BoD Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni yako

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,480
5,504
Habari za wakati huu;

Kwanza kabisa nitanguliza shukrani za dhati kwa mwenyezi Mungu kwa neema zake.Leo nataka tuzungumzie issue ya BODI ya kampuni na umuhimu wake.Kampuni nyingi private huwa zinafeli kwa sababu ya kuwa na BODI(BOARD ambayo ni pungufu)

Ni muhimu kwa mmiliki kwa mjumbe wa bodi lakini anao uwezo wa kuteua BOARD members ambao sio wamiliki lakini ambao watasaidia kampuni kufikia malengo yake.Kwa mfano unapounda kampuni ya Constructionni muhimu uwe na board member mmoja ambaye ama ni mdau wa sector au ni mtu nyeti katika sekta mfano kutoka katika taasisi za manunuzi za serikali au private.

Sheria inamkataza board member kutumia nafasi yake kufaidika na kampuni husika lakini haimzuii kufaidisha kampuni yake katika nafasi yake nyingine provided sio board member huko(Wanasheria watafafanua zaidi)

Kwa maana nyingine wewe ukiwa na board member ambaye Mtu mzito TANROADS basi unaweza kufahamu ya TANROAD mapema kuliko kampuni nyingine na hata ukawa na advantage.

Swali la kujiuliza je unaweza kumteua mtu awe BOARD member wa kikampuni chako kipya,utamlipaje?Ana mamlaka gani?Hayo ni maswala ambayo yanahitaji kujadiliwa zaidi na wadau humu ndani ila kadiri BODI ya kampuni inapokuwa na watu wenye influence ndivyo uwezekano wa kampuni kufanikiwa unaongezeka.

Nawatakieni kila heri katika mjada huu.
 
Uelewa wa watu katika hili unachangia mtu kuachana na kuteua board members. Mtu ukimuomba awe mjumbe wa board yako anakuwa kama kapata ajira full kukuegemea.
 
Uelewa wa watu katika hili unachangia mtu kuachana na kuteua board members. Mtu ukimuomba awe mjumbe wa board yako anakuwa kama kapata ajira full kukuegemea.
Kuwa Board member ni kazi na kila kikao lazima ujue kuwa wanatakiwa walipe.Unless unafikiri kwamba ni kujitolea.Kujitolea ni kwenye NGO.Kama board members wanaweza kukuwezesha kuingiza pesa zaidi kwa nini usiwalipe?
 
Na wewe pia uelewa wako hauko sawasawa.
 
Na wewe pia uelewa wako hauko sawasawa.
Mkuu inawezekana uelewa wangu hauko sawa.Unafikiri utamuita mtu aje kupanga na kuamua uelekeo wa kampuni yako with all related risk huku ukitaka ajitolee?SERIOUSLY.Cha muhimu ni kutafuta board members ambao wanajiweza ili waongeze thamni katika kampuni yako.
 
Kwanza hamna sehem kasema hao members wasilipwe au hawalipwi. So naungana na yeye kwa uelewa wako hauko sawa sawa!

Anachosema ni kwamba mtu ukimpa hiyo nafasi ni kila saa anakutegemea plus kuombwa ela kila siku...
 
Kazi ya board members ni kuoversee management, sasa itakuwa kitu cha ajabu kuweka board members including board chairperson wasiwe na ufanisi au ujuzi kwenye industry ambayo kampuni inaoperate.

Lakini pia ni vyema kuchagua watu ambao hawana maslahi na kampuni au watu wao wa karibu kuwa na maslahi ya kampuni.

Nimimi, chairlady wa XYZ Company.
 
Kwanza hamna sehem kasema hao members wasilipwe au hawalipwi. So naungana na yeye kwa uelewa wako hauko sawa sawa!

Anachosema ni kwamba mtu ukimpa hiyo nafasi ni kila saa anakutegemea plus kuombwa ela kila siku...
OOOOH unazungumizia vizinga?HIvyo hata mtu asipokuwa board member ni sehemu ya desturi za wabongo wengi so sidhani ni tatizo.Kwani unapotaka mtu awe mkurugenzi kwenye kampuni yako unaangalia vigezo gani hasa kwa huyo mtu?
 
Back
Top Bottom