Bodaboda waelimishwe zaidi fursa za kiuchumi

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,503
2,980
Chimbuko la bodaboda ni neno la Kingereza 'border' lenye maana ya mpaka. Baada ya Idi Amin kuipindua Serikali ya Rais Milton Obote mwaka 1971, Uganda ilikumbwa na uhaba wa bidhaa muhimu za nyumbani, hivyo kuanzia mwaka 1972 wajasiriamali wa Uganda walitumia baiskeli kuvusha bidhaa kama sukari, chumvi, unga na sabuni kutoka Kenya, eneo la Busia.

Usafiri huo wa baiskeli hutumika pia upande wa Tanzania na Kenya katika mpaka wa Holili na Taveta, kuvusha bidhaa na abiria. Baada ya pikipiki kuingia, wasafirishaji wengi waliachana kutumia pikipiki, lakini jina bodaboda likabaki na kusambaa mpaka maeneo ya mjini unakotumika zaidi usafiri wa pikipiki.

Pamoja na uwezeshaji kiuchumi unaofanywa kutokana na maelfu ya vijana kuajiriwa katika kazi ya bodada lakini ipo haja ya kuhakikisha kuwa bodaboda wanapata elimu sahihi ya usalama barabarani pamoja na na kutambua fursa za kiuchumi zilizo mbele yako kama mikopo pamoja na elimu ya biashara na uwekezaji

Sehemu ya andiko hili imetokana na habari katika Gazeti la Mwananchi

Boda.jpeg
na baiskeli na
 
Back
Top Bottom