Bodi ya Ligi yamsimamisha Kelvin Yondani huku suala lake likipelekwa kamati ya nidhamu

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Kufuatia kitendo cha mchezaji wa Yanga Kelvin Yondani kutemea mate Asante Kwasi wa Simba SC, Aprili 29 katika mechi namba 178 kwenye patashika ya mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara (VPL), mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura, ametangaza kusimamishwa kucheza mpira huku suala lake likipelekwa kwenye kamati ya nidhamu litakapotelewa uamuzi.
FB_IMG_1525347410939.jpg
 
Hongereni kwa kuelekea kwenye maamuzi ya adhabu. Mpira si vita
 
Ni jambo la kushangaza sana kwa Mchezaji kama Yondani kwa uwezo wake na uzoefu kufanya ujinga wa kiasi kile tena kwenye Mechi kubwa kama ile ya Watani wa Jadi..,
Ngoja apumzishwe kidogo ili azidi kujifunza!!!
Tena siku hiyo alikuwa kapteni kabisa.
 
Unamuadhibu kwanza halafu unasikiliza kesi bongo bana
Mkuu naona msumari umeingia. Hivi unakumbuka Abi Banda, tukipinga kitu Simba SC tunakuwa na mtanzamo wa mbele kuwa huenda kesho ikaja upande wako wakapata adhabu hizi za ajabu. Kwa hivyo vumilia tu
 
Mkuu naona msumari umeingia. Hivi unakumbuka Abi Banda, tukipinga kitu Simba SC tunakuwa na mtanzamo wa mbele kuwa huenda kesho ikaja upande wako wakapata adhabu hizi za ajabu. Kwa hivyo vumilia tu
Sipingi mtovu wa nidhamu kuadhibiwa, napinga mtu kusimamishwa ndiyo kamati ya nidhamu ikae
 
Back
Top Bottom