Travelogue_tz
JF-Expert Member
- Sep 28, 2010
- 855
- 1,224
Bodi ya Kimataifa ya Ushauri kwa Bodi na Watendaji wa Barrick iliundwa kwa lengo la kutoa ushauri katika Nyanja za kisiasa, kijografia na masuala mbalimbali ya kimkakati yanayoweza kuathiri uendeshaji wa kampuni.
Ni wazi kwamba Barrick kama Mwanahisa Mkubwa (Majority shareholder ) wa Acacia, inayomiliki zaidi ya hisa asilimia 60 inaathirika zaidi na mgogoro unaoendelea kati ya Acacia na Serikali ya JPM.
Kwa mujibu wa malengo ya uanzishwaji wa Bodi, moja ya kazi zake kuu ni kuishauri Bodi ya Wakurugenzi na watendaji katika kutatua migogoro na hivyo kuhakikisha kampuni inajiendesha kwa faida na hivyo kulinda Imani ya wanahisa na wadau mbalimbali kwa kampuni.
Bila shaka katika hili la Zuio la Mchanga, Ripoti ya Prof. Mruma, kushuka kwa mapato ya Acacia, kuporomoka kwa thamani ya hisa zake katika masoko ya hisa ya dunia ni lazima litapelekea wajumbe hawa muhimu kukaa na kutoa maelekezo kwa Bodi ya Wakurugenzi au kufanya jambo kutokana na uzoefu na ushawishi wao.
Safu ya wajumbe hawa imesheheni watu maarufu, wanasiasa wenye ushawishi zaidi duniani na historia mbalimbali, mambo yanayofanya mgogoro huu kuwa na dhana ya umakini wa Tanzania katika kufikia malengo yake.
Wafuatao ni baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Kimataifa ya Ushauri na wasifu wao;
1. Mwenyekiti ni Hon. Brian Mulroney ambae amewahi kuwa Waziri Mkuu wa Canada kati ya Mwaka Prime Minister 1984-1993
2. Mh.. José María Aznar ( Mjumbe) ambae amewahi kuwa Waziri Mkuu wa Hispania kati ya Mwaka 1996-2004.
3. Hon. John R. Baird( Mjumbe) ambae amewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada kati ya Mwaka 2011-2015
4. Gustavo A. Cisneros ( Mjumbe) , ambaye ni mfanyabiashara maarufu Nchini Dominica na Mwenyekiti wa Makampuni ya Cisneros Group of Companies
5. Secretary William S. Cohen( Mjumbe) ambae amewahi kuwa Seneta wa Marekani kati ya Mwaka 1979-1997 na pia Waziri wa Ulinzi wa Marekani kati ya Mwaka 1997-2001
6. Mhe. Newt Gingrich ( Mjumbe) , amewahi kuwa Spika wa 50 wa Bunge la Wawakilishi la Marekani (Speaker of the House of Representatives) kati ya Mwaka 1995-1999. Mwaka 2012, Gingrich alikuwa Mmoja wa watafuta uteuzi wa nafasi ya Urais ndani ya Chama cha Republican. (https://en.wikipedia.org/wiki/Newt_Gingrich)
7. Mhe.Karl-Theodor zu Guttenberg ( Mjumbe), amewahi kuwa Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani kati ya Mwaka 2009-2011.
8. Mhe. Lord Charles Powell of Bayswater KCMG( Mjumbe), ambae amewahi kuwa mshauri wa sera wa mambo ya nje wa Waziri Mkuu wa Uingereza Margaret Thatcher 1983-1991.
9. Mhe. Vernon E. Jordan, Jr. ( US) , ambae amewahi kuwa mshauri wa karibu wa masuala ya sheria wa Rais wa Marekani bwana Bill Clinton kati ya mwaka 1992-1993, mbali na hilo Vernon anatajwa kuwa Mfanyabiashara maarufu na Mtetezi wa haki za binadamu mwenye ushawishi mkubwa katika siasa za Marekani. Pia amehusika kwa kiwango kikubwa katika kashfa ya ngono maarufu kama Clinton–Lewinsky scandal.
10. Wengine ni Andrónico Luksic (Chile), Peter Munk
Canada (Founder and Chairman Emeritus, Barrick Gold Corporation) na John L. Thornton
United States (Executive Chairman, Barrick Gold Corporation).
NB: Andiko hili halina lengo la kuwakatisha tamaa, bali kufahamu vizuri adui yako, na pengine inaweza kuamua aina ya mbinu inayoweza kutumika kufikia ushindi.