Bodi ya Ligi yatoa tamko kuhusu sakata la mechi ya Simba na Yanga

Lee

JF-Expert Member
Jul 31, 2013
43,905
150,212
Kile kilichotokea Jumamosi ya tarehe 8 na kauacha sintofahamu mpaka mda huu idara husika zinazidi kuchanganya wapenda kabumbu kwani TFF wanadai ilipokea taarifa kutoka bodi ya ligi leo hii bodi ya ligi inadai TFF, tusubirie kikao cha leo.

Subpost%201%20-%20TAARIFA%20YA%20BODI%20YA%20LIGI%20KUU_%20.jpg
Subpost%202%20-%20TAARIFA%20YA%20BODI%20YA%20LIGI%20KUU_%20_Kamati%20ya%20saa%2072%20itakutana...jpg
 
Bado ya ligi, twambie sababu hasa ya kusogeza muda wa mechi hiyo mbele kwa masaa mawili, TFF walisema al-shabab wameshafika uhasibu au kimbunga Jobo kiko kigamboni tayari? Hayo ndiyo tunataka kujua.

Twambie vilabu yaani Simba na Yanga mliwapa taarifa kwa maandishi au kwa mdomo tu.

Twambie vilabu vilikubali ana nanyi kwa maandishi au kwa mdomo tu!

Tuwaambie uamuzi wa kuahirisha mechi umetokana na kikao gani?

Tuwaambie, Yanga walivunja kanuni au la! Kama hawajavunja kanuni kwanini wasipewe point zao.

Twambie Kuwa Simba walidanganywa kwa kuambiwa mechi ni saa 1 badala ya saa 11 nao wakakubali kwakuwa wao wakisaidiwa na mzee wao Ismail Rage Ni wataalamu wa sheria za soka, imekuwaje waingize choo cha kike?

Mengine endeleeni!
 
Kwahiyo kwa mara nyingine, Bodi ya LIgi wanathibitisha kwamba hapakuwa na mashauriano yoyote kati ya vilabu na TFF licha ya kutambua walitaka kupeleka mechi mbele kinyume na kanuni!!

Yaani, TFF walikosa kabisa busara ya kukutana na timu zote mbili ili kujadiliana na kutoa sababu zao ni kwanini mchezo upelekwe mbele kinyume na kanuni inayosema taarifa ay kupeleka mchezo mbele inatakiwa kutolewa angalau saa 24 kabla ya tarehe ya mchezo iliyopangwa mwanzo!!

Bila kujali TFF walipokea maelekezo kutoka kwa nani, ukweli ni kwamba ni wao ndio wanaotakiwa kubebeshwa msalaba!!

Inawezekana Mama SSH (PLEASE, THIS'S JUST MY ASSUMPTION) alitaka kwenda kuosha macho pale Benjamin Mkapa, nae akawasiliana na wizara husika ambayo nayo wakaiagiza TFF moja kwa moja au kupitia BMT!

Na kama sio SSH basi watu kama akina P. Mpango ambao wanajinasibisha na ushabiki wa timu hizi mbili! Inawezekana kuingiliana huku kwa ratib kulitokana na baadhi ya hawa Waheshimiwa kuwa kwenye uzinduzi wa kitabu cha Mzee Mwinyi, na ili yeyote miongoni mwao aweze kushiriki sehemu zote mbili, ikaonekana tukio la kupeleka mbele ni lile ambalo lilikuwa halijaanza... yaani Simba SC vs Yanga SC Match!

Kwavile si TFF wala wizara wangehoji nia hiyo ya SSH, ndipo TFF nao bila kufuata taratibu wakaamua kuagiza timu kuhusu mabadiliko hayo badala ya kujadiliana nao!

Kama hisia zangu kuhusu SSH au mtu mwingine yeyote anayekaribiana na yeye kimamlaka zinakaribia na ukweli, na endapo TFF wangeziita timu zote mbili kuwaeleza sababu ndo hiyo, I AM SURE, kwa kuheshimu Mamlaka ya Rais, pasingekuwa na timu ya kupinga, na kwahiyo kungekuwa na makubaliano ya pamoja ya kupeleka mchezo mbele!!
 
Bado kuna mchawi anafichwa na mimi ndio namtafuta kweli, taarifa imeshindwa kujibu swali la msingi kwa nini mchezo ulisogezwa mbele? ili kama Yanga SC walikosea waadhibiwe, au kama Simba SC walikosea waadhibiwe, na kama kosa ni la TFF au Bodi ya ligi tujue.
 
Back
Top Bottom