BODI YA CHAKULA NA DAWA ZANZIBAR YAANGAMIZA TANI 520 ZA SUKARI ISIYOKUWA NA KIWANGO.

maimonides1

Member
Oct 13, 2018
13
45
Na Maryam Kidiko - Maelezo. 02.03.2019

Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda Hassan Khamis Hafidh amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itachukuwa hatuwa kali kwa Mfanyabiashara yoyote atakaeingiza bidhaa isiyokuwa na kiwango kwa ajili ya matumizi ya wananchi.

Aliyasema hayo Bandari ya Malindi Zanzibar alipofika kuangalia zoezi la kuhamisha tani 520 za sukari kwenda kuangamizwa kwenye mashimo ya mchango katika kijiji cha Zingwezingwe baada ya kugundulika kukosa kiwango kwa matumizi ya binaadamu.

Alisema kuwa Serikali ipo makini kulinda afya za Wananchi wake hivyo haitakubali kuingizwa bidhaa yoyote isiyofaa kwa matumizi ya wananchi ili kuwaepusha na maradhi.

Aidha alisema ulinzi mkali wa vikosi vya ulinzi na usalama umeandaliwa kwa ajili ya kusimamia sukari hiyo ili kuhakikisha hakuna mtu atakaefanya mbinu ya kuipata mpaka zoezi zima la kuiangamiza limalizike.

Aliwataka Wafanyabiashara kuendesha biashara zao kwa njia za halali na kuacha tabia ya kununua bidhaa za gharama nafuu bila ya kuangali ubora wake kwa lengo la kutafuta faida kubwa.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Chakula na Dawa Dk. Khamis Ali Omar alisema Makontena 20 ya sukari isiyo na kiwango yenye uzito wa Tani 520 ya Kampuni ya Rashid Ali Trader yaliingizwa Zanzibar mwaka uliopita kwa awamu mbili na alipewa tahadhari kuhusu tatizo la sukari hiyo alipoingiza kwa mara ya kwanza lakini aliendelea kuiingiza.

Alisema baada ya sukari hiyo kufanyiwa uchunguzi ilionekana haina kiwango na kuchukuwa hatua za kisheria ili isiweze kufika kwa wananchi kwa matumizi mbali mbali.

Alisema baada ya kugundulika kasoro hiyo, mmilikiwa huyo Rashid Ali alishauriwa kuirejesha ilikonunua ama kuiingamiza lakini mashauri yote mawili aliyakataa.

Katika siku ya kwanza ya zoezi la kuangamiza sukari hiyo katika mashimo ya mchanga ya Zingwezingwe makontena matatu kati ya 20 yaliharibiwa chini ya ulinzi mkali wa vikosi vya ulinzi na usalama

Kwa Upande wake Mrakibu Muandamizi wa Jeshi la Polisi Khamis Ramadhan alisema zoezi la kusafirisha sukari hiyo kutoka Bandari ya Malindi na kufika katika sehemu ya kuangamizwa limeenda vizuri na hakuna tatizo lolote lililojitokeza hadi lilipomalizika kwa siku ya kwanza.

Alisema zoezi hilo lililoongozwa na maafisa wa Bodi ya Chakula na Dawa Zanzibar limeshirikisha Vikosi vya Ulinzi na Usalama na wafanyakazi wa kitengo cha Mazingira Zanzibar.
IMG-20190303-WA0002.jpeg
IMG-20190303-WA0003.jpeg
IMG-20190303-WA0004.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom