Bodaboda, bajaji, na kero zingine Daresalaam...

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,871
Hivi viongozi wetu huwa hawasafiri na kuona miji mingine mikubwa

inavyo endeshwa????????

hivi hizi bodaboda zinavyo ongezeka na bajaji na kuzidisha kero jijini hapa
hakuna anaetazama na kuliona hili???????

hizi bodaboda zimeshakuwa' uchafu mtupu' halafu madereva wake ni jeuri na
hawajui sheria za barabarani...wanasababisha ajali na wao ndo wanakuwa wakali....

hivi kuna chombo kinacho regulate hizi bodaboda na bajaji?
ziko ngapi now daresalaam mfano? tutajuaje kuwa zimezidi mahitaji?
hivi ni lazima hili jiji liwe na boda boda na bajaji??????

mtu anaendesha gari,ghafla unakuta kulia kuna bodaboda na kushoto pia..
wakigongwa wanakuja juu na ugomvi....wameanza na tabia ya kuchoma magari wanapogongwa..
imetokea juzi tegeta.....

hivi hili jiji kuwa na ma meya zaidi ya sita na wakuu wa wilaya na mkoa inasaidia nini???????
 
Hao viongozi wanatembea kukicha hawakai nchini kwao lakini sijui hawaoni aibu?au ndio wasohaya wanamji wao, wanachumia matumbo yao na familia zao.....
 
Hizi bodaboda na bajaji kwa kweli zimekuwa kero, si Dar es salaam tu, ni karibu miji yote hapa nchini.
 
THE BOSS;nafikiri mradi wa vigogo fulani,haiwezekani jiji liwe na msongamano mkubwa wa magari halafu bado waruhusu haya mabodaboda na bajaj katikati ya jiji,yaani kuna sehemu huwezi kupita kama kkoo utapata ugonjwa wa moyo mara moja yaani bodaboda ikikukosa,basi either bajai itakugonga au mkokoteni aaaagh yaani mpaka jiji hili limepoteza kabisa hadhi yake,the only time peaceful ni usiku tu..
 
Acheni watu wapande maboda boda kama vipi wajengewe barabara zao. Usafiri wa boda boda upo poa sana.
 
wameunda chama chao cha kuwalinda wanasema wanaonewa...........yaani kero isiyopimika............usiombe itoke ajali wataitana zaidi ya 100 watafanya fujo bila kujua mwenye makosa ni nani......mpaka police wafike gari ishakuwa majivu au umepata kichapo hatari......inatakiwa kuangaliwa kwa jicho la 3 la sivyo wasiboziba ufa watajenga ukuta
 
Inaitajika Maboresho tu maana zinasaidia sana haswa sisi wenye vipato vya chini na hata kufika sehemu ambazo si rahisi kufikiwa kwa magari.
 
wameunda chama chao cha kuwalinda wanasema wanaonewa...........yaani kero isiyopimika............usiombe itoke ajali wataitana zaidi ya 100 watafanya fujo bila kujua mwenye makosa ni nani......mpaka police wafike gari ishakuwa majivu au umepata kichapo hatari......inatakiwa kuangaliwa kwa jicho la 3 la sivyo wasiboziba ufa watajenga ukuta

unayosema ni kweli, leo nimeshuhudia first hand tukio kama hilo, ilikuwa hivi,
wakati natembea kuelekea kazini asubuhi maeneo ya usalama wa taifa, makumbusho mara mbele yangu nikaona bodaboda kama nne zikiwa na abiria wa 3 kila moja zikija kwa kasi mbele yangu, huku wameshika mawe kuangalia pembeni naona kuna breakdown imebeba bajaji pamoja na gari ya ulinzi, inavyoonekana ndio iliyohusika kwenye ajali na bodaboda, bahati mbaya kwa yule dereva wa gari ambaye alikuwa amekaa nyuma kwenye breakdown kulikuwa na ka foleni na mvua ilikuwa imeanza kunyesha basi walivyomfikia wakaanza kumvuta na kumtoa kwenye breakdown, yule dereva akachomoka akakimbilia usalama wa taifa, bahati nzuri wanajeshi kama 6 hivi wakatoka wale maboda boda wakakimbia kurudi uelekeo wa mwenge. Na wakati wote kwenye msafara wa breakdown kulikuwa na trafick officer, hadi wale wanajeshi wakaanza kumkebehi.
Yaani hii nchi inaanza kuwa lawless, halafu waendesha boda boda wenyewe wanatisha kama ma rebel wa liberia au sierra leone.

ZIPIGWE MARUFUKU!!!
 
wameanza kuwa na sheria zao wenyewe hawa..
 
MMM BODA ZINASAIDIA SN UHARAKA WA SAFARI HAPA TOWN!TATIZO NI ULEGELEGE WA HAWA WANAUSALAMA BARABARANI
WANAPOKEA RUSHWA HOVYO NDOMANA WANASHINDWA KUDHIBITI HIZ BODA! KARIBU ASILIMIA 80 YA WAO MA BODABODA RIDERS HAWANA LESENI! WALA HAWAJUI SHERIA ZA BARABARANI,UNAMKUTA HAJUI SHERIA NA KUCHOMEKEA WAKWAnza kabeba mshkaki wa watu kibao hawana kofia na mwendo ni wa kasi!askari wanawaona,wakiwakamata wanawashkisha buku3 wanatambaa ndo mana ajali kila uchao
 
harley-davidson-steampunk-motorcycle-mod-design-2.jpg

hydraulicinnovations.jpg
 
the boss ingesaidia sana iwapo ungekuja na takwimu zinazoonyesha ongezeko la kero(mfano ajali) mara baada ya kuongezeka kwa bajaji,hii ingesaidia kuonyesha kuwa bajaji au toyo sio msaada bali ni maafa.bila kufanya hivi hawatakusikiliza kabisa.
 
THE BOSS;nafikiri mradi wa vigogo fulani,haiwezekani jiji liwe na msongamano mkubwa wa magari halafu bado waruhusu haya mabodaboda na bajaj katikati ya jiji,yaani kuna sehemu huwezi kupita kama kkoo utapata ugonjwa wa moyo mara moja yaani bodaboda ikikukosa,basi either bajai itakugonga au mkokoteni aaaagh yaani mpaka jiji hili limepoteza kabisa hadhi yake,the only time peaceful ni usiku tu..

Mkuu kwa kkoo umesahau kelele za majenereta na moshi wa majenereta ni kero tupu
 
Back
Top Bottom