Bobi Wine awasili Uganda apakizwa kwenye gari la jeshi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Kwa ufupi
Wakati polisi nchini Uganda wakionya mikusanyiko kwa ajili ya mapokezi ya mbunge wa Kyadondo, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, mwanasiasa huyo leo Septemba 20, 2018 amewasili nchini humo akitokea Marekani

By Mwandishi Wetu, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz
Kampala. Baada ya kuwasili Uganda akitokea Marekani alipokuwa akipata matibabu, Mbunge wa Kyadondo, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, amepakizwa kwenye gari la jeshi.

Mara tu baada ya kushuka kwenye ndege ya Kenya Airways, Bobi Wine, alipakizwa kwenye gari ya jeshi na kupelekwa kijijini kwake Magere.

Awali mwanamuziki huyo aliyegeuka mwanasiasa aliapa kukaidi amri hiyo iliyotangazwa mapema akieleza kuwa yeye ni raia huru wa Uganda mwenye haki zote za kutembea kokote hivyo asipangiwe nani ampokee na aende wapi.

Bobi Wine aliyekwenda Marekani kwa ajili ya matibabu baada ya kudai kupigwa na kuteswa wakati akiwa mikononi mwa polisi, amesema kurejea kwake Uganda hakuwahusu polisi, hawapaswi kuhoji nani atampokea.

"Nimekuwa najiuliza kwa nini hawa maofisa wa polisi wanakubali kujidhalilisha kiasi hicho. Wanataka kuamua nani aje kunipokea na wapi nielekee baada ya kuwasili?” Amehoji.

Vyombo vya habari nchini Uganda vimemnukuu msemaji wa polisi, Emilian Kayima aliyewaambia waandishi wa habari kuwa atakapowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Entebbe, mbunge huyo atapokelewa na familia yake na atapatiwa ulinzi kutoka uwanja wa ndege mpaka nyumbani.
42292956_1894104344003014_7184279005330145280_n.jpg
 
Mbunge machachali wa uganda anaye mnyima usingizi m7 amerejea leo mchana akitokea usa kwenye matibabu amepokewa kifalme na wana uganda huku vikosi vya jeshi vikimchukua kwenye gari la kijeshi,haya ni maandalizi ya jinsi atakavyo pokewa Lissu
FB_IMG_1537450345295.jpeg
FB_IMG_1537450395391.jpeg
 
Mbunge machachali wa uganda anaye mnyima usingizi m7 amerejea leo mchana akitokea usa kwenye matibabu amepokewa kifalme na wana uganda huku vikosi vya jeshi vikimchukua kwenye gari la kijeshi,haya ni maandalizi ya jinsi atakavyo pokewa LissuView attachment 872326View attachment 872327
Hahahaha
Tundulissumsaliti hamna mtu mwenye haja naye, hata chama chake nacho wamemchoka kwa kuwaita boys! Hovyo kabisa walahi!
 
Meet Lady Afande Kentalo Pamella who has been Spying on Hon Bobi Wine all the way from US to Amsterdam via Nairobi till Uganda .
Kampalafm.com
 
Back
Top Bottom