Bodi ya Maziwa kuharibu maziwa ya ng'ombe kwa kuyamwagia mafuta ya taa

fundimchundo

JF-Expert Member
Jul 23, 2010
616
904
ITV leo asubuhi imemuonyesha Waziri wa Mifugo, Mhe. Luhaga Mpina akitoa maelekezo ya kuzuia vitendo vya KISHETANI vinavyofanywa na Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania kuchafua maziwa ya ng'ombe yanayouzwa na Wajasiriamali wanawake katika eneo la Ubungo kwa kuyamwagia mafuta ya taa, au rangi ili yasifae kutumika.

Maziwa hayo huwa yanauzwa yakiwa katika ndoo safi za plastic zenye mifuniko.

Najiuliza: Matendo ya Watendaji wa Bodi ya Maziwa ya kutumia pesa za Umma kwa kununua mafuta ya taa na kwenda kuyamwaga juu ya maziwa na hivyo kuwahujumu Wajasiriamali, tena akina mama, hakina ujinai ndani yake?
 
Tukisema CCM ni CHAMA CHA MASHETANI muwe mnatuelewa jamani
Hata kichaa huwa anasema lakini asemayo ni pumba.

Hata Mbowe alisema watu wasiojulikana kumbe ni Konyagi.

Kwahiyo kusema sema wakati mwingine bila kuwaza ni sawa na ukichaa
 
Taarifa yako Kama imekaa kishabiki hivi? Kwanini yamwagiwe mafuta ya taa?
Hakuna ushabiki maana hii ni taarifa ya ITV ya saa 12.00 asubuhi, Ijumaa tarehe 26.6.2020.
Waziri wa Mifugo amefika Ubungo, sehemu yanapouzwa hayo maziwa saa 11.00 alfajiri, akakutana na akina mama wauza maziwa, kisha Msajili wa Bodi ya Maziwa, akiwa na Mtumishi mwenzake mmoja wakasema ni kweli wanamwagia mafuta ya taa kwenye maziwa na kuyatia rangi ili yasitumiwe na binadamu.
Kosa lililotajwa ni kwamba kuna kifungu cha sheria kinasema maziwa yauziwe kwenye 'container' ya aluminium.
Hawa wanauzia kwenye ndoo za plastic.
Watumiaji wote wa maziwa nchini tunahifadhi maziwa kwenye ndoo za plastic.
Kwa Bodi ya Maziwa, adhabu yetu ni kumwagiwa mafuta ya taa.
Tena yaliyonunuliwa kwa kodi zetu.
Kwa bahati nzuri Waziri Mpina amepiga marufuku tabia hiyo ya kuwahujumu hao akina mama Wajasiriamali.
Swali langu, hao Watumishi wa Bodi ya Maziwa, hawastahili kupelekwa Kisutu?
 
Watoe taarifa inayoeleweka na ufanunuzi yakinifu wananchi waweze kuwaelewa.

Kwamba maziwa yakiuziwa kwrnye ndoo za plastic yana madhara gani kwa binadamu? Siyo kutoa tu marufuku, watanzania wote waelewe!

Na kama kuna madhara mbona vifungashio vya hayo maziwa ni plastic na vimejaa kwenye Supermarkets na mafuka mengi tu ya rejareja? Je, TFDA wanalijua hilo na wanapita kwenye hzo supermarkets?

Kama kuna madhara basi Watanzania wengi sana watakuwa wamedhurika!!
 
Hii nchi imerogwa hii.
 
Tukisema CCM ni CHAMA CHA MASHETANI muwe mnatuelewa jamani
Na shetani mkuu ni huyu hapa!
1592575.jpg
 
ITV leo asubuhi imemuonyesha Waziri wa Mifugo, Mhe. Luhaga Mpina akitoa maelekezo ya kuzuia vitendo vya KISHETANI vinavyofanywa na Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania kuchafua maziwa ya ng'ombe yanayouzwa na Wajasiriamali wanawake katika eneo la Ubungo kwa kuyamwagia mafuta ya taa, au rangi ili yasifae kutumika.

Maziwa hayo huwa yanauzwa yakiwa katika ndoo safi za plastic zenye mifuniko.

Najiuliza: Matendo ya Watendaji wa Bodi ya Maziwa ya kutumia pesa za Umma kwa kununua mafuta ya taa na kwenda kuyamwaga juu ya maziwa na hivyo kuwahujumu Wajasiriamali, tena akina mama, hakina ujinai ndani yake?
Tanzania tuna import maziwa yenye thamani ya zaidi ya bil 500 kila mwaka ikiwamo maziwa ya azam yakitokea India na kuwa reconstituted.

Bodi ya maziwa walau ingejenga platform/bridge ili tuongeze capacity ya kuzalisha maziwa kama hao wauzaji wa ubungo na kuchakata pia.

Kwanini tunakosa innovators kwenye bodi za muhimu kama maziwa, kahawa, korosho. Labda niseme kitu, mara nyingi sana bodi huwa zinaongozwa na wastaafu au watu ambao wanakaribia umri wa kustaafu.
Ningeshauri kwa baadhi ya bodi maziwa na vijana wenye maono ya namna gani tunaweza ku-invent the wheel.

Bodi inge-open avenue ya kuwa na policy na kushirikiana na wizara ya mifugo na wizara ya fedha ili kuziba pengo la ku-import UHT milk kwa kuhakisha uzalishaji unafanyika ndani.

Watanzania wenye uwezo wa kuanzisha miradi kama hii tupo, fedha za uwekezaji mwaka jana zimebaki nyingi tu TIB kwa mujibu wa waziri wa fedha wakati anasoma bajeti. Wangeondoa urasimu kwenye access ya investment credit, nchi hii ingekuwa kwa haraka kiuwekezaji na kuwapa Watanzania unafuu wa bei ya maziwa badala ya kutegemea imports.

1593218665030.png

Hii ni moja ya falsafa ya uongozi ambapo hata bodi ya maziwa wanawajibika kutafuta uhitaji wa watu/wadau kwenye sekta ya maziwa ili kuikuza sekta ya maziwa.
 
Watoe taarifa inayoeleweka na ufanunuzi yakinifu wananchi waweze kuwaelewa.

Kwamba maziwa yakiuziwa kwrnye ndoo za plastic yana madhara gani kwa binadamu? Siyo kutoa tu marufuku, watanzania wote waelewe!

Na kama kuna madhara mbona vifungashio vya hayo maziwa ni plastic na vimejaa kwenye Supermarkets na mafuka mengi tu ya rejareja? Je, TFDA wanalijua hilo na wanapita kwenye hzo supermarkets?

Kama kuna madhara basi Watanzania wengi sana watakuwa wamedhurika!!
Maziwa ya mgando ya Tanga Fresh na Asas yanauzwa madukani yakiwa katika vifungashio vya plastic.
Iweje ndoo za plastic ziwe haramu, lakini vifungashio viwe halali?
Katika hatua nyingine, Msemaji wa Wizara ya Mifugo ametangaza kwamba Waziri Luhaga Mpina ametengua uteuzi wa Msajili wa Bodi ya Maziwa aliyekuwa anaongoza zoezi la kumwagia mafuta ya taa kwenye maziwa kuanzia jana tarehe 26 Juni 2020.
 
Back
Top Bottom