Lee
JF-Expert Member
- Jul 31, 2013
- 43,901
- 150,180
- Thread starter
- #21
Mkuu umeongea ukweli , ila siku ya mechi bendi ilikuwa inajipanga kupiga gwaride sijajua kiongoz gani alikuwa anatarajiwaKwahiyo kwa mara nyingine, Bodi ya LIgi wanathibitisha kwamba hapakuwa na mashauriano yoyote kati ya vilabu na TFF licha ya kutambua walitaka kupeleka mechi mbele kinyume na kanuni!!
Yaani, TFF walikosa kabisa busara ya kukutana na timu zote mbili ili kujadiliana na kutoa sababu zao ni kwanini mchezo upelekwe mbele kinyume na kanuni inayosema taarifa ay kupeleka mchezo mbele inatakiwa kutolewa angalau saa 24 kabla ya tarehe ya mchezo iliyopangwa mwanzo!!
Bila kujali TFF walipokea maelekezo kutoka kwa nani, ukweli ni kwamba ni wao ndio wanaotakiwa kubebeshwa msalaba!!
Inawezekana Mama SSH (PLEASE, THIS'S JUST MY ASSUMPTION) alitaka kwenda kuosha macho pale Benjamin Mkapa, nae akawasiliana na wizara husika ambayo nayo wakaiagiza TFF moja kwa moja au kupitia BMT!
Na kama sio SSH basi watu kama akina P. Mpango ambao wanajinasibisha na ushabiki wa timu hizi mbili! Inawezekana kuingiliana huku kwa ratib kulitokana na baadhi ya hawa Waheshimiwa kuwa kwenye uzinduzi wa kitabu cha Mzee Mwinyi, na ili yeyote miongoni mwao aweze kushiriki sehemu zote mbili, ikaonekana tukio la kupeleka mbele ni lile ambalo lilikuwa halijaanza... yaani Simba SC vs Yanga SC Match!
Kwavile si TFF wala wizara wangehoji nia hiyo ya SSH, ndipo TFF nao bila kufuata taratibu wakaamua kuagiza timu kuhusu mabadiliko hayo badala ya kujadiliana nao!
Kama hisia zangu kuhusu SSH au mtu mwingine yeyote anayekaribiana na yeye kimamlaka zinakaribia na ukweli, na endapo TFF wangeziita timu zote mbili kuwaeleza sababu ndo hiyo, I AM SURE, kwa kuheshimu Mamlaka ya Rais, pasingekuwa na timu ya kupinga, na kwahiyo kungekuwa na makubaliano ya pamoja ya kupeleka mchezo mbele!!