Sami Omary Khamis
Member
- Sep 8, 2020
- 67
- 133
Turudi nyuma kidogo. Wafanyabiashara wadogowadogo mnakumbuka mateso mliyoyapata tena kwenye ardhi yenu ya nyumbani Tanzania? Bodaboda, machinga na mama n'tilie. Mkabughudhiwa kufanya shughuli zenu kwenye maeneo flanflan ya nchi kama vile nyie sio binadamu na kwamba hamtakiwi. Yani kwenye ardhi ya Tanzania pakawa pana sehemu pakwenda kufanya biashara na pengine marufuku. Mkafukuzwa, kupokonywa bidhaa zenu na kutozwa misululu ya kodi na tozo kila siku bila huruma katu. Yani mkanyanyaswa vilivyo.
Kuingia kwa Rais John Pombe Magufuli mwaka 2015 akasema imetosha na hapana tena kunyanyasa wala kuonea wafanyabiashara wadogowadogo wala kuzuiliwa kufanya biashara maeneo flanflan, kutozwa hela na misululu ya kodi na kuonya uonevu wowote kwa wafanyabiashara wadogo na kwamba atakayejaribu atakiona.
Serikali ya Awamu ya 5 chini ya uratibu wake mwenyewe Rais John Pombe Magufuli akaanzisha utaratibu wa mmachinga kulipa elfu 20 tu kwa mwaka mzima kufanya biashara zake bila kusumbuliwa na kubughuziwa na mtu yeyote yule badala ya ile hali ya mmachinga na mama ntilie kumswekea msululu wa kodi na tozo anazotakiwa kulipa kila siku.
Kutoka utaratibu wa kulipa karibu kila siku ambao ukipiga mahesabu kwa mwaka mzima mmachinga au mama ntilie alifika kulipa mpaka zaidi ya Million, ikawa sasa unajipatia kitambulisho chako tu cha mjasiriamali kwa elfu 20 tu unafanya biashara zako kwa mwaka mzima bila fyoko na bughudha ya yeyote yule.
Hapo hujaenda kwenye mpango wa Serikali ya Rais Magufuli kutenga maeneo rasmi yenye ukubwa wa hekta 15,822.64 nchi nzima kwa ajili wajasiriamali wakiwemo mama lishe na wauza mbogamboga kufanya biashara zao na kuongeza upatikanaji wa mikopo yenye masharti nafuu kwa wafanyabiashara wadogo ambapo mfuko wa Small Entrepreneur Loan Facility (SELF) ambao umetoa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo yenye thamani ya shilingi billioni 26 na kutengeneza ajira 13,000 mpaka sasa.
Halafu aje mtu hapa kuanza kupiga longolongo, kunanga na kudanganya watu kuhusu mzigo na tabu hii ambayo Rais Magufuli ameitua kwa wafanyabiashara wadogo, tutamshangaa! Nani kama Magufuli eti? Kura zote kwa Dkt John Pombe Magufuli Oktoba 28.