Bodi ya Filamu yasitisha usambazaji wa Filamu ya “Imebuma”

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,879
6,356
1.JPG
Bodi ya Filamu Tanzania imesitisha usambazaji wa filamu ya “Imebuma” mpaka pale maudhui yake yatakapofanyiwa marekebisho.

Akisitisha usambazaji wa filamu hiyo, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi Joyce Fisso amesema mtengenezaji wa filamu hiyo hana kibali cha kutengenza filamu kutoka Bodi ya Filamu na hajazingatia Sheria na kanuni za utengenezaji wa filamu.

Bi Joyce Fisso amesema filamu hiyo imesitishwa kwenda sokoni kutokana na kukiuka vifungu vya kanuni za sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza ya mwaka 2011 ambayo inakataza kuonesha namna yoyote ya udhalilishaji wa kibinadamu katika filamu na maigizo.

“Baada ya kuangalia kwa makini filamu hii na kuona mapungufu ambayo yanakinzana na Kanuni za Sheria ya filamu na Michezo ya kuigiza nimeamua kuisitisha usambazaji wake mpaka pale wahusika watakaporekebisha maudhi yake” Alisema Bi Joyce.

Bi Joyce amefafanua kuwa filamu hiyo imeonesha baadhi ya matukio ya udhalilishaji wa kibinadamu, ushawishi wa matendo ya ngono na ushoga ambayo ni kinyume na madili ya mtanzania.

Aidha kwa upande wake Afisa Utamaduni kutoka Bodi ya Filamu Tanzania Bw. Julius Tairo amewataka waandaaji na waigizaji wa filamu nchini kufanya utafiti wa kutosha kuhusu maudhui ya filamu kabla ya kutengeneza ili kuondokana na utengenezaji wa filamu zisizofata Sheria na kanuni za utengenezaji wa filamu Tanzania.
 
Kama ina mambo ya ushoga naunga mkono ipigwe marufuku lakini sio kumfungia msanii kama waziri alivyofanya kwa msanii wa wimbo wa chura
 
Mtu anakaa chini naku tunga vilamu zaki shoga upuzi kabisa.

Ila kama zina shawishi hayo mambo hivi wanao zikagua huwa hawa shawishiki.??.
 
Kwahiyo imebuma rasmi. Halafu mtu unaanza kutengeneza filamu ina ushoga ndani yake kama na wewe si muhisika kweli? Wasiruhusu kabisa hiyo kitu
 
Kama ina mambo ya ushoga naunga mkono ipigwe marufuku lakini sio kumfungia msanii kama waziri alivyofanya kwa msanii wa wimbo wa chura


Chura amekuwa akirudiarudia makosa yake ana maonyo mengi tu jaribu kuzikumbuka nyimbo zake zilizopigwa ban anashindana na serikali kwa nn haachi hayo mambo na kuzihurumia pesa zake anowekeza huko kwa kitu kisicho na manufaa?
 
Back
Top Bottom