FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 37,898
- 43,806
Nimepita hapa na kukuta damu kwenye lami Tabata relini ikiwa imefukiwa na mchanga.
Nasikia kuna wale wanaokamata Pikipiki walimvuta mkono na kwa bahati mbaya akaingia kwenye lori na kuminywa, nasikia amekufa.
Polisi wote wamekimbia. Mwenye taarifa athibitishe
UPDATE:
Nasikia kuna wale wanaokamata Pikipiki walimvuta mkono na kwa bahati mbaya akaingia kwenye lori na kuminywa, nasikia amekufa.
Polisi wote wamekimbia. Mwenye taarifa athibitishe
UPDATE:
Kuanzia mida ya asubuh pamekuwa na milio ya risasi huku askari wakikamata na kuwashambulia bodaboda
Chanzo ni kuwa kwa sasa kuna zoezi la kukamata bodaboda kama mnavojua linaendelea, sasa kuna bodaboda mmoja kituo cha hapa tabata Magengeni katika harakati za kuwa kimbia akagongwa na gari maeneo ya tabata relini akawa amefariki, baada ya kupasuka kichwa.
Sasa bodaboda wenzake wakaenda pale Buguruni wakawakamata askari wawili wanaozikamata wakawapiga sana ikabidi askari nao waanze kulipiza.
Mpaka muda huu bado mabomu ya machozi yanalia maeneo ya tabata shule huku bodaboda wakikimba huku na kule