Bodi ya atcl ni batili!! Mh waziri omary tunaomba bodi mpya


P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Messages
39,842
Likes
8,660
Points
280
P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2007
39,842 8,660 280
Kumezuka system ya Bodi kuendelea kufanya kazi huku zinaisha muda wao..tumeona Bodi nyingi zilizoua makampuni yetu zimekuwa zikiachwa kuendelea bila kujulikana nini kinaendelea..hivi karibuni tuliona kuna baadhi ya bodi zilikuwa zimeisha mpaka wafanyakazi wakaja juu.....MoJA YA bODI ILIOISHA MUDA WAKE NI BODI YA ATCL

Ikiongozwa na aliekuwa waziri serikali ya Rais JK NYERERE (MAREHEMU) MUSTAPHA NYANGANYI
Bodi ya ATCL Kisheria imeisha tangu mwezi wa 4..Toka hapo aliekuwa waziri wa miundo mbinu
mh kawambwa amekuwa akihojiwa na kushindwa kutoa jibu zaidi ya kusema atatangaza bodi mpya muda si mrefu..kwa bahati mbaya ama nzuri kwa upande wa wana bodi waziri akamaliza muda wake na kuelekea kudai ubunge tena..kwa ajili ya kusubiri mjomba kumchagua tena..unaweza ona tuna serikali ya wapuuzi namna gani frm APRIL-NOV waziri ameshindwa kuchagua bodi ya kuongoza ATCL..IKUMBUKWE Bodi hii imelalalamikiwa sana ikigawana hela kama njugu na pengine kuweka maumivu kwa wafanyakazi kama ugonjwa wa kansa lakini bila kujali mpaka leo hii bodi hii inakaa kujadili shida na matatizo ya kampuni huku mwenyekiti akichukua cash doller 600 na wengine doller 500

Huu ni upuuzi ambao atuna haja ya kuendelea nao huku tukiona shirika likiendelea kufa...inashangaza kuona waziri aliechangia kuiua ATCL na TRL ati akipelekwa wizara ya elimu huyu kama ukimpa afya si anakuwekea SUMU??je kwa Kumekosekana na wana Bodi wa kuiongoza ATCL kweli??kwa nini tuwe na watu wanaojali na kuhifadhi matumbo yao bila kujali umuhimu wa watanzania..awajali wala kujua hata pesa wanazogawana ni za kodi za mtanzania..achlia mbali in doller bado wanakaa kila mwezi mara mbili wakati mwingine wakijiita emergency mtn mpaka 3

Mh Waziri tunaomba kama mmeamua kuikoa ATCL basi muwe wa kweli na unafiki atutaki kama vipi nenda kwenye wizara ya comedy & origin..wapo waliotishia adi kuiondoa Bodi..leo hii wako WIZARA YA ELIMU ...unaweza jua wanawapeleka wapi???

Tunaitaji bodi ya watu wanaojua ANGA na si kuletana ujombana ushangazi na umates kwenye maslahi ya umaa wa watanzania...tafadhali tutadili na wewe kwenye hili mpaka kieleweke mh..tunaitaji kuona Kampuni nyingi za ndege zikiruka na kwa bei rahisi bila kujali mashirika machahce yaliopo

Kila la kheri
 

Forum statistics

Threads 1,235,102
Members 474,351
Posts 29,212,403