanataraji kuweka friji mbalimbali za maziwa yao katika ofisi za serikali pamoja na mabenki kama njia mojawapo ya kutanua huduma wanayozalisha.

Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha David Lyamongi, alisema kuwa mipango huo ni fursa kwa wafugaji na wenye viwanda vya maziwa kujiongezea kiapato na kukuza Uchumi wa viwanda Nchini.

Lyakurwa alisema kuwa mpango huo umelenga kuwajengea watoto utamaduni wa kunywa maziwa, ili baadae kuwe na kizazi ambacho kutakuwa kinatumia maziwa na bidhaa zake, Kama sehemu ya maisha yao yao ya kila siku na kujenga Afya ya Akili na mwili.

Kwa upande wake mwanasheria kutoka bodi ya maziwa Tanzania Edwin Bantulaki, alisema kuwa Bodi ya maziwa nchini ndiyo chombo kikuu Cha kudimamia Tasnia ya Maziwa nchini hivyo imeamua kuingia makubaliano na kiwanda Cha Galax Food Beverages LTD kuuza maziwa shuleni.

Alisema kuwa malipo hiyo muuzaji atalipwa na kamati ya shule,atakuwa na jukumu la kupeleka maziwa shuleni pia atalipwa punde atakapokabidhi maziwa au atakapokabidhi maziwa awamu nyingine.

"Endapo shule husika itashindwa kulipa maziwa kwa muda uliokubaliwa kwa wamu mbili mfululizo Basi shule husika itahesabika kuwa imevunja makubaliano na itawajibika kulipa gharama zoye ambazo muuzaji atakuwa ameishia kw awakati huo" alisema mwanasheria wa Bodi ya maziwa Tanzania.

Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa shule waliopo kwenye mradi huo mwalimu Mwl.Mkuu wa shule ya msingi Longido Charles Efatha Mbando alisema kuwa wameupokea kwa mikono miwili, na kuwashirikisha wazazi kwa kutambua kuwa maziwa ni sehemu ya mlo kamili kwa watoto.

Mbando alisema kuwa kutokana na mpango wa unywaji maziwa kwa wanafunzi mashuleni, wanatarajia kwa mwaka 2021 idadi ya ufaulu kwa wanafunzi itakuwa juu kwani maziwa yanajenga Afya uelewa wa wanafunzi mashuleni.

Aidha mpango huu Mkoani Arusha ulianza tarehe 14 Januari 2021, wakati timu ya Bodi ya maziwa iliookutana na wataalam kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa Afisa (Mifugo, Afisa Elimu, Afisa Ustawi wa Jamii na Afisa Lishe) na wadau wa Elimu. Wazazi, wakuu wa shule na kamati ya Chakula ya Shule).

View attachment 1715765 View attachment 1715766 View attachment 1715767
Naomba kujua kwa Dar ofisi zao ziko wapi?
Kwani mm nimeanza Biashara ya kuuza Mtindi hapa Dar.
Nataka kujua tarabu zao kwani kuna mambo nakutana nayo nadhani wao ni jibu kwangu
 
Mnyatiaji

JF-Expert Member
Dec 13, 2018
1,888
2,000
Kama sijakosea miaka ya nyuma kidogo kabla ata ya 2014 program kama hii ilianza sijui ilifia wapi
 
marxlups

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
14,821
2,000
Akizungumza katika kikao cha kusaini makubaliano ya utekelezaji wa mpango huo Mkoani Arusha, Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania Noel Byamungu, alisema kuwa mpango huo kwa Sasa umeanza kwa majaribio kwa kuzihusisha shule 13 za msingi za Serikali (9)na binafsi (4)zenye zaidi ya wanafunzi 10,000 ambapo watatekeleza mpango huo kwa miezi 12.

Byamungu alisema kuwa shule zilizochaguliwa kuanza mpango huo wa unywaji maziwa,shuleni hizo zinatoka katika Halmashauri za wilaya za Arusha Jiji (8)Arumeru(2) na Longido 3.
Wanafunzi hao watakunywa kwa niaba ya wengine🤣 na virutubisho vitasafiri kutoka kwa mwanafunzi mmoja hadi mwingine kwa njia ya osmosis
 
imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
26,954
2,000
Hivi Bodi ya maziwa inaongeleaje Ile Bodi ya Nyama kuwazulumu Wananchi nyama zao

Swali hilohilo liziendee Bodi za Chai na Chapati

Hii Nchi imekuwa na Bodi za ajabuajabu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom